NGONO: Wanawake na Wanaume tunapoamua 'kujiachia' na Madhara yake…

Shem nimekuitika kwa mapenzi ya dhati.

BTW leo jumatatu, weekend ulijiachiaje na bro wangu?

Nashukuru sana kwa kuitikia... Bro wako hana wasi wasi when it comes to that! Lol

Kujiachia muhimu shem... Hasa kama unaye umpendaye na anakushibisha kiasi kwamba hujuitii kujiachia kwake.
 
Sijambo bibie - Vipi wewe u mzima? Sijajiachia siku nyingi japo!

Ha ha ha! Baba Enock umenichekesha hadi wamenishangaa hapa... Vipi Mama Enock kasafiri au wewe ndiyo umesafiri? :A S 39:

Mie mzima wa afya... Nafurahi kusikia na wewe haujambo pia.
 
Dada AshaDii Millions of Thanks kwa uzi wako uliojaa tafakari mwanana. Pamoja na mengi, nimeguswa na quote hii..

Kujipenda, haina maana kujipenda sura na mwili tu... Kujipenda ni pia kujitazama 'Pride' na 'Dignity' yako ina thamani ipi.
Wajameni tukumbuke kufanya mapenzi ni zaidi ya kufurahisha vikojoleo vyetu. Wakati unapofanya mapenzi unajivua aibu na usiri wako kwa kuonyesha viungo vyako yule unaye mnaniii..

Mwili wako ni pride na dignity yako!!!...kuonyesha vikojoleo hadi kwa housegirls na shambaboys ni kuukosea haki mwili wako..hakuna mapenzi, au ushindi kuwa wewe ni rijali !
 
Dada
AshaDii
Millions of Thanks kwa uzi wako uliojaa tafakari mwanana. Pamoja na
mengi, nimeguswa na quote hii..

Wajameni tukumbuke kufanya mapenzi ni zaidi ya
kufurahisha vikojoleo vyetu. Wakati unapofanya mapenzi unajivua aibu na
usiri wako kwa kuonyesha viungo vyako yule unaye mnaniii..

Mwili wako ni pride na dignity yako!!!...kuonyesha
vikojoleo hadi kwa housegirls na shambaboys ni kuukosea haki mwili
wako..hakuna mapenzi, au ushindi kuwa wewe ni rijali !

I think you hav a point here ....
 
AshaDii huu wimbo ni mzuri sana, lakini kwa bahati mbaya nadhani watu wanaopenda kucheza nyimbo kama hizi ni wachache sana..... Inasikitisha lakini ukweli ndo huo.
watu siku hizi tumekuwa kama akili zimefyatuka kidogo..... hii siyo kwa vijana wa siku hizi tu, hata watu wazima tunawashuhudia jinsi wanavyopenda kujiachia.....
Nina bahati nzuri huwa nina marafiki wa rika nyingi sana, wengine wana watoto ambao wanakaribia kulingana na mimi.... full kuwaita mama, wengi wanadhani ni mama zangu kumbe ni rafiki zangu. kwa vile ni marafiki basi huwa tunaendelea na story za kawaida za marafiki wanazopiga, sometimes huwa naishia kushangaa kichwani kwangu, naogopa kuwashangaa live, hadithi zinatisha na maisha yanaendelea.
watu wengi siku hizi hawathamini kabisa miili yao, pamoja na matishio yote tunayoyaona yanayotokana na kujiachia lakini watu utafikiri tumetiwa pamba masikioni na tuna upofu, hatusikii wala hatuoni, ni balaa tupu. sijui huko mbele hali itakuwaje yaani
 
Last edited by a moderator:
Mkuu AshaDii, baadhi ya watu hawana woga kabisa katika hili jambo la kujikinga. Kuna njemba mmoja yeye alikuwa anaokoteza hovyo hovyo hata wale waliovaa soksi (hawa ni wale wamepigwa vumbi la kutosha ukiangalia tu miguuni utadhani wamevaa soksi kumbe ni vumbi) Njemba ilikuwa inadai lazima inanihii kila siku vinginevyo akili yale haifanyi kazi. Sijui akili ya kichwa kikubwa au kidogo. Njemba bahati mbaya ikagusa mawayawaya na baada ya kuugua kwa muda mrefu ikarudisha namba.

