Hii stori ina la kujifunza

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
*MITOMINGI*; nadhani sasa mgeni amekwisha kumaliza kula hebu nenda kaondoe vyombo

*MAMA_MAZOEA*; Basi fanya haraka (Mazoea anatoka, anaenda kwa Ngoswe alipo).

*MAZOEA*; Hodi! Hodi!

*NGOSWE*; Karibu

*MAZOEA*; (Akiingia). Ahsante. Nimekuja kuchukua vyombo.

*NGOSWE*; Vyombo! Kaa basi mbona unasimama kama vile hakuna viti.

*MAZOEA*; Nimeambiwa nifanye haraka.

*NGOSWE*; Mmm! Haya ngoja ninawe basi (Ngoswe ananawa kwa taratibu jicho likiwa usoni mwa Mazoea ambaye anatazama kando). Hivo mzima wee?

*MAZOEA*; Bee?

*NGOSWE*; Salama?

*MAZOEA*; Salama tu.

*NGOSWE*; Sasa ndio umekataa kukaa?

*MAZOEA*; (Ajidai hakusikia) Si umekwisha maliza?

*NGOSWE*; Bado kidogo.

*MAZOEA*; Basi nitakuja chukua baadaye. (Ataka kutoka)

*NGOSWE*; Basi nenda navyo. (Mazoea anarudi kuinama kuvichukua. (Ngoswe kwa sauti ndogo). Hivyo waitwa nani?

*MAZOEA*; Mie?

*NGOSWE*; Ndio wewe hapo kisura.

*MAZOEA*; (anatabasamu huku akiondoka). Mazoea!i

Story ni tamu ila tulishaambiwa ya Ngoswe tumuachie Ngoswe! ! !

 
You take me far Back to form tatu aisee mazoea ngoswe cjui kina takadini na kina mama ntilie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom