Nguvu ya kucha na nywele katika ulimwengu wa kichawi

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
📣📣📣📣📣📣📣📣
Nguvu ya kucha na nywele katika ulimwengu wa kichawi

🗣️Leo nimeona ni vyema niwaletee makala hii fupi kuhusiana na kucha na nywele zinavyo husika katika ulimwengu wa kichawi ulimwengu huu ni mpana sana, basi bila kupoteza wakati twende sawa.

👉Nywele na kucha zinaaminika kuwa na nguvu sana katika ulimwengu wa kichawi hivyo vimekuwa viungo muhimu katika kutengeneza uchawi (magic spells).

🙅🏿‍♀️Pia Nywele zinahusishwa kubeba nguvu ya mchawi mhusika na pia ni kama kinga, katika historia za miaka ya nyuma, kuwa na nywele nyingi iliaminika kuwa ni moja wapo ya alama ya utajiri na nguvu kwa wafalme wengi, pia Wamisri wa zamani waliamini kuwa dawa iliyotengenezwa kwa nywele, vipande vya kucha na damu ya mwanadamu inampa mtu nguvu nyingi zaidi kuliko wengine.🤔

🧜‍♂️Kama nilivyoeleza awali, nguvu za kichawi za mchawi zimefungwa kwenye nywele zake hivyo katika kutengeneza uchawi mchawi akitikisa nywele zake nguvu ya huo uchawi inaongezeka mara mbili.🤔

👉Katika ulimwengu wa nguvu za kichawi kukata nywele kunachukuliwa kama kitendo cha kumdhoofisha mchawi na kupoteza nguvu zake pia ni udhalilishaji au adhabu.🔥

🔰Samsoni japo hakuwa mchawi alipoteza nguvu wakati Delila alikata nywele zake hii inaonesha ni kwa jinsi gani nywele zinaweza kubeba nguvu za mtu husika katika ulimwengu wa kiimani pia Wabils wa India ya Kati walitesa wachawi wanaoshukiwa, kisha wakakata nywele zao na kuzika ili kukata uhusiano kati ya wachawi na nguvu zao za kichawi hii hata Tanzania huwa inatokea sana pale wachawi wanapokamatwa, wachawi walinyolewa kwa imani kwamba iliwafanya wasiwe na nguvu na uwezekano mkubwa wa kukiri; pia, walinyolewa kutafutwa alama katika miili yao ambazo zinaweza kutambuliwa kama alama za kichawi.🎇

💅Kucha ndefu huwa zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na mashetani au majini ndio maana katika utamaduni wa Wayahudi na jamii zinginezo ni marufiku mtu kufuga kucha ndefu hivyo huhakikisha kucha zao ni fupi muda wote pia makabila ya huko Madagaska wanaamini kuwa Ibilisi au majini huishi chini ya kucha zisizo katwa yaani kucha ndefu.🤔

🗣️Habari hizi za nywele na kucha ndefu katika ulimwengu wa kichawi zinatupeleka nyuma hadi katika Vendidad kitabu cha Zoroastrian kilichoandikwa katikati ya karne ya 5, Kulingana na yaliyoandikwa katika Vendidad, nywele na kucha ni vyombo/viungo muhimu katika ulimwengu wa uovu kwa sababu nywele na kucha hukua katika maisha yote ya mwanadamu hivyo vinaweza kutenganishwa na mwili ili kutumiwa na wachawi kuita mizimu na majini, kuroga na kutengeneza uchawi (spells) katika kipindi hiko mtu ajulikanaye kama Ahura Mazda alitoa mila maalumu iitwajo Zarathustra kwa utupaji salama wa vipande vya nywele na vifurushi vya kucha ambayo ina husisha kuzizika/kuzifukia ili zisiweze kutumika katika shughuli za kichawi.

👉Mila ya kuzika/kufukia nywele zilizokatwa na kucha iliendelea katika jamii nyingi watu walikuwa wanatupa nywele zao na kucha kwa siri sana kwa maisha yao yote mila hii ilikuwa ikitumiwa katika jamii nyingi sana hasa ndani ya bara la ulaya katika kipindi hiko.

♦️Pia waganga wa jadi katika jamii hizo walikuwa wanatumia nywele za mtu aliyerogwa na wachawi kutengeneza dawa kuponya mtu aliye athiriwa na nguvu za kichawi, nywele za mwathiriwa aliyerogwa zilitupwa ndani ya moto iliaminiwa kuwa kadri zile nywele zinavyo ungua maumivu ya moto hurudi kwa mchawi aliyemroga mtu huyo.🤔

👉Wakati huo watu walitumia nywele za mtu aliyekufa kama njia ya kuwadhoofisha maadui zao kwa kuchukua nywele za maiti na kuzifukia chini ya kizingiti cha mlango wa adui inasemekana ilisababisha adui kupata ugonjwa wa homa kali na kutetemeka endapo atazivuka zile nywele pia Katika sehemu za Ujerumani, walikuwa wanatumia begi dogo la nywele laini za binadamu kufunga juu ya tumbo la mtu ili kujua mtu huyo amerogwa au laah kama mtu huyo amerogwa basi zile nywele ni lazma zijinyonge nyonge baada ya siku tatu kama nywele hizo zikitoka zimenyooka ilimaanisha mtu huyo hajarogwa.🔥

👉Nywele, haswa zile za sehemu za siri (mavuzi) inachukuliwa kama kiungo chenye nguvu katika kutengeneza hirizi au dawa za mapenzi, Kulingana na vitabu mbalimbali, John Fian, mchawi wa Scotland wa karne ya 16, alijaribu kumfanya msichana mdogo ampende kwa kutengeneza dawa kwa kutumia nywele tatu za sehemu za siri kutoka kwa msichana huyo kwa bahati mbaya akatokea mtu akazibadilisha zile nywele za yule msichana na kuweka nywele kutoka kwa kiwele cha ng'ombe John Fian yeye bila kujua akatengeneza dawa kwa kutumia zile nywele hatimae ng'ombe alimpenda Fian na kuanza kumfata mji kote hata hivyo bado ni kawaida kwa wapenzi kubeba vifuniko vya nywele za kichwa, na katika karne zilizopita, wasichana wadogo mara nyingi walitengeneza bangili za nywele kuwapa wapenzi wao ili waendelee kuwa waaminifu.🧚🏽‍♀️

👩‍🦰Katika jamii za ulaya watu waliamini kuwa watu wenye nywele nyekundu ni wachawi, kulingana na imani moja ya zamani ushahidi upo kuonyesha kwamba kuna wachawi wa kipagani walipaka nywele zao rangi nyekundu kama mila katika ulimwengu wa kichawi, pia nywele nyekundu zilikuwa ni kawaida kwa Weltel ambao mila zao zilikuwa zimejaa uchawi pia wakati wa uwindaji wa wachawi watu wenye nywele nyekundu mara nyingi walishukiwa na kukamatwa na uchawi.

👉Kulingana na ushirikina, kukata nywele ni lazima kuendane na wakati kulingana na majira ya mwezi kulingana na jinsi mchawi anavyotaka nywele zikuwe na nguvu ipi kwa haraka.

By
Mchawi wa wachawi

✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️
 
IMG-20250320-WA0348.jpg
 
Kiroho nywele humfanya mtu ajiamini na awe na nguvu kiroho, kiakili na kimtazamo.
Watu wanaonyoa / nyolewa nywele zao kuna vitu fulani vya kiroho hupungua kwa namna moja ama nyingine, ila hawaishiwi kabisa.
Kati ya adhabu kubwa alizopewa mtu mkorofi zamani kabla dini hazijachukua nafasi ya mambo ya rohoni, ilikuwa ni kumnyoa nywele zake (kunyolewa nywele na ndevu)

Wanafunzi wakorofi mashuleni walipoanza kunyolewa nywele ukorofi wao ulipungua kwa asilimia kubwa.
Mfungwa asipinyolewa kichwa chake atasumbua sana akiwa gerezani.
Ndio maana jeshini huwezi kwenda na minywele, wanakunyoa ili uwe chini ya amri ya jeshi!
Hebu kumbuka kipindi ulipokuwa hujaanza kunyoa na sasa ambapo nywele zako hazikai kichwani kwako unaziachaga saluni, ni lini ulikuwa na uwezo mkubwa wa ku- reason, ku- argue, kujisimamia nk?
Kama hujanielewa jaribu kufanya research mwenyewe ukiwa na nywele kichwani na ukiwa huna nywele, utajionea utofauti!

