Nguvu kubwa kusema hakuna njaa, ila walaji wanalalama

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,314
72,740
Kuna nguvu kubwa sana inatumika kwa viongozi wa kuteuliwa kuunga mkono kauli ya mkuu kuwa hakuna njaa na vyombo vya habari kadhaa kama Star TV na Uhuru. Lakini vijijini kwenye walaji wenyewe wanapohojiwa wanakiri kuna njaa. Hata mijini njaa ipo ila watu wanasaidiwa na akiba yao ya fedha.
Tumeona na viongozi wa dini makini ambao wanapata data zao kutokea chini kabisa nao wanesema ipo shida na tuwaombee viongozi waione na kuchukua hatua.
Utetezi wa hao wanaounga mkono kuwa hakuna njaa ni eti wanasiasa na wafanyabiashara ndio wanapotosha.
Jee kutokuwepo njaa ni vyakula kujaa kwenye maghala ya serikali wakati wananchi wanalalia embe?
 
Viongozi wa DINI MAKINI??????......kumbe wapo ambao si makini????...sasa ebu tuthibitishie UMAKINI wao umeupima vipi????.......NCHI hii hakuna VIONGOZI wa DINI....bali kuna viongozi wa DINI MASLAHI....VIONGOZI WA DINI WACHUMIA TUMBO....VIONGOZI WA DINI WANASIASA......refer UCHAGUZI WA MWAKA 2015....ndio utatambua NCHI HII HAINA VIONGOZI WA DINI.......VIONGOZI WA DINI WANAOTOA MATAMKO KWA MASLAI YA WANASIASA.....VIONGOZI wa dini wanaotoa MATAMKO BAADA YA KUHONGWA PESA NA WANASIASA....refer aliyoyasema Dr. SLAA juu ya kuhongwa kwa VIONGOZI wa DINI na ENL........Haya matamko yangekuwa na IMPACT atleast angesema MZEE WA WATU MWAKASEGE.... he is too NEUTRAL.....
 
Hata mijini njaa ipo ila watu wanasaidiwa na akiba yao ya fedha.
HIKI NI NINI ULICHOANDIKA????....eti mjini kuna njaa ila watu wanasaidiwa na AKIBA YAO YA PESA........viroba hivi vinatuharibia VIJANA WETU AISEEEH
 
Huwezi kuelewa kutokana na mfumo wa elimu uliokujenga. Mjini wengi hawapati chakula kutoka katika mashamba yao Bali madukani,sokoni au supermarket na huko ni pesa zitokanazo na kazi wafanyazo.
Kijijini akioatacho shamba ni chakuka na pesa kutokana na chakula atakacho uza. Hivyo ukame ndio ukomo wa yote
 
Mmechanganyikiwa na propaganda zenu uchwara, umechukua picha ya Godwin Gongwe analia eti mkaandika wananchi wake wanashindia maembe, amekanusha peupe na amewaacha uchi, picha ya muda mrefu kwenye msiba wa rafiki yake.
 
Tujifunze kuipenda nchi yetu jamani. ..tukatae mbinu za wazungu. ..MWENYE ENZI MUNGU IBARIKI TANZANIA MILELE. ...AMEN RA
 
Mjini wengi hawapati chakula kutoka katika mashamba yao Bali madukani,sokoni au supermarket na huko ni pesa zitokanazo na kazi wafanyazo.
Kumbe mjini watu wanapesa za kwenda kununua VITU SUPERMARKET...daah aiseeh....SASA MBONA KILA SIKU MNAPIGA KELELE HUMU YA KUWA MH. RAIS kaficha PESA?????......hiki kizazi cha NDIMI MBILI ni hatari sana...na hii yote ni urithi mnaopata toka kwa KINA MSIGWA...LISSU....MBOWE maana hawa VIONGOZI kwa ndimi mbili ni BALAAA....sasa naona na VIJANA mmeisharithi......na kamwe hamjui mnasimamia nini...
 
Viongozi wa DINI MAKINI??????......kumbe wapo ambao si makini????...sasa ebu tuthibitishie UMAKINI wao umeupima vipi????.......NCHI hii hakuna VIONGOZI wa DINI....bali kuna viongozi wa DINI MASLAHI....VIONGOZI WA DINI WACHUMIA TUMBO....VIONGOZI WA DINI WANASIASA......refer UCHAGUZI WA MWAKA 2015....ndio utatambua NCHI HII HAINA VIONGOZI WA DINI.......VIONGOZI WA DINI WANAOTOA MATAMKO KWA MASLAI YA WANASIASA.....VIONGOZI wa dini wanaotoa MATAMKO BAADA YA KUHONGWA PESA NA WANASIASA....refer aliyoyasema Dr. SLAA juu ya kuhongwa kwa VIONGOZI wa DINI na ENL........Haya matamko yangekuwa na IMPACT atleast angesema MZEE WA WATU MWAKASEGE.... he is too NEUTRAL.....
Kiongozi wa dini makini anaweza kuonekana kwa kauli zake.
Pengo alisema hali ya uchumi imekuwa bora kipindi hiki cha awamu ya tano.
Shoo akasema hali ya uchumi imekuwa ngumu.
Magufuli akasema (tena kanisani) kuwa hali itakuwa ngumu hadi fedha zikosekane makanisani.
Kati ya Pengo na Shoo (viongozi wa dini) nani ni kiongozi makini?
 
Inawezekana kabsa wakakusanywa kikundi cha WANYWA VIROBA wakaambiwa waseme wanashindia na kulalia MAEMBE....kwa lengo tu la KUNUFAISHA wachache.......
Kwa naneno haya ndio thread inapata uhalali.
Nguvu kubwa inatumika kuunga mkono kauli mbaya za mkuu.
Kwa hiyo wananchi wakisema taabu inayowakabili lakini ni kinyume na atakavyo mtukufu basi wamenyweshwa viroba?
Wale wamama wazee na vikongwe kweli twaweza waambia ni wanywa viroba? Taifa lina laana!
 
Serikali imeamua kusambaza tani milioni 1.5 za mahindi,,,, sijui kwa ajili ya nini?
 
Kuna nguvu kubwa sana inatumika kwa viongozi wa kuteuliwa kuunga mkono kauli ya mkuu kuwa hakuna njaa na vyombo vya habari kadhaa kama Star TV na Uhuru. Lakini vijijini kwenye walaji wenyewe wanapohojiwa wanakiri kuna njaa. Hata mijini njaa ipo ila watu wanasaidiwa na akiba yao ya fedha.
Tumeona na viongozi wa dini makini ambao wanapata data zao kutokea chini kabisa nao wanesema ipo shida na tuwaombee viongozi waione na kuchukua hatua.
Utetezi wa hao wanaounga mkono kuwa hakuna njaa ni eti wanasiasa na wafanyabiashara ndio wanapotosha.
Jee kutokuwepo njaa ni vyakula kujaa kwenye maghala ya serikali wakati wananchi wanalalia embe?
HAKUNA NJAA KWASABABU WALIOTUZUNGUKA WOTE HAWAJATANGAZA NJAA=== MAAJABU YA MWAKA
TUNAGAWA TANI 15 MILION ZA CHAKULA...........WANAPELEKEWA KINA NANI==== AJABU LA TISA LA DUNIA
HAKUNA MTU KUTANGAZA BAA LA NJAA====== ONLY IN TZ DW WAKOWAPI WATUSAIDIE KUIAMBIA DUNIA MAANA HAPA TZ IKITANGAZWA GAZETI HUSIKA LINAPIGWA NYUNDO
 
Viongozi wa DINI MAKINI??????......kumbe wapo ambao si makini????...sasa ebu tuthibitishie UMAKINI wao umeupima vipi????.......NCHI hii hakuna VIONGOZI wa DINI....bali kuna viongozi wa DINI MASLAHI....VIONGOZI WA DINI WACHUMIA TUMBO....VIONGOZI WA DINI WANASIASA......refer UCHAGUZI WA MWAKA 2015....ndio utatambua NCHI HII HAINA VIONGOZI WA DINI.......VIONGOZI WA DINI WANAOTOA MATAMKO KWA MASLAI YA WANASIASA.....VIONGOZI wa dini wanaotoa MATAMKO BAADA YA KUHONGWA PESA NA WANASIASA....refer aliyoyasema Dr. SLAA juu ya kuhongwa kwa VIONGOZI wa DINI na ENL........Haya matamko yangekuwa na IMPACT atleast angesema MZEE WA WATU MWAKASEGE.... he is too NEUTRAL.....
Mwakasege uzuri wake sio kiongozi wa dini, ni Mwalimu. Anawalisha watu neno la Mungu.
 
Kumbe mjini watu wanapesa za kwenda kununua VITU SUPERMARKET...daah aiseeh....SASA MBONA KILA SIKU MNAPIGA KELELE HUMU YA KUWA MH. RAIS kaficha PESA?????......hiki kizazi cha NDIMI MBILI ni hatari sana...na hii yote ni urithi mnaopata toka kwa KINA MSIGWA...LISSU....MBOWE maana hawa VIONGOZI kwa ndimi mbili ni BALAAA....sasa naona na VIJANA mmeisharithi......na kamwe hamjui mnasimamia nini...
Kwako wewe kununua bidhaa zako supermarket ni kuwa na Pesa nyingi? Una mawazo analog kweli!
 
Back
Top Bottom