Nguvu ya msamaha katika mahusiano/mapenzi

Nguvu ya msamaha katika mahusiano/mapenzi

everlenk

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
11,628
Reaction score
15,032
Habari za mchana wana MMU,natumai wote ni wazima kwa kudra za mwenyezi Mungu na wale ambao si wazima Mungu awaponye.

Moja kwa moja kwenye mada husika,ni story imemtokea rafiki yangu nimeona si mbaya tukajifunza kitu wote,rafiki yangu huyu alipokuwa mtoto kama miaka 10 alibakwa na baba yake mzazi,hii ni kitu ilimuumiza sana na kumuathiri mno kisaikolojia,alimchukia sana baba yake maisha yote,ni jambo lililokuja kufahamika kifamilia hivyo kikao kiliketi na baba alipewa adhabu kulingana na mila zao,na aliomba msamaha sana kwa bintiye lakini binti alikataa katakata,na alikuwa amedhamiria haswaa toka moyoni mwake ni lazima amuue baba yake yeye mwenyewe,baada ya majaribio kadhaa kushindwa ya uuaji binti aliamua kuondoka kwao na kwenda kuishi na baba yake mkubwa.

Binti alifanikiwa kupata elimu nzuri mpaka Masters,alipokuja uraiani alitafuta Kazi sana bila mafanikio yoyote kwa miaka 4,ilipofika mwaka jana alijaribu biashara lakini ilikuwa shida sana mtaji unakata,mara anaibiwa,mara manispaa wamefanya yao yaani ni tabu tupu,niliendelea kumtia moyo kwamba asikate tamaa aendelee kuapply pia biashara huku tukimwomba Mungu.

Siku moja alinijia akiwa analia sana baada ya duka alilolifungua kupata moto,aliniambia sasa amechoka na haoni tena faida ya kuishi,alilia mno mpka nami nililia sana,katikati ya kilio changu nikajikuta natulia sauti inaniambia moyoni mwangu neno 'Msamaha 'ikawa inarudia tu mpka nijajikuta nimeongea kwa sauti kubwa,best yangu akastuka,nikamwambia unabidi umsamehe baba yako,tena niliongea kwa ukali sikujua hata ukali umetoka wapi,best yangu naye akawa mkali kwelikweli na kilio juu kwamba kamwe hawezi,yupo tayari hata kuingia motoni kwa jambo hilo,lakini nikaendelea kumsisitiza ni vizuri atengeneze na baba yake,nilijikuta nimekuwa mwinjilisti ghafla na kumpa maneno yote juu ya msamaha,hakukubali kirahisi ila aliondoka akaniambia tutaonana kesho,kesho yake kuja akaniambia ameamua kumsamehe baba yake huku akilia sana,nikamwambia ni vyema twende hadi kwa baba yake akatangaze msamaha huko.

Basi hiyo ilikuwa ni mwaka huu mwezi wa kwanza tukaenda hadi kwao tukamkuta baba yake ni mgonjwa sana ila alivyomuona tu mwanae aliinuka kitandani akafurahi sana akaomba mwanae ampe mkono,mwanae akaanza kulia akamwambia 'baba nimekusamehe' kwa yote uliyonitenda nami naomba 'unisamehe kwa yote niliyokutenda' wote wakaingia katika kilio kikubwa wakakumbatiana wakalia sana.

Baada ya siku 5 tulirudi Dar,wiki iliyofuata alianza kupata simu za kuitwa kwenye interview,aliitwa sehemu 7 tofauti mpka akawa anachanganyikiwa, kote alienda kufanya interview na kote alipita ila sehemu hiyo moja ikawa ndo bora zaidi maana aliingia kama mkurugenzi na mshahara mnono sana,nyumba kapewa na gari ya kutembelea.

Baada ya muda mfupi historia yake ikabadilika, akaamua kuifufua biashara yake akamwachia mdogo wake biashara imekubali si mchezo,kila baada ya wiki lazima aingize mali mpya toka kiwandani.

Miezi uliopita katoka kumaliza kujenga ghorofa yake,kaingiza fuso mbili kwaajili ya mizigo yake na kafungua duka lingine. Hapohapo kapata promo kazini anatakiwa aende Marekani baada ya kampuni kumkubali utendaji wake wa Kazi ndani ya hiyo miezi 6,aliweza kuzuia uwizi wa 500m. Yaani mpka sasa ni mtu mwingine haswaa si yule tena aliyekuwa na maisha mabaya. Kila siku mambo yake yanamnyookea mpaka tunashangaa wote hizi baraka zilivyozidi hadi yeye haamini mambo yalivyobadilika,amekuwa mtu wa furaha sana,hata maisha yake ya kimahusiano yamebadilika maana yalikuwa majanga kila siku,alikuwa hakai na mwanaume miezi 6, mwezi wa 12 Mungu akipenda atakuwa akifunga ndoa.(yuko 35)

Wenzangu wana MMU tujifunze kusamehe haijalishi tumeumizwa kiasi gani,kuna baraka kubwa katika kusamehe,wakati mwingine tunaingia katika matatizo makubwa kwasababu hatujawasamehe wengine, tujifunze kutokaa na kinyongo,jua lisizame bado tuna hasira mioyoni mwetu,ipo nguvu katika kusamehe,tuwe watu wa kuachia,tuache kulipiza visasi kisasi si juu yako bali cha Mungu.

Karibuni wote kwa mawazo zaidi na muwe na weekend njema.
 
Ok thanx ubarikiwe, embu ngoja nicheck check ni nani alinikosea na nina kinyongo nae nikatangaze msamaha chaaaapu ili hizi baraka ziendelee kunimiminikia.
 
Yeye asiyesamehe ni sawa na mtu ambae anakataa kubeba ubao, ambao akifika mtoni anaambiwa bila ubao uliouacha hutaweza kuvuka. Hivyo anapaswa kuurudia ili avuke.
Hakika everlenk Tunahitaji kumuomba Mungu atupe nguvu ya kusamehe, si rahisi, tunahitaji uwezo wake.
^^
 
Last edited by a moderator:
Hapa somo kubwa ni msamaha mengine yote ni matokeo tu.

Umenikumbusha pia habari za maandiko juu ya mwana mpotevu alipoamua kurudu nyumbani na kuomba msamaha kwa baba yake, baada ya kusota kwa maisha ya mateso na kula mabaki huku nyumbani kwao watumishi wa baba yake wakila vizuri na kusaza.
 
Honestly mimi masomo ya msamaha na yooote yahusuyo kuwapenda adui nayaaogopa coz nahisi hapo ndipo jehanam yangu ilipo so so currently nimekua sipendi hata kuyasikia. Kuna watu sidhani ka nitakuja kuwasamehe hivyo kuwachukulia kama ilivyokuwa awali......SIWAPENDI MAISHA!!!
 
Yeye asiyesamehe ni sawa na mtu ambae anakataa kubeba ubao, ambao akifika mtoni anaambiwa bila ubao uliouacha hutaweza kuvuka. Hivyo anapaswa kuurudia ili avuke.
Hakika everlenk Tunahitaji kumuomba Mungu atupe nguvu ya kusamehe, si rahisi, tunahitaji uwezo wake.
^^
Ni kweli Himidini umenena vyema peke yetu hatuwezi ila kwa msaada wa Mungu yote yawezekana.
 
Last edited by a moderator:
embu naoomba namba zake basi nmkope hata mil 5, mana miradi yote hyo na kila k2 anacho....
msamaha ni jambo zuri sana kwenye maisha, usijaribu kulipiza ubaya kwa ubaya, fanya yaliyomema ili uweze barikikiwa

Hahahahaha!!!! I wish ningekupatia...... kweli kabisa lipa wema kwa ubaya.
 
Alikuwa kitaani ghafla anapata ukurugenzi!!

Hata mm nimeduwaa kidogo hapa mkuu coz logically it doesn't make sense at all, mtu kamaliza chuo miaka 4 iliyopita, she's got no experience at all except for the series of bad experiences she's had in the past then gafla bin vuu kapata ajira tena managerial position,duh! Ila ya Mungu mengi, greatest lesson from this whole story is FORGIVENESS, hiyo siwezi pingana nayo.
 
Honestly mimi masomo ya msamaha na yooote yahusuyo kuwapenda adui nayaaogopa coz nahisi hapo ndipo jehanam yangu ilipo so so currently nimekua sipendi hata kuyasikia. Kuna watu sidhani ka nitakuja kuwasamehe hivyo kuwachukulia kama ilivyokuwa awali......SIWAPENDI MAISHA!!!

Pole sana Avemaria kwa ulivyoumizwa lakini pamoja na yote inabidi utangaze msamaha,kusamehe si rahisi ila inawezekana,fikiria huyu rafiki yetu alibakwa na baba yake mzazi aisee ni jambo linaloumiza sana....samehe hata Baba wa mbinguni atakusamehe wewe makosa yako....
 
Last edited by a moderator:
jamani sijui kama nitaweza kuja kumsamehe my X kwa moyo mmoja kabisa???? cjui aisee najitahidi sana bt najikuta nafikilia aliyonitendea najikuta hasira inaongezeka x100 mungu anisaidie kwa hili.
 
Back
Top Bottom