Nguvu ya Maandamano: Baraza la Mawaziri nchini Mali lajiuzulu

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali amekubali ombi la kujiuzulu kwa waziri mkuu na baraza lake zima la mawaziri. Soumeylou Boubeye Maiga alichukuwa hatua hiyo hapo jana, kufuatia wiki mbili za maandamano ya umma dhidi ya mauaji ya kiholela katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

Maandamano hayo yalichochewa na mauaji ya wachungaji 160 wa jamii ya Fulani, ambayo yanashukiwa kufanywa na watu wa jamii ya Dogon, wanaoishi kwa kilimo na uwindaji.

Mauaji hayo yaliitikisa Mali, ambayo katika miezi ya karibuni imeshuhudia mauaji mengine kadhaa, yakiwemo yale ya wanajeshi 23 walioshambuliwa kwenye kituo chao.

Juzi Jumatano, bunge lilijadili uwezakano wa kura ya kutokuwa na imani na serikali kutokana na mauaji hayo na pia kushindwa kuwanyang'anya silaha na kuwazuwia wanamgambo wa itikadi kali.

Umoja wa Mataifa una zaidi ya wanajeshi 16,000 nchini Mali, vikiwemo vikosi kutoka Ufaransa na Ujerumani.
 
Waziri mkuu wa Mali amejiuzulu yeye na serikali yake yote.
Soumeylou Boubeye Maiga, alijuzulu kufuatia shinikizo kutoka kwa wabunge aondoke madarakani kwa kushindwa kuzuia mauaji ya zaidi ya watu 160 wa jamii ya Fulani waliouawa na watu wanaodhaniwa kutoka kwa jamii hasimu ya Dogon.
Rais Ibrahim Boubacar Keita ameidhinisha kuvunjika kwa utawala wa Maiga.
Je viongozi wa ukanda huu wa Afrika Mashariki wanapaswa kujifunza kuwajibikia wananchi ?

Chanzo ni BBC SWAHILI
 
Africa, serikali nyingi zitakuwa hatarini kuondolewa madarakani sbb ya ugumu wa maisha.
 
Waziri mkuu wa Mali amejiuzulu yeye na serikali yake yote.
Soumeylou Boubeye Maiga, alijuzulu kufuatia shinikizo kutoka kwa wabunge aondoke madarakani kwa kushindwa kuzuia mauaji ya zaidi ya watu 160 wa jamii ya Fulani waliouawa na watu wanaodhaniwa kutoka kwa jamii hasimu ya Dogon.
Rais Ibrahim Boubacar Keita ameidhinisha kuvunjika kwa utawala wa Maiga.
Je viongozi wa ukanda huu wa Afrika Mashariki wanapaswa kujifunza kuwajibikia wananchi ?

Chanzo ni BBC SWAHILI
Huku kwetu ukileta vyoko mashangazi watapigwa sana… na hivi akidi inatosha ndo balaa
 
Huku hata mfe elfu tatu hamna anayejali kile kivuko cha Ukerewe kiliondoka na wangapi ?

Ni kina nani waliowajibishwa ?
 
Kama waziri wa usafiri wakati wa MV Bukoba na Ukerewe hawakujiuzulu hata wakati wa train ya Dodoma, iwe lolote, Waziri mkuu aliyejiuzuru ni mmoja tu ambaye ni Lowasa basi. Waziri mwingine alikuwa mzee Mwinyi akiwa waziri wa mambo ya ndani. Wengine ni wachumia tumbo.
 
Moto wa msituni polepole huteketeza msitu mzma na kila kitu isipokua tu mawe. Maandamano Africa yalioanzia Uarabuni na kushuka hadi Zimbabwe yamewatoa wababe madarakani. Lakn nayaona mawe ambayo hayatateketezwa na moto huu wa msituni (Africa)
Sababu kuu ni Unafiki na uoga wa watu wale licha kua ni watumwa wa yale mawe yasiokua na uhai ndani yake.
 
Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali amekubali ombi la kujiuzulu kwa waziri mkuu na baraza lake zima la mawaziri. Soumeylou Boubeye Maiga alichukuwa hatua hiyo hapo jana, kufuatia wiki mbili za maandamano ya umma dhidi ya mauaji ya kiholela katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

Maandamano hayo yalichochewa na mauaji ya wachungaji 160 wa jamii ya Fulani, ambayo yanashukiwa kufanywa na watu wa jamii ya Dogon, wanaoishi kwa kilimo na uwindaji.

Mauaji hayo yaliitikisa Mali, ambayo katika miezi ya karibuni imeshuhudia mauaji mengine kadhaa, yakiwemo yale ya wanajeshi 23 walioshambuliwa kwenye kituo chao.

Juzi Jumatano, bunge lilijadili uwezakano wa kura ya kutokuwa na imani na serikali kutokana na mauaji hayo na pia kushindwa kuwanyang'anya silaha na kuwazuwia wanamgambo wa itikadi kali.

Umoja wa Mataifa una zaidi ya wanajeshi 16,000 nchini Mali, vikiwemo vikosi kutoka Ufaransa na Ujerumani.
Hope and Pray itokee Tz
Wananchi wanaumia sana mioyoni
Viongozi wa Africa kama jehanamu kweli ipo na wote wakaangamie huko.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bunge letu limejaa wahuni, wezi na mafisadi toka ccm limepoteza umuhimu wa kuendelea kuwepo zaidi ya kulipwa mabilioni kila mwaka huku kukiwa hakuna chochote cha maana wanachokifanya zaidi ya kuunga mkono maovu mbali mbali yanayofanywa na dikteta wa Ikulu ikiwemo wizi na ubadhirifu wa kutisha wa pesa za walipa kodi.

Nataman bunge livunjwe tu sijaona faida yao kama kila kitu kinafanywa kutokea juu
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽

Back
Top Bottom