NGOs zalia njaa fedha za UKIMWI

Nzowa Godat

JF-Expert Member
Jun 15, 2011
2,759
794
VYAMA vya kiraia
vinavyoshughulikia
mapambano dhidi ya
maambukizi mapya ya Ukimwi,
vimeanza kukosa kazi
kutokana na uhaba wa fedha
za uendeshaji, baada ya
wafadhili wa nje kupunguza
misaada ya kifedha na wengine
kuwakimbia.
Mwenyekiti wa Mtandao wa
Vyama vya Watu Wanaoishi na
VVU nchini (Tanopha), Julius
Kaaya, alisema hayo Dar es
Salaam, wakati akiwasilisha
taarifa ya shughuli za mtandao
huo kwa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Masuala ya Ukimwi.
Kwa mujibu wa Kaaya,
wafadhili waliokuwa
wakiwapatia misaada hiyo ya
kifedha, wamekuwa
wakijiondoa taratibu kwa
kadiri siku zinavyokwenda na
kufadhili miradi mingine.
“Nafikiri ni kwa sababu
wameona suala la Ukimwi
limezoeleka sana nchini na
kwamba pengine sio tatizo
kubwa kama zamani,” alisema
Kaaya.
Alifafanua kuwa dhana hiyo
siyo sahihi kwa sababu virusi
vilivyopo ndani ya damu,
vinaendelea kubaki pale pale
na kumuumiza aliyenavyo kwa
ukubwa ule ule hata kama
watu wamelizoea tatizo.
“Nafahamu kupunguza kwao
ufadhili au kujiondoa kabisa
hakumponyi mwenye VVU,
bali kunamuongezea mzigo wa
matatizo kutokana na
kumkwamisha kuendesha
shughuli alizokuwa akizifanya,”
alisema Kaaya.
Kutokana na hali hiyo, Kaaya
alipendekeza Serikali iingilie
kati na kubeba jukumu la
kufadhili
masuala ya Ukimwi kwa
asilimia 100 ili watu wake
wasiumie. Nawasirisha.
 

OMGHAKA

Member
Aug 15, 2011
97
23
Serikali ipo bado haijajitoa, na kuna ARV nyingi zinaagizwa mpaka nyingine zinaoza stoo. Tatizo NGO zinataka kupambana na UKIMWI kwa kupiga na kucheza ngoma, sasa hapa inatia shaka kama wanapambana na tatizo la UKIMWI au njaa zao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom