TANESCO
Official Account
- Jul 12, 2014
- 4,801
- 2,318
Ndugu mpendwa mtejaKwenye mtaa wangu ninaoishi hatuma umeme toka kuumbwa Kwa Dunia . tumejaribu kufuatilia toka mwaka Jana mpaka Leo hakuna hata dalili
Ila kuna mdau ametudokezea ili tuletewe umeme sharti tujikusanye wakazi wote wa huu mtaa tuchange kila mtu sh 200000 Kwa ajili ya nguzo
Bado kuvutiwa umeme kuingia ndani
Swali
Langu je ni halali kuuziwa nguzo sh 200000?
Au Mimi niendelee kutumia soral
Au tanesco wanatuibia ?
Naomba kuwakilisha kwenu mnisaidie
Sent using Jamii Forums mobile app
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) halina utaratibu wa kutoza pesa nje ya kiwango ambacho mteja anapaswa kulipa kupitia ofisi zetu au Bank zilizobainishwa. Aidha wapo watu wanajifanya ni wafanyakazi wa TANESCO ambao wanafanya udanganyifu kwa wateja wetu na kuwalaghai ili kujipatia fedha kinyume na sheria, hivyo basi kwa swala lako tunaomba utupatia taarifa zifuatazo ili tuweze kukupatia ufafanuzi wa eneo husika.
Namba ya simu?..........
Mkoa
Wilaya
Kijiji
Mtaa uliopo
Kwa taarifa hizi tutakupatia ufafanuzi stahiki mpendwa mteja
TANESCO HUDUMA KWA WATEJA
MAKAO MAKUU,SIMU 0768985100/0222194400
Sent using Jamii Forums mobile app