Unataka niendelee?
Wafia dini mnisamehe kwa leo, mimi naongea lugha msiyoweza kuielewa😎
 
📣📣📣📣📣📣📣📣
Nguvu ya kucha na nywele katika ulimwengu wa kichawi

🗣️Leo nimeona ni vyema niwaletee makala hii fupi kuhusiana na kucha na nywele zinavyo husika katika ulimwengu wa kichawi ulimwengu huu ni mpana sana, basi bila kupoteza wakati twende sawa.

👉Nywele na kucha zinaaminika kuwa na nguvu sana katika ulimwengu wa kichawi hivyo vimekuwa viungo muhimu katika kutengeneza uchawi (magic spells).

🙅🏿‍♀️Pia Nywele zinahusishwa kubeba nguvu ya mchawi mhusika na pia ni kama kinga, katika historia za miaka ya nyuma, kuwa na nywele nyingi iliaminika kuwa ni moja wapo ya alama ya utajiri na nguvu kwa wafalme wengi, pia Wamisri wa zamani waliamini kuwa dawa iliyotengenezwa kwa nywele, vipande vya kucha na damu ya mwanadamu inampa mtu nguvu nyingi zaidi kuliko wengine.🤔

🧜‍♂️Kama nilivyoeleza awali, nguvu za kichawi za mchawi zimefungwa kwenye nywele zake hivyo katika kutengeneza uchawi mchawi akitikisa nywele zake nguvu ya huo uchawi inaongezeka mara mbili.🤔

👉Katika ulimwengu wa nguvu za kichawi kukata nywele kunachukuliwa kama kitendo cha kumdhoofisha mchawi na kupoteza nguvu zake pia ni udhalilishaji au adhabu.🔥

🔰Samsoni japo hakuwa mchawi alipoteza nguvu wakati Delila alikata nywele zake hii inaonesha ni kwa jinsi gani nywele zinaweza kubeba nguvu za mtu husika katika ulimwengu wa kiimani pia Wabils wa India ya Kati walitesa wachawi wanaoshukiwa, kisha wakakata nywele zao na kuzika ili kukata uhusiano kati ya wachawi na nguvu zao za kichawi hii hata Tanzania huwa inatokea sana pale wachawi wanapokamatwa, wachawi walinyolewa kwa imani kwamba iliwafanya wasiwe na nguvu na uwezekano mkubwa wa kukiri; pia, walinyolewa kutafutwa alama katika miili yao ambazo zinaweza kutambuliwa kama alama za kichawi.🎇

💅Kucha ndefu huwa zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na mashetani au majini ndio maana katika utamaduni wa Wayahudi na jamii zinginezo ni marufiku mtu kufuga kucha ndefu hivyo huhakikisha kucha zao ni fupi muda wote pia makabila ya huko Madagaska wanaamini kuwa Ibilisi au majini huishi chini ya kucha zisizo katwa yaani kucha ndefu.🤔

🗣️Habari hizi za nywele na kucha ndefu katika ulimwengu wa kichawi zinatupeleka nyuma hadi katika Vendidad kitabu cha Zoroastrian kilichoandikwa katikati ya karne ya 5, Kulingana na yaliyoandikwa katika Vendidad, nywele na kucha ni vyombo/viungo muhimu katika ulimwengu wa uovu kwa sababu nywele na kucha hukua katika maisha yote ya mwanadamu hivyo vinaweza kutenganishwa na mwili ili kutumiwa na wachawi kuita mizimu na majini, kuroga na kutengeneza uchawi (spells) katika kipindi hiko mtu ajulikanaye kama Ahura Mazda alitoa mila maalumu iitwajo Zarathustra kwa utupaji salama wa vipande vya nywele na vifurushi vya kucha ambayo ina husisha kuzizika/kuzifukia ili zisiweze kutumika katika shughuli za kichawi.

