NGOME J&U wana huduma bora, sambaeni mitaani pia.

NGOME J&U wana huduma bora, sambaeni mitaani pia.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,255
Reaction score
16,185
Mimi sijui kirefu cha Ngome J&U ila najua ni vituo vya kuuza mafuta ya Petroli kwa vyombo vya moto (Petrol stations) vinavyopatikana kwenye maeneo/kambi ya jeshi la wananchi JWTZ yanayotazamana na barabara kuu. Inawezekana ni vituo vinavyomilikiwa na jeshi kwakuwa viko maeneo ya jeshi na vina nembo ya JWTZ pia.

Ukweli wanatoa huduma bora sana kwa wateja, ombi langu wajitanue hata kwenye maeneo ya kawaida ya wananchi kutoa huduma hiyo badala ya kusalia kwenye maeneo yao ya jeshi tu. Hii itatusaidia watanzania wengi kupata mafuta wakati wote na vipindi vyote hata kukitokea migomo na ubabaishaji mwingine wa wafanyabiashara au machafuko. Lakini utajitanua kibiashara hata nyinyi na kuongeza mapato kama kampuni.

Vituo hivi ndivyo vilivyokuwa vinatoa huduma kwa