The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,780
- 8,155
KUSAMEHE NA KUTOLIPA KISASI NI KWA AJILI YA FAIDA YAKO BINAFSI ❤️🌹🍎
Kusamehewa walio tukosea ni jambo gumu sana, ila ni la muhimu sana pia. Ktk hii dunia lazima utakutana na watu wabaya ktk maisha yako.Unaweza kuwatendea mema sana wanadamu,lakini wao watakufanyia mabaya au ubaya kama malipo yako.
Watakufanyia mambo ya kinyama ya kuumiza moyo wako. Na utatamani uwalipize kisasi. Lakini Yesu Kristo anajua hayo yote na alituagiza tuwasamehe hao watu.Haijalishi kiwango cha ubaya uliotendewa, ila agizo la Yesu Kristo ni kuwa unatakiwa kusamehe tu.
Kwa sababu kisasi hapa duniani ni mali ya Mungu na yeye ni fundi wa kuwalipa maadui zetu kisasi kuliko sisi.Hivyo kuwa upande wa Mungu kwa kutolipa kisasi kamwe ktk maisha yako.
Fanya uamuzi thabiti wa kutomlipa mtu yeyote kisasi hata kama anastahili kulipwa mabaya yake.
Mtu anayemjua Mungu anaweza kudai haki zake mahakamani;lakini kamwe halipi kisasi kwa wabaya wake.Kudai haki siyo lazima kuambatane na kulipa kisasi.Soma{ mithali 19:11 Busara ya mtu huihairisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa}.
Chagua fungu hili jema la kusamehe na kuachilia kabisa kutoka kwenye moyo wako kisasi maana wewe ni mwana wa Mungu.
Kutokulipa kisasi hukufanya kujiepusha na mabaya mengi.Soma{ mithali 17:13 yeye arudishaye mabaya badala ya mema, Mabaya hayataondoka nyumbani kwake }.
Hivyo chagua fungu moja jema la kutokulipa kisasi kwa watu au mtu yeyote. Ishi kwa furaha na amani kwa kutoishi na kinyongo au uchungu.
Thamani yako ni kubwa sana duniani hivyo mwachie Mungu tu na usilipe kisasi wala kuwaombea maadui zako mambo mabaya.
Jiunge na group la Nuru ya Injili International WhatsApp, ili ujifunze Neno la Mungu kila siku kwa njia ya sauti. Bonyeza link 👇👇 hapo juu ya picha ujiunge wewe mwenyewe. By pastor Mfinanga.+255762048897