Kuna baadhi ya akina dada inadaiwa kwamba njemba ikitumia kinga wanajiona wamedharauliwa kama vile wamewekwa kundi moja na machangu doa na huweza kuzua kizaazaa cha kutisha, "Kama ulikuwa unajua utavaa ndom si ungeenda kwa chandu doa tu!? Mimi si muhuni wa kuvaliwa ndom kwa kuvaa ndom unaonyesha kwamba unaniogopa naweza kukupa mawayawaya" na baadhi ya njembas wamesikika wakisema, "Yule binti alivyoumbika hutakiwi kuvaa ndom vinginevyo utapata laana ya Mungu" kwa kauli kama hizi ndio maana maambukizi bado ni mengi sana.

Kuna baadhi ya njemba hutembea na zana 24/7 kwa kujua wakati wowote ule zinaweza kuhitajika na hivyo kutumika katika kujikinga na maambukizi lakini hutokea baada ya kupata kilevi baadhi husahau zana zao na kujirusha pekupeku wakija kustuka kesho yake ndio wanagundua kwamba walipiga game peku peku. Baadhi hubaki na majuto mjukuu.

Miaka michache iliyopita nilisoma katika gazeti mohja nchini kwamba management ya TANESCO na tawi la jumuiya ya wafanyakazi walikuwa wakutane katika kupanga taratibu za namna ya kupunguza Wafanyakazi miezi michache baadaye nikasoma tena zoezi la kupunguza Wafanyakazi wa TANESCO halitakuwepo tena kwa kuwa kumetokea vifo vingi. Nilifuatilia kwa karibu kwa baadhi ya marafiki pale TANESCO na wao wakathibitisha kwamba ni kweli katika kipindi kifupi kumetokea vifo vingi na kuna wakati walikuwa wakihudhuria kati ya vilio vitatu na zaidi vya Wafanyakazi wenzao. Hali inatisha kusema kweli sukari imeingia sumu.

Upo sawa kabisa Blue G. Naomba nitoe mtazamo wangu wa kwanini such an attitude?

Wengi ni kuwa tuko waoga sana wa kupima afya zetu upande wa HIV/AIDS tokana na ngono zembe ambayo tunafanya. Hiyo ya 'wacha tule raha' mara nyingi hutokana na mtu kuto jua afya yake na anaona ni kheri tu aendelee kujilipua kwa woga wa kupima.

Ndiyo maana unaweza kuta aliye kuwa anaongea hivo akilazimika kupima na akajikuta kuwa afya yake ni HIV (-) kwa kiasi kikubwa wengi hubadilika kabisa na kuacha kabisa ngono zembe na kumfanya awe makini zaidi.

Hili suala la HIV/AIDs ni kubwa sana. Na ni janga ambalo kwa kiasi kikubwa wengi limetukuta. Ila bahati mbaya ni kuwa wengi hatujui sababu tupo waoga mno kutambua afya zetu pande hizo.
 
Last edited by a moderator:
nderingosha... Asante sana. Umezungumzia suala la tamaa vema sana, na nimependa the fact kuwa umeona wazi kuwa hiyo ni kwa wote iwe wanawake ama wanaume. Na nadhani hii sababu ndiyo hasa inashika hatamu ya sababu zote zinazopelekea kujiachia kwa wengi.

..……kinachouma ni kuwa jamii ya Mtanzania imeathirika na hii kitu (tamaa ya ngono) kwa ujumla….kuanzia mkubwa kwa mdogo….Unakuta mtu ana mke wake mrembo na wamekuwa kwenye ndoa au mahusiano kwa miaka mingi bila baadhi ya vitu (material)…..kama gari kwa mfano..lakini anatokea mmoja wao kukutana na mtu (malaya/fisadi)anampa gari..na malipo yake yanakua ni kujiachia (ngono)….matokeo yake ndoa/mahusiano yake na mtu wake yanaharibika….na wengine (wanawake)wanajitoa jumla mpaka tiGo…kama malipo ya vitu wanavyopewa (ambavyo hawakuwa navyo awali)….Mwanamke akihojiwa na mmewe gari katoa wapi anasema kakopa saccos na maisha yanaendelea na mchezo unaendelea….

