Ngumu kumeza lakini ndio Tanzania yetu hio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngumu kumeza lakini ndio Tanzania yetu hio

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Crucifix, Aug 1, 2012.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Tumeshuhudia utawala wa sasa ukitumia vyombo vya dola kama nyenzo na matokeo yake wote mmeona. Nchi imekuwa ngumu kutawalika, ufisadi umeongezeka, rushwa hadi bungeni!!! Uchaguzi uliopita ulimleta msemaji wa jeshi kuhusu utaratibu; lakini hapaswi kuongea hata pale nchi inapovamiwa - bali waziri ndiye mwenye jukumu. Mabomu ya machozi yamerindima kila kona na sasa hadi watoto wa shule (primary) nao wamepuliziwa. Usalama wa Taifa leo ni mtuhumiwa wa utekaji na utesaji, lisemwalo lipo...........

  Kada zote, kuanzia rais, makamu hadi mlalahoi tumekuwa wajasiriamali; wakubwa kwa wadogo. Na hatulipi kodi ipasavyo. Kodi wameachiwa walevi (samahani kwa wanywaji) na wavuta sigara. Sisi ni taifa la wabangaizaji! AIBU. Usistaajabu utakapoambiwa SIDO wanalipa kodi kuliko benki.

  Leo wamegoma madokta, kesho walimu, jana wa migodini. Life expectancy 44yrs mafao uyasubiri 55yrs. Sheria za game zinabadilishwa dakika 90 bado! Wakitangaza kugoma serikali inakimbilia mahakamani. Majaji na mahakimu ni wateule wa rais. Duh! Utawala unatumia mabavu zaidi! Polisi wamekuwa watii hata kuwapiga virungu watu wanaotetea maslahi yao!

  Chama cha wafanyakazi (TUCTA) mimi nakiita 'bukta' hakina meno! Bunge haliwezi kukemea serikali tena! Kila mbunge wa CCM anavizia uwaziri. Vyama vya upinzani vinafukuza wabunge machachari. NGO zinajaribu lakini ndio kila siku utawasikia kina 'analialia' Nkya tu! Hao hao. Ina maana hakuna wanaharakati wengine wa kuongeza nguvu? Akina Baregu walinyimwa ajira na kina Marando 'imara' wanatetea watuhumiwa wa serikali, hiyohiyo wanayoipinga!

  Wenye 'kiherehere' wanalishwa 'polodium' na wakinusurika wanazawadiwa uwaziri. Urais unatafutwa hadi kwa waganga wa jadi. Uhasama katika siasa unatisha. Hii nchi inakwenda wapi? Leo mgomo wa wafanyakazi wa mgodi mmoja tu unatikisa matajiri wa marekani, nchi yenye akiba kubwa ya dhahabu kuliko zote duniani.

  SITASUBIRI 2015. NITATUMIA FURSA YOYOTE ITAKAYOPATIKANA KUELEZA UKWELI NA KUUTEKELEZA. LIWALO NA LIWE. MKINIOKOTA MABWEPANDE MJUE NA NYINYI MKO NJIANI.

  Ngumu kumeza lakini ndiyo Tanzania yetu aliyotupatia Mungu, ni sisi wenyewe tunashindwa kuibeba.
   
 2. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mhh...Noted
   
 3. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Hii ndo inaitwa Bongoland Tanzania chini ya Chama Cha Majambazi. What do you expect?
   
 4. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  100% perfect!
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  Hili nalo neno! Mabavu kila mahali!
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa
   
 7. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You are a GREAT THINKER WA UKWELI.
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  hamna kitu!
   
 9. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Unaposema who jah bless, no one curse - kisha hamna kitu....huyo jah wako atakuwa mwendawazimu kuliko watawala wa nchi hii. Sisi Jah wetu, ni Mungu aliye hai anajua kuna kitu (sio hamna kitu). Hali ya nchi inasikitisha. wafanyakazi serikalini leo tarehe 2 mishahara hamune! Waziri anaongelea kuhusu ujenzi wa reli ili wabunge wapige makofi! reli iko wapi? Mjumbe wa bodi ya shirika la umma analipwa mshahara badala ya posho moja tu ya kikao anachohudhuria? Kila shule ya kata ina bodi inayopaswa kukutana mara nne kwa mwaka bali hukutana mala moja tu! Unasema hamna kitu. Siku si nyingi yatakutoka machozi utakapokwama sehemu kwa sabau huna rushwa ya kutosha............laana hii na ikutafune
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu,namna unavoona wewe mambo c lazima na mwingine aone kwa muono huo huo. Hakuna haja ya kutamkiana "laana",besides huna ubavu kumtangazia/mwombea mtu hayo wewe!
   
 11. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ndio maana nimekushangaa unaposema "hamna kitu" sivyo mimi nionavyo, mbona unameza matapishi yako mwenyewe? Nchi hii haitaendelea kwa sababu ya vijitu kama wewe. Badala ya kutoa mawazo yako, wewe kazi yako kutoa matamshi ya kijingajinga tu humu! Nakwambia hiyo laana ya kupuuza hali na ikutafune! Endelea kusema sina ubavu wa kukulaani........
   
 12. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Leo hadi wachungaji tuliodhani ni wapakwa mafuta wa Bwana wanaiba hadi umeme!!!!!!!!!!
   
 13. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu crucifix nime kukubali sana hachan na hoyu mla "nyasi", ndipo akili zake zilipo ishia. hii ni nchi yetu tutaipigia kelele mpaka mwisho "bravo mkuu"
   
 14. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,228
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Good, but, how long did you construct this?!, it looks copmrehensive.
   
 15. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  The 'Arab Spring' has almost played its course. Whether it has succeeded or not it is not for me to say. What we need now is to start an 'African Summer'. Anybody ready to join me on the streets? If not you are a coward and you have no right to complain or speak about change that you are not ready to bring about.
   
Loading...