Nguvu ya Media: Aliyepaswa kuwa maarufu ni OYADEPO sio TB Joshua

Jehovah na mwanae Yesu wako mdomo wazi! Hii ndio Injili siku hizi, nani ana pesa?!
Hii injili ni ya zamani tangu edeni mkuu.
Umesahau Jehovah aliwawekea hadi dhahabu bustanini. Yawezekana hawa wakuu wao waliamua kuanza kula maisha bora kabla ya Yale yaliyohaidiwa
 
Jehovah na mwanae Yesu wako mdomo wazi! Hii ndio Injili siku hizi, nani ana pesa?!
Injili ni uweza.
Hata kumiliki mapesa unahitaji uweza.
Wanaonyesha mfano mzuri, kuwa fedha ni za Mungu mwenye uweza na wao watoto wake wanamiliki kwa uweza huohuo wakosahihi mkuu.

Tuwajadili tu.
Ukristo sio umasikini na kuishiwa.
 
Ukiteka vyombo vya habari umeteka dunia.

TB Joshua (hayati) alikuwa amkaribii kwa chochote Mzee Oyadepo.
Oyadepo ndio mchungaji Tajiri kuliko wote ulimwengini.

Amehamasisha watu wengi kuwa matajiri duniani. Ukisoma kitabu cha Oyadepo ukaja ukisoma cha TB ni sawa na kula Mua na kisha ukaletewa menyu ya miwa iliyotafunwa na kutolewa utamu.

Ndio Muafrika wa kwanza kuwa na makanisa hadi ulaya. Ukraine alikuwa na kanisa kubwa lenye waumini wazungu kibao wakati TB anaarika wazungu SCOAN na kuwapa coverage kubwa.


TB alikuwa bingwa wa kuaminisha kwa kutumia media. Hata alipofungiwa na serikali akafanya mchongo wa kuhamia kwenye Satellite broadcast hapo ndipo alipoteka soko kote duniani hasa Africa huku wanigeria wenzake wakibaki local.

Somo : Kuna nguvu katika Media, Ukiwa na kitu chako lakini hujitangazi utabaki kuonekana duni licha ya kuwa na uwezo mkubwa.

SOMO: Oyadepo na yeye anafundisha watu tufocus katika matokeo sio maneno. Oyadepo anamengi ya kufundisha kuliko.

Note: Oyadepo ndio mmiliki wa makanisa ya Winners.

Mnaomfahamu zaidi mtujuze na mambo ya kujifunza kutoka kwao ukiacha figisu zao visonzoni mwa sadaka.
Umaarufu wa watumishi wa Mungu huwa hautegemei utajiri ulioko kwenye mifuko yao, bali karama ya kiroho waliyokirimiwa na Bwana katika kuifanya kazi yake.

Mfano mzuri hapa kwetu nchini Tanzania, Mwalimu Mwakasege ndiyo mtumishi wa Mungu maarufu karibia kuzidi watumishi wote Afrika Mashariki, lakini sina uhakika kama ndiye mtumishi wa Mungu anayeongoza kwa utajiri kwa watumishi wote wa Mungu walioko Afrika Mashariki
 
Back
Top Bottom