Nguvu ya mila

Satuuuu

JF-Expert Member
Dec 3, 2015
1,849
1,993
Yapo makabila yenye kuamini sana katika mila na inasemekana mtu asipofanya au kufanyiwa mila mambo yake yaweza enda kombo. Yapo makabila mtoto akizaliwa kama ni mjini lazima atapelekwa kwa mababu lasivyo ataumwa..... Je ni nini hasa kinachosumbua kuna ukweli au ni imani tu ?
 
Mila ni social assumptions tu, mababu waliweka ili kuongoza/kufafanua jambo fulani, au namna fulani watu wapaswa waishi katika jamii yao. Jambo lingine kuhusu mila/desturi ni kuwa watu wanao waza freely bila kujali jamii inasema nini huwa hawaamini mambo haya kwasababu hayana mashiko kwa undani wake. Pia inaonyesha ukipata elimu na ikakukomboa hasa, hutoamini hizo mila/desturi ulizojaribu kuelezea.
 
Mila ni imani na imani yoyote duniani ukiiamini inakuponya.
Kumbuka babu wa babu zetu waliomba kwenye miti mvua na ikanyesha kwa sababu waliamini.
Sasa na wewe ukiamini itakuwa na usipoamini haitakuwa...kazi kwako
 
Haya mambo ya mila nimeshayasikia sana, wengine wanapokiuka mila zao inafikia kupukutika, yaani vile vifo/misiba mfululizo, mpaka waende kwenye mizimu yao wakiomba msamaha ndio mambo yanatulia.

NB: Ni mambo ambayo nimeyasikia, nimehadithiwa, sikuwahi kuyashuhudia kwa macho yangu
 
Umenikumbusha,nilisafiri na rafiki yangu tukaenda kwao vijijini kufika,wakachukua sijui unga wakawa wana umwaga kiduchu duchu huku wanasema maneno hata nilikua siyafahamu mwisho yule mama akatia maji mdomoni akawatemea mie nikasema
hili sasa balaa,ukizingatia yule bibi ndio katoka kuamka.........
 
Kufuata Mila kuna faida sana kwa wale waaminio kwani pale ni unajiconnect na mizimu ya kwenu kwa imani ya kuwa ni mababu wa mababu wako ambalo kupitia hiyo utalindwa, utafanikiwa na utapata mambo mengi kwa kadiri ya mahitaji yako ili mradi tu utii masharti upewao na sharti kubwa sana huwa ni kutoa sadaka...
 
Kufuata Mila kuna faida sana kwa wale waaminio kwani pale ni unajiconnect na mizimu ya kwenu kwa imani ya kuwa ni mababu wa mababu wako ambalo kupitia hiyo utalindwa, utafanikiwa na utapata mambo mengi kwa kadiri ya mahitaji yako ili mradi tu utii masharti upewao na sharti kubwa sana huwa ni kutoa sadaka...
Wewe unafata mila?
 
Back
Top Bottom