Tanesco!1 Mbezi Marambamawili tusaidie na sie tupate Nishati ya Umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco!1 Mbezi Marambamawili tusaidie na sie tupate Nishati ya Umeme

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mbano, Apr 23, 2012.

 1. m

  mbano Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana jamii mwenzangu.kweli naomba nilete kero hii hapa kwenu muweze kutupa mwongozo.sie wakazi wa Mbezi Maramba mawili tuna shida sana na umeme.tumeshaangaika sana kufatilia umeme tanesco ila wanatuhangusha sana.Wanzoni mwa mwaka 2008 tulienda kuomba umeme tukaambiwa mradi hauwezi kuja kwa sababu wakazi ni wachache, hapo tulikuwa wakazi zaidi ya 200.tukakubali mwakwaa 2010 tukaandika barua tena ya kuomba mradi tukanzungushwaa kweli kweli tukapewa kiswahili tu.
  2011/2012 tukakusanyika tena na kamati yetu ya umeme tukafatilia Tanesco tukaambiwa tufatilie tanesco kituo cha Mbezi mwisho.Tumefatilia kweli hapo mwisho wa siku hatukupata jibu linaloeleweka.tukadanganywa kwamba nguzo zipo ila hawana transforme.

  Sasa tupo wakazi zaidi ya 1500 tunaoishi Maramba mawilli stand ya basi mwisho.Umeme umeishia hapo Kifuru bjia ya kwenda Kinyerezi jirani kabisa na maramba mawili umbali wa 1KM na ukitokea mvezi umeme umeishia hapo msikitini umbali kidogo sana hata 1 Km haifiki.

  Tumeenda Tanesco kuwaomba tujivutie hata huwo wa jirani zetu Kifulu au msikitini hapo lakini tunakataliwa na Tanesco wanatwambia umeme mdogo hautoshelezi.Tusubilie wa mradi ambao tumeombea toka mwaka 2008 adi leo hii 2012 hawajatuletea uwo mradi.

  Maisha yamekuwa magumu sana kwa kukosa nishati ya umeme.matukio ya ujambazi yameongezeka kwa sababu ya Giza.Ukifika saa2 kupita njiani kuelekea Kinyerezi hatuwezi tunaogopa majambazi wanatumia mwanya wa Giza kufanya uhalifu.MBunge wetu John Mnyika taarifa tumeshakupatia ila hukuweza kuja hata kutusikiliza.Diwani wetu hata hatukufahamu sasa sie wananchi nani wa kutusaidi.
  Mwenyekiti serikali za mtaa nae kazi imemshinda anakesi kila siku na wananchi wapenda maendelea hatuna pa kukimbilie tumetengwa na serikali yetu.
  Miaka 50 ya uhuru lakini sie tupo gizani hadi leo hii.

  Tunaomba wahusika wa Tanesco watusaidi kutufikishia huduma hii ya umeme tafadhali.

  Wakazi wa Maramba Mawili.
   
 2. Kappa

  Kappa Senior Member

  #2
  Dec 3, 2013
  Joined: Feb 17, 2013
  Messages: 105
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bwana mbano hii ni december 2013, vipi umeme tayari huko? Nina mpango wa kupata eneo huko lakini hili swala la umeme limenipa mawazo sana. Kuna mwanga wowote? Na vipi kuhusu hali ya maji, maji yanapatikanaje?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. m

  mbano Member

  #3
  Jan 29, 2014
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  loh wamesha weka nguzo na wameshaanza kutantaza nyaya njoo tu mkuu.adi Feb wataanza kuvuta majumbani.
   
Loading...