👉Mila ya kuzika/kufukia nywele zilizokatwa na kucha iliendelea katika jamii nyingi watu walikuwa wanatupa nywele zao na kucha kwa siri sana kwa maisha yao yote mila hii ilikuwa ikitumiwa katika jamii nyingi sana hasa ndani ya bara la ulaya katika kipindi hiko.

♦️Pia waganga wa jadi katika jamii hizo walikuwa wanatumia nywele za mtu aliyerogwa na wachawi kutengeneza dawa kuponya mtu aliye athiriwa na nguvu za kichawi, nywele za mwathiriwa aliyerogwa zilitupwa ndani ya moto iliaminiwa kuwa kadri zile nywele zinavyo ungua maumivu ya moto hurudi kwa mchawi aliyemroga mtu huyo.🤔

👉Wakati huo watu walitumia nywele za mtu aliyekufa kama njia ya kuwadhoofisha maadui zao kwa kuchukua nywele za maiti na kuzifukia chini ya kizingiti cha mlango wa adui inasemekana ilisababisha adui kupata ugonjwa wa homa kali na kutetemeka endapo atazivuka zile nywele pia Katika sehemu za Ujerumani, walikuwa wanatumia begi dogo la nywele laini za binadamu kufunga juu ya tumbo la mtu ili kujua mtu huyo amerogwa au laah kama mtu huyo amerogwa basi zile nywele ni lazma zijinyonge nyonge baada ya siku tatu kama nywele hizo zikitoka zimenyooka ilimaanisha mtu huyo hajarogwa.🔥

👉Nywele, haswa zile za sehemu za siri (mavuzi) inachukuliwa kama kiungo chenye nguvu katika kutengeneza hirizi au dawa za mapenzi, Kulingana na vitabu mbalimbali, John Fian, mchawi wa Scotland wa karne ya 16, alijaribu kumfanya msichana mdogo ampende kwa kutengeneza dawa kwa kutumia nywele tatu za sehemu za siri kutoka kwa msichana huyo kwa bahati mbaya akatokea mtu akazibadilisha zile nywele za yule msichana na kuweka nywele kutoka kwa kiwele cha ng'ombe John Fian yeye bila kujua akatengeneza dawa kwa kutumia zile nywele hatimae ng'ombe alimpenda Fian na kuanza kumfata mji kote hata hivyo bado ni kawaida kwa wapenzi kubeba vifuniko vya nywele za kichwa, na katika karne zilizopita, wasichana wadogo mara nyingi walitengeneza bangili za nywele kuwapa wapenzi wao ili waendelee kuwa waaminifu.🧚🏽‍♀️

👩‍🦰Katika jamii za ulaya watu waliamini kuwa watu wenye nywele nyekundu ni wachawi, kulingana na imani moja ya zamani ushahidi upo kuonyesha kwamba kuna wachawi wa kipagani walipaka nywele zao rangi nyekundu kama mila katika ulimwengu wa kichawi, pia nywele nyekundu zilikuwa ni kawaida kwa Weltel ambao mila zao zilikuwa zimejaa uchawi pia wakati wa uwindaji wa wachawi watu wenye nywele nyekundu mara nyingi walishukiwa na kukamatwa na uchawi.

👉Kulingana na ushirikina, kukata nywele ni lazima kuendane na wakati kulingana na majira ya mwezi kulingana na jinsi mchawi anavyotaka nywele zikuwe na nguvu ipi kwa haraka.

By
Mchawi wa wachawi

✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️
Ingeweka fact ingekuwa vizur zaidi nakuwa supported na practical, kuliko theories au hadithi za vitabu..
 
Back
Top Bottom