THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Hatimaye ile nguvu ambayo umma wa waTanzania umekuwa ukiitegemea pale watawala wanapofanya ndivyo sivyo imekufa rasmi baada ya BAVICHA kubariki hilo litokee.
Falsafa ya nguvu ya umma/people's power ya CHADEMA kwa muda mrefu imetumika kuongoza harakati ambazo matokeo yake hayapaswi kupuuzwa hata kidogo.
Kwa bahati mbaya kiongozi mpya wa CHADEMA ndugu Lowassa amesema hataki kuona falsafa hiyo pendwa ikiendelea kufanya kazi.
Akitoa muelekeo huo mpya wa chama Lowassa alisema;
"Uanaharakati ni nini, ni ile unagombea jambo, unafanya maandamano, unasukuma hiki, unasukuma hiki, unaregista hiki, kupiga mistari kwenye ukuta, unaweka matangazo, na nini, halafu mnazuia serikali isifanye kazi yake, maandamano kila siku, huo ndiyo uanaharakati".
Baada ya kuuelezea uanaharakati alisema CHADEMA haitaendelea kufanya hayo tena.
Baada ya tamko la Lowassa mwenyekiti wa CHADEMA mh.Mbowe aliibuka na kuwakataza BAVICHA wasiende Dodoma kufanya harakati waliyokusudia.
Leo BAVICHA wamesema rasmi wametii kauli ya Mbowe japo hawakubaliani nayo na kudai ni itifaki imewalazimisha kukubali.Kitendo hiki kinatosha kusema ile falsafa ya PIPOZ POWER kwaheri.