….rafiki yangu kanambia kuna family wana mtoto wao binti mdogo wa form 2 ambaye walikuwa hawajawahi kumnunulia simu……lakini majuzi amekuja home akiwa na simu 3 (zote smart phones)…akiulizwa anasema kapewa zawadi…..Wanaomjua wanasema zote kapewa na wanaume watatu (watu wazima) tofauti wanaomla…mtoto mdogo huyo…..kisa anataka vitu (material)…alafu mnashangaa kwanini watoto wanafeli siku hizi!!...hao ndio wagawa tiGo wakubwa mjini…..Ukitaka kujua hili pita mashuleni ulizia….kwa Dar anza na Kinondoni….utashangaa……na haijalishi…ni wasichana kwa wavulana….Baba na mama hawana hata muda wa kujua maendeleo ya mtoto shuleni…….kwa kuwa nao wote wako bize kutafta vitu (material)….

..Nimewahi kuona (true story) kule zenj…..familia moja yenye baba, mama na watoto wa kike (watatu)….woote family nzima walikuwa wanajiuza (bila mmoja kumjua mwingine)…ili kutafta vitu (material)….Mama anatoka anaenda kwa mabasha zake wanampa hela ya kujipamba……..baba nae (shoga) anatoka anaenda kwa mabasha zake wanampa hela ya mboga na home…..mabinti nao wanatoka kila mtu kwa nafasi yake kimtindo…..wanaenda kwa mabasha zao wanapata matumizi…….baba yeye anahakikisha family inakula tu…..mambo mengine kila mtu atajijua……lakini jioni wote wanakutana kama family…..na maisha yanaendelea….

Hii picha iko sana mijini (kama Dar)…sema tu haisemwi katika bigger picture…..na inatokea si kwa member wote wa family…Mnashangaa tu matokeo yake…..magonjwa kuongezeka, ndoa kuvunjika……watu kutoaminiana kwenye mahusiano….watu kuibiana wapenzi…..watoto kuharibika……mimba kwa watoto…na hata mayatima mitaani…….ufisadi (maana watu wanaiba ili wapate vitu na pia waweze kuhonga vitu)…etc …etc……yoote hii kwasababu watu wako bize kutafta vitu (material)……tamaaa kwa vitu wasivyonavyo………Wanaume wanawazengea wanawake wenye hela kwa kupitia ngono ili wapate vitu….vile vile wanawake….Ngono (na ufisadi) imekua short cut ya kupata mali….kwa watu woote…wakubwa kwa wadogo….na hata maskini na matajiri…

…msingi wa kupata mali siku hizi umekuwa si kufanya KAZI kwa bidii…….bali NGONO…na UFISADI…na hii ni kwa miji mingi mikubwa (haswa Dar)…..Anayefanya kazi kwa bidii….na asiyetoa ngono….ni ----….haya ndo maisha ya mjini….sifa ni kuwa na vitu vingi/wapenzi wengi..…na kwa gharama yoyote…hata kama uwezo hana…alafu watu wanajidanganya kuwa hayo ndo maendeleo…..People are not real yaani…..Kwa nilivyokusoma Asha…..yaelekea wewe ni kati ya wachache mliotulia kwenye mahusiano…na unayekula jasho lako….keep the good faith……..ciao!!!

Angalizo: Isionekane kuwa nime generalize…maana kuna watu wengi tu wana enjoy mahusiano yao..na wanakula jasho lao pia….Hii matatizo ipo sana mijini…kama Dar..maana ndiko kuna vitu….
 
AshaDii huu wimbo ni mzuri sana, lakini kwa bahati mbaya nadhani watu wanaopenda kucheza nyimbo kama hizi ni wachache sana..... Inasikitisha lakini ukweli ndo huo.
watu siku hizi tumekuwa kama akili zimefyatuka kidogo..... hii siyo kwa vijana wa siku hizi tu, hata watu wazima tunawashuhudia jinsi wanavyopenda kujiachia.....
Nina bahati nzuri huwa nina marafiki wa rika nyingi sana, wengine wana watoto ambao wanakaribia kulingana na mimi.... full kuwaita mama, wengi wanadhani ni mama zangu kumbe ni rafiki zangu. kwa vile ni marafiki basi huwa tunaendelea na story za kawaida za marafiki wanazopiga, sometimes huwa naishia kushangaa kichwani kwangu, naogopa kuwashangaa live, hadithi zinatisha na maisha yanaendelea.
watu wengi siku hizi hawathamini kabisa miili yao, pamoja na matishio yote tunayoyaona yanayotokana na kujiachia lakini watu utafikiri tumetiwa pamba masikioni na tuna upofu, hatusikii wala hatuoni, ni balaa tupu. sijui huko mbele hali itakuwaje yaani

Mazingira ya makuzi na makuzi yenyewe yanaathiri sana tabia ya mtu... Si kwa asilimia zote ila ina nafasi kubwa sana. Inapokuwa wewe unawashangaa hao wa mama kufanya hivyo ina maana kuwa there is hope kuwa kuna watu ambao wapo straight na masuala kama haya wanazingatia hivyo kwa maana nyingine ni kuwa atajali makuzi ya watoto wake (hasa wa kike) kujitambua uthamani wao na miili yao.

Naomba nigusie kuwa haina taaabu kama mama mtu mzima anafanya hivyo lakini anazingatia makuzi ya watoto wake kwa kuegemea katika kujitambua, kujipenda na kujithamini. Huwa inasikitisha sana kama mtoto mdogo kama wa miaka 16 anaona the way mama yake anajiachia ovyo... Msingi wa huyo mtoto unakuwa umebomolewa kwa kiasi kikubwa sana.
 
Kuna baadhi ya akina dada inadaiwa kwamba njemba ikitumia kinga wanajiona wamedharauliwa kama vile wamewekwa kundi moja na machangu doa na huweza kuzua kizaazaa cha kutisha, "Kama ulikuwa unajua utavaa ndom si ungeenda kwa chandu doa tu!? Mimi si muhuni wa kuvaliwa ndom kwa kuvaa ndom unaonyesha kwamba unaniogopa naweza kukupa mawayawaya" na baadhi ya njembas wamesikika wakisema, "Yule binti alivyoumbika hutakiwi kuvaa ndom vinginevyo utapata laana ya Mungu" kwa kauli kama hizi ndio maana maambukizi bado ni mengi sana.

Umeeleza kwa kina saana BAK... Nimekupata vema nashukuru... As much as ni habari ya kusikitisha nimecheka mno suala la wa vumbi miguuni kana kwamba wamevaa soksi.

Hili ambalo nime quote hapa... Mie ni shahidi kabisa! Roomate wangu Chuo siku moja alikuja ana furaha sana dom, Kisa?? Eti mpenzi wake siku hiyo alilala naye bila Condom! Akieleza kuwa ilimuuma sana kuwa mara ya kwanza na ya pili Mpenzi wake huyo alitumia condom hivyo ilikuwa wazi kuwa alikuwa haaminiki ila sasa anaaminika...

Inasikitisha sana... Huyo anaye ongea hivyo ni mwana chuo... Just imagine yule ambae hajabahatika kusoma akakomboka? Ama yule aliye ishia kidato cha 4? Unabaki huelewi ni wapi tunaenda.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
..Nimewahi kuona (true story) kule zenj…..familia moja yenye baba, mama na watoto wa kike (watatu)….woote family nzima walikuwa wanajiuza (bila mmoja kumjua mwingine)…ili kutafta vitu (material)….Mama anatoka anaenda kwa mabasha zake wanampa hela ya kujipamba……..baba nae (shoga) anatoka anaenda kwa mabasha zake wanampa hela ya mboga na home…..mabinti nao wanatoka kila mtu kwa nafasi yake kimtindo…..wanaenda kwa mabasha zao wanapata matumizi…….baba yeye anahakikisha family inakula tu…..mambo mengine kila mtu atajijua……lakini jioni wote wanakutana kama family…..na maisha yanaendelea….

nderingosha... Umeongea mengi ya msingi na kufunza... Ila huu mfano wako... Nimeishiwa kabisa maneno! Hii sasa Laana!
 
Last edited by a moderator:
Post ambayo ulininukuu haikukaa vema nikashindwa kuelewa maoni uliyokuwa umetoa. Ndio maana nimeomba kama hutajali urudie kutoa maoni ulitoa.

aaah..ndio maana nikasema kwamba tumecho$hwa na mapenzi ya BBM...unajua nilicho maani$ha?
{1} mapenzi tumefanya kama fashion{2}uaminifu hakuna yaani ziro na {3} ni ajira kwa dada/mam zetu..mf: ukienda kuomba kazi hupati mpaka utoe rushwa ya ngono na imekuwa kawaida saaana...$o mtu mwenyewe ndio anachagua aishi vipi..ilimradi tu amani inapatikana...au $io $i$t.!
 
Sasa nimekupata na Asante kwa ufafanuzi... Nimependa zaidi hapo; kuwa mtu mwenyewe ndio anachagua... Upo sawa kabisa!
 
Kwa wanaume .mara nyingi haiachi footprint ila kwa wanawake lol lol lol lol ukijiachia tu waishia kuzeeka na kudharauliwa kusikoish ,ndio sababu unasikia wakisema huyu mwanamke ni malaya na wanaume wanasema huyu mwanaume ni mhuni hahahahah.asante dada AshaDii hii ni mad nzudi sana hasa kwa hawa vijana wetu waliomaliza form four na six na lastd7 kama wapo humu.hata wana chuo na wanaofanya kazi nakujiachia kama mzabzab

Tena kwa mwanaume jamii inamwona wa kawaida hata kama watasema aisee yule jamaa mhuni kweli (wanakuwa hawapo serious sana na kuchukulia poa) tofauti kama ikiwa ni kwa mwanamke watamsema vibaya yaani kama ni dada yako alafu ukakuta anasemwa unaweza kuzirai.

Wakati mwingine huwa najiuliza, pamoja na kwamba mwanaume anajulikana ni mhuni lakini ajabu mabinti bado wanamiminika kwake na pengine si kwamba ana hela au vipi na wadada ambao wanamfuata ni wadada hawa hawa ambao tunawaona wa kawaida. Hapa ni kujiuliza sijui wanafuata nini hasa pengine wana amini kwamba jamaa yupo fit kwenye masuala ya kumtosheleza mwanamke.
 
AshaDii huu wimbo ni mzuri sana, lakini kwa bahati mbaya nadhani watu wanaopenda kucheza nyimbo kama hizi ni wachache sana..... Inasikitisha lakini ukweli ndo huo.
watu siku hizi tumekuwa kama akili zimefyatuka kidogo..... hii siyo kwa vijana wa siku hizi tu, hata watu wazima tunawashuhudia jinsi wanavyopenda kujiachia.....
Nina bahati nzuri huwa nina marafiki wa rika nyingi sana, wengine wana watoto ambao wanakaribia kulingana na mimi.... full kuwaita mama, wengi wanadhani ni mama zangu kumbe ni rafiki zangu. kwa vile ni marafiki basi huwa tunaendelea na story za kawaida za marafiki wanazopiga, sometimes huwa naishia kushangaa kichwani kwangu, naogopa kuwashangaa live, hadithi zinatisha na maisha yanaendelea.
watu wengi siku hizi hawathamini kabisa miili yao, pamoja na matishio yote tunayoyaona yanayotokana na kujiachia lakini watu utafikiri tumetiwa pamba masikioni na tuna upofu, hatusikii wala hatuoni, ni balaa tupu. sijui huko mbele hali itakuwaje yaani
FP Umenitsha!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom