Ngoswe penzi kitovu cha uzembe

A man with one idea

Senior Member
Jul 18, 2022
126
264
PENZI KITOVU CHA UZEMBE

KISA CHA NGONSWE NA MAZOEA KWENYE SENSA

MITOMINGI: nadhani sasa mgeni amekwisha kumaliza kula hebu nenda kaondoe vyombo.

MAMA MAZOEA: Basi fanya haraka (Mazoea anatoka, anaenda kwa Ngoswe alipo).

MAZOEA: Hodi! Hodi!

NGOSWE: Karibu.

MAZOEA: (Akiingia). Ahsante. Nimekuja kuchukua vyombo.

NGOSWE: Vyombo! Kaa basi mbona unasimama kama vile hakuna viti.

MAZOEA: Nimeambiwa nifanye haraka.

NGOSWE: Mmm! Haya ngoja ninawe basi (Ngoswe ananawa kwa taratibu jicho likiwa usoni mwa Mazoea ambaye anatazama kando). Hivo mzima wee?

MAZOEA: Bee!?

NGOSWE: Salama?

MAZOEA: Salama tu.

NGOSWE: Sasa ndio umekataa kukaa?

MAZOEA: (Ajidai hakusikia) Si umekwisha maliza?

NGOSWE: Bado kidogo.

MAZOEA: Basi nitakuja chukua baadaye. (Ataka kutoka)

NGOSWE: Basi nenda navyo. (Mazoea anarudi kuinama kuvichukua. Ngoswe kwa sauti ndogo). Hivyo waitwa nani?

MAZOEA: Mie?

NGOSWE: Ndio wewe hapo kisura.

MAZOEA: (anatabasamu huku akiondoka). Mazoea!

Story ni tamu ila tulishaambiwa ya Ngoswe tumuachie Ngoswe!

JIANDAE KUHESABIWA.
 
PENZI KITOVU CHA UZEMBE

KISA CHA NGONSWE NA MAZOEA KWENYE SENSA

MITOMINGI
: nadhani sasa mgeni amekwisha kumaliza kula hebu nenda kaondoe vyombo.

MAMA MAZOEA: Basi fanya haraka (Mazoea anatoka, anaenda kwa Ngoswe alipo).

MAZOEA: Hodi! Hodi!

NGOSWE: Karibu.

MAZOEA: (Akiingia). Ahsante. Nimekuja kuchukua vyombo.

NGOSWE: Vyombo! Kaa basi mbona unasimama kama vile hakuna viti.

MAZOEA: Nimeambiwa nifanye haraka.

NGOSWE: Mmm! Haya ngoja ninawe basi (Ngoswe ananawa kwa taratibu jicho likiwa usoni mwa Mazoea ambaye anatazama kando). Hivo mzima wee?

MAZOEA: Bee!?

NGOSWE: Salama?

MAZOEA: Salama tu.

NGOSWE: Sasa ndio umekataa kukaa?

MAZOEA: (Ajidai hakusikia) Si umekwisha maliza?

NGOSWE: Bado kidogo.

MAZOEA: Basi nitakuja chukua baadaye. (Ataka kutoka)

NGOSWE
: Basi nenda navyo. (Mazoea anarudi kuinama kuvichukua. Ngoswe kwa sauti ndogo). Hivyo waitwa nani?

MAZOEA: Mie?

NGOSWE: Ndio wewe hapo kisura.

MAZOEA: (anatabasamu huku akiondoka). Mazoea!

Story ni tamu ila tulishaambiwa ya Ngoswe tumuachie Ngoswe!

JIANDAE KUHESABIWA
.
Nilitokea kukielewa hiki kitabu . "Sarawili yake kama kengele za bomani ".

Mwingine analalamika kupunjwa miaka.

Mama anaficha watoto wake anaogopa watarogwa (mara mtoto anatokezea mama panya kaingia kwenye mtungi).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom