Ngome ya Zitto Kabwe yavunjwa


Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Leonard Mubali, Kigoma

KAMATI Maalum ya Ushauri ya mkoa wa Kigoma imevunja ngome ya kisiasa ya mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe baada ya kupitisha mgawanyo wa majimbo katika wilaya za Kigoma na Kasulu.

Endapo mapendekezo ya kamati hiyo yataridhiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (RCC), ngome kuu ya mbunge huyo machachari wa Chadema na mahala alipozaliwa patamegwa na kuingizwa katika jimbo Kigoma Mjini linaloshikiliwa na mbunge wa CCM, Peter Selukamba.


Kutokana na mgawanyo huo Zitto ataathirika kwa kukosa kura 20,688 za wakazi wa kata ya Mwandiga ambao sasa wameondolewa kutoka Jimbo la Kigoma Kaskazini na kupelekwa katika jimbo jipya la Kigoma ambayo ni sehemu ya manispaa ya Kigoma Ujiji.


Mwaka 2005 Zitto alishinda ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini baada ya kupata 28,198 akimbwaga kwa mbali mpinzani mkuu Halimeshi Mayonga wa CCM ambaye alipata kura 21,822. Sehemu kubwa ya ushindi wa Zitto ulipatikana katika kata ya Mwandiga


Wagombea wengine walioshiriki uchaguzi huo na kura zao kwenye mabano ni Matete Kaseba wa CUF (3,73 na Kassim Wamala wa DP (49).


Kutokana na mabadiliko hayo, kuna uwezekano mkubwa Zitto kwenda kugombea Kigoma Mjini na hivyo kuweka nafasi ya Selukamba katika hali tete.


Wachambuzi wengine wa mambo wanadai kwamba hatua ya RCC inaweza kumfanya Zitto kugombea jimbo mojawapo jijini Dar es Salaam ambako ana ushawishi mkubwa kutokana na kufanya kazi nyingi za kitaifa.


Akisoma maazimio ya kikao hicho ambacho hakikuhudhuriwa na mbunge mmoja yeyote wa mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Mkoa huo Joseph Simbakalia alisema, mkoa wa Kigoma sasa umependekezwa kuwa na majimbo 10 ya uchaguzi badala ya majimbo saba yaliyopo.


Katika manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Jimbo la awali la Kigoma Mjini limegawanywa na kupatikana majimbo mawili ya Kigoma na Ujiji ambapo wapiga kura 54,701 kutoka jimbo la Kigoma Kusini litakalojulikana kama Jimbo la Malagarasi watahamia katika Jimbo la Ujiji.


Simbakalia alisema kuwa baada ya mapendekezo hayo kupitishwa na NEC, Halmashauri ya Wilaya Kigoma itakuwa na majimbo matatu ambayo ni Buhingu na Malagarasi (yaliyokuwa Jimbo la Kigoma Kusini) na Kalinzi (lililokuwa jimbo la Kigoma Kaskazini).


Kwa hali hiyo kupitishwa kwa mapendekezo hayo kunaifanya wilaya ya Kigoma kuwa na jumla ya majimbo matano ya uchaguzi kutoka majimbo matatu yaliyopo sasa.


Aidha, mapendekezo hayo yaliyopitishwa na kamati ya ushauri ya mkoa yameifanya wilaya Kasulu kuwa na majimbo matatu ambayo ni Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini baada ya Jimbo la Kasulu Mashariki kugawanywa huku jimbo la Kasulu Magharibi likibaki kama lilivyo.


Hakuna mapendekezo yoyote yaliyotolewa na wilaya Kibondo katika mchakato huo wa kuongeza majimbo mkoani Kigoma na kwamba majimbo hayo kwa sasa yatabaki kama yalivyo.


Kama utetezi wao kuhusu kugawanywa kwa majimbo hayo Wakuu wa wilaya za Kasulu na Kigoma, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri walisema kuwa mapendekezo yao yamelenga kupeleka uwakilishi karibu na wananchi na kufanya huduma muhimu na maendeleo kuwafikia kwa haraka.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kigoma John Mongela alisema kuwa kutekelezwa kwa mpango maalum wa kiuchumi kutaifanya manispaa ya Kigoma Ujiji kuwa na ongezeko kubwa la watu na shughuli ambazo zinahitaji usimamizi wa karibu wa kiutawala.


Sambamba na hilo alisema kuwa wakati Manispaa ya Kigoma Ujiji ikiwa hivyo sehemu ya Lugufu ya Halamshauri ya Wilaya Kigoma itakuwa na shughuli nyingi za kilimo ikiwa ni kituo muhimu cha kilimo mkoani Kigoma ambacho kitachangia ongezeko kubwa la watu katika wilaya hiyo.
 
Fugwe

Fugwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,680
Likes
244
Points
160
Fugwe

Fugwe

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,680 244 160
tutashukuru pale tu mgawanyo huo utakapokuwa na matokeo chanya kwa wakazi wa majimbo hayo.

Nimeshindwa kuelewa mpaka wa jimbo la buhingu na kalinzi. Tusaidie hapo
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Mimi huwa napata na shinda sana kuona mgawanyo wa majimbo huwa mara nyingi sana katika sehemu za Upinzani tu na sio sehemu nyingine maana unaweza kuona hali kama hii hakuanza leo wa jana tokea kipindi cha Benjamin Mkapa
 
Ibrah

Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Messages
2,720
Likes
58
Points
145
Ibrah

Ibrah

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2007
2,720 58 145
Kugawawanya majimbo ya uchaguzi kwangu si tatizo; tatizo langu ni hapo kwenye kuongeza majimbo maana sioni faida yoyote zaidi ya kuongeza matumizi yasisyo ya lazima kwenye mambo yasiyo ya lazima. Pato la taifa bdo ni dogo sana na bado tunategemea wafadhili kuchangia bajeti yetu kila mwaka lakini kwa upofu tulionao bado tunataka kuongeza matumizi ya kuwalipa hao Wabunge!

Nashindwa kuelewa kabisa juu ya vipau mbele vyetu, yaani kuongeza idadi ya Wabunge ndo kipaumbele kweli? Shame! Kama tunadhani kuwa tuna mapesa ya kuwalipa hao wabunge walioongezeka basi ni vema kama tungezipeleka kuweye kuongeza miundo mbinu hasa bara bara maana huko Kigoma hali ni mbaya sana na badala ya Uongozi wa Mkoa kupeleka mapendekezo serikalini kueleza juu ya matatizo ya miundo mbinu wao wanakimbilia mapendekezo ya kugawa majimbo zaidi. Kigoma ndo Mkoa uliotengwa zaidi katika Tanzania kwa kukosa barabara za kuunganisha ni mikoa mingineyo; hivi kweli Wana-Kigoma wanahitaji ongezeko la wabunge na Majimbo kwa maendeleo yao? Shame on you leaders!
 
Wacha1

Wacha1

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2009
Messages
12,765
Likes
1,031
Points
280
Wacha1

Wacha1

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2009
12,765 1,031 280
Kuongeza majimbo ni sera ya kutafuna fweza ya walipa kodi. Karibu tutashindana na Zanzibar kuwa na wabunge wengi ambao kazi yao ni kuwakilisha matumbo yao. Hawa waliopo sijui kama kweli wanawakilisha wananchi walio wachagua zaidi ya mitumbo yao.
 
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2008
Messages
1,322
Likes
21
Points
135
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2008
1,322 21 135
Wasi wasi wangu ni kuwa wasipunguze majimbo 2015 kama walivyofanya kule Pemba.
 
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Messages
21,829
Likes
155
Points
160
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2008
21,829 155 160
Its another political move kwani mtoa habari hajarefer popote faida za kugawanya hilo jimbo, hatujaambiwa chochote zaidi ya serukama, zitto, kura na alipozaliwa zitto.... kama sababu ni hizo alizoandika mwandishi then we are really myopic, ila kama mwandishi ametaka iwe ya kisiasa zaidi then he thinks using his arse
kinachonisikitisha ni kwamba sijawahi kusikia wanaunganisha majimbo
 
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
1,338
Likes
127
Points
160
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
1,338 127 160
Leonard Mubali, Kigoma
Kwa hali hiyo kupitishwa kwa mapendekezo hayo kunaifanya wilaya ya Kigoma kuwa na jumla ya majimbo matano ya uchaguzi kutoka majimbo matatu yaliyopo sasa.
Hapa ndipo panaponipa shida kubwa, kuwa tunaweka mikakati jinsi ya kuila nchi badala ya kuijenga nchi. Majimbo mengi yamekuwa yakiwekwa zaidi kwa nia ya kuwapa mlo wanasiasa hasa inapoonekana kuna msuguano. Na kwa mtindo huu na ongezeko la watu Tanzania, sio ajabu mwaka wa 2050 Tanzania ikawa na majimbo zaidi ya 2000!

Ishu Tanzania ni jinsi ya kuila nchi na wala sio kuinjenga nchi, KUUMBEEE!
 
jmushi1

jmushi1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2007
Messages
19,444
Likes
5,548
Points
280
jmushi1

jmushi1

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2007
19,444 5,548 280
Utaratibu wa kuyagawanya maeneo ambayo wapinzani either wana nguvu ama wanaelekea kuya dominate ulianzia enzi za Mkapa na sasa naona bado unaendelezwa...Ni kama kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja kwani ni tactic ya kui neutralize nguvu ya upinzani na at the same time dividing and rule.
 
P

PUNJE

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2008
Messages
349
Likes
91
Points
45
P

PUNJE

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2008
349 91 45
......kwa nini wasiseme tuu, kata au tarafa au kila kijiji kiwe na mbunge?? Wataichangua nchii yote hatimaye tutafikia kuwa na mbunge kila mtaa!!!!!
 

Forum statistics

Threads 1,251,742
Members 481,857
Posts 29,783,194