Nguvu ya Binadamu katika Uharibifu

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,431
19,776
F16F14AF-5DB9-45DC-9790-61D4461BA76E.jpeg

Beirut,Lebanon

Mlipuko mkubwa umetokea, Chanzo bado kina utata(Tani 2750 za Ammonium Nitrate au Shambulio?)

MBUZI WA KAFARA:
Meli moja inayomilikiwa na Kampuni kutoka Urusi ikiwa na usajili(Bendera) ya Moldova ilifanya safari September 2013 kutoka bandari ya Batumi, Georgia ikiwa inaelekea Beira, Msumbiji

Meli hio ilikua imebeba tani 2,750 za ammonium nitrate, ambayo huwa iko kwenye mfumo wa chengachenga na hutumika kama mbolea ya mashambani, tatizo ni kwamba Ammonium Nitrate ikichanganywa na petroli huwa inatumika kwa ajili ya milipuko kwenye migodi na kwenye upasuaji wa miamba wakati wa ujenzi.

Kabla ya kufika mwisho wa safari yake Rhosus ilipata hitilafu ya kiufundi katika Bahari ya Mediterania na ikalazimika kutia nanga Beirut.
FFBB3CA4-08D4-4024-9057-11E63C51AC45.jpeg


Rhosus ilikaguliwa na maafisa wa bandari wa Beirut na ikapigwa marufuku kuendelea na safari kwasababu ya ubovu.

AB8F18B5-EB6A-4F89-9FB5-1A1360855B2A.jpeg

Ramani ikionyesha Safari ya Rhosus

Wafanyakazi wa meli hio walirudishwa makwao(Repatriation) isipokua Nahodha wa meli Boris Prokoshev(Mrusi) na wafanyakazi wengine watatu wenye uraia wa Ukraine.

Kwa mujibu wa Nahodha wa meli hiyo Mr Prokoshev tatizo la meli hio ni kwamba ilikua inavuja lakini ilikua na uwezo wa kuendelea na safari(Seaworthy) kinyume na uamuzi wa maafisa wa Bandari wa Beirut kuizuia.

Prokoshev anasema pamoja na matatizo ya kiufundi aliyopata pia alitia nanga Beirut kwa maagizo ya mmiliki wa meli kwamba kuna mizigo ya kuongeza pale(Heavy equipments)

Hata hivyo walishindwa kupakia mzigo huo na walikaa kwa muda mrefu katika bandari hiyo hadi mmiliki akashindwa kulipia gharama za bandari na serikali ya Lebanon ikaitafisha meli pamoja na mzigo wake

Ammonium Nitrate ikaenda kuwekwa kwenye ghala


Miaka Sita baadae🔥🔥🔥🔥
 
E2983014-2543-40D2-8001-F773609F6CA7.jpeg

Alama nyekundu Ghala inalosemekana lilihifadhi hizo Fertillizers, alama kijani limetokomea kabisa
D319C7E8-ACB5-4E66-BAA8-02253AD52519.jpeg

Je hii ni ajali kama ajali nyingine za kemikali hatari? Au kuna nguvu ya Binadamu katika Kufanya uharibifu?

Muda ni msemakweli, tuvute subra
D386031D-6EC0-4DF6-B525-68C26F394F24.jpeg
 
Naona tatizo ni huo utaifishaji uliofanywa. Wenye mali yao wakaamua kulipa kisasi
 
Back
Top Bottom