Nguvu ya Umma yamshusha Katibu mkuu wa CCM juukwaani

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Katibu mkuu wa chama cha magamba Wilson Mukama jana alionja joto ya jiwe baada ya kuzomewa na wananchi wilayani Musoma mkoani Mara.
Mukama alipata dhahama hiyo baada ya kuisema vibaya chadema. Taarifa zinadai baada ya katibu huyo kuanza kuisema vibaya chadema wananchi walianza kuondoka na wale waliobaki walimzomea hadi alipoamua kushuka jukwaani.
:A S thumbs_up:

Source: Taarifa ya habari ITV jana.
 
Analeta usharoharo kwenye kazi,muraaa ningemkuta angejutaaa kuja musoma, anadhani ingekuwa ndiyo mzeee imekula kwao safari hii watahaha sana huu ndiyo mwisho wao muraa
 
Kwanini hawajampa dozi ya mawe?

Nadhani sehemu kubwa ya usalama wa taifa ilikuwa huko. Kwa hiyo nguvu ya umma ikaona ni bora kutumia sauti yao. Sauti ya nguvu ya umma ikawa kubwa kuishinda ile ya Mkama na magamba wenziye.
Tena akina Mkama wanadai Mbunge wa chadema Mh. Vincent Nyerere (Chadema) eti amewaibia madawati yao, na hapo ndipo walipochokoza nyuki.
 
Hiyo hata ITV waliitangaza walikwenda watu kibao kumpokea but kwenye mkutano woote waliiishia njiani!
HII AIBU YAO!
 
kule arusha wanadai eti mafisadi ndoo walio organize ile maandamano ya juzi.
sisi wana chama imara wa chadema hatujali kama ni mafisadi au ni wana ccm gani,
tunachojali ni kua asa tunaeleweka vyema kwa uma.
 
Mkama anatia huruma masiKIni na kile kipara chake na ndevu zake, jamani! Yeye si alisema ndiyo anaweza kuirudishia heshima CCM!?
 
kule arusha wanadai eti mafisadi ndoo walio organize ile maandamano ya juzi.
sisi wana chama imara wa chadema hatujali kama ni mafisadi au ni wana ccm gani,
tunachojali ni kua asa tunaeleweka vyema kwa uma.

Sawa kabisa mkuu.Kinachohitajika ni upinzani wa aina zote dhidi ya ccm. Na hapo kazi yetu cdm inakuwa rahisi sana hasa kuelekea 2015.
 
hii inazidi kunitia moyo kwamba sasa angalao baadhi yetu si lazima mtu fulani aje kutuambia kwamba fulani anatudanganya.
tumeanza kupata uwezo wa kupambanua mambo ijapokuwa tumechelewa sana.
 
du mambo magumu..... hata tbc hawakuleta report toka musoma mjini kama kawaida yao....tupeni taarifa kwa aliyekuwa mkutanoni mwa mukama magamba alisema nini kuhusu cdm?
 
du mambo magumu..... hata tbc hawakuleta report toka musoma mjini kama kawaida yao....tupeni taarifa kwa aliyekuwa mkutanoni mwa mukama magamba alisema nini kuhusu cdm?

Ukiona hata tbc wameshindwa ku-edit ili itoke habari nzuri ujue mambo yakpo taiti kwa watu wa magamba.
Mi nakwambia watavua hadi ngozi safari hii.
 
Sawa kabisa mkuu.Kinachohitajika ni upinzani wa aina zote dhidi ya ccm. Na hapo kazi yetu cdm inakuwa rahisi sana hasa kuelekea 2015.

Tusijidanganye! Bila katiba mpya,bila tume huru ya uchagazi,bila mshikamano wa upinzani,bila active civil movements,bila mahakama huru kuchukua dola will for ever remain a dream to be pursued but never attained na huo ndio ukweli.
 
Nnafurahi sasa hivi baadhi ya wananchi wameanza kuwa na uelewa juu ya chama cha mafisadi(wahujumu uchumi/wezi)Mungu ibariki Tanzania,wabariki na watu wake,pia kibariki Chama cha Chadema
 
Nnafurahi sasa hivi baadhi ya wananchi wameanza kuwa na uelewa juu ya chama cha mafisadi(wahujumu uchumi/wezi)Mungu ibariki Tanzania,wabariki na watu wake,pia kibariki Chama cha Chadema

Uko sahihi mkuu. Hata hivyo haya yanayotokea sasa ni ishara tosha kuwa watu wamechoshwa na utawala wa ki-imla.
Kulikuwa na dhana kuwa ni rahisi kuwadanganya watu wa vijijini. Nadhani sasa ni dhahiri shahiri kuwa zama hizo sasa zinakaribia kuzikwa.
Na tayari harakati zimeshaanza na wananchi wenyewe.
 
CCM maji ya shingo kila mtu analilia nafsi yake.
Chadema zidisheni mashambulizi pande zote! Aibu iwe kwa wote wanamagamba si Mkama peke yake
 
Back
Top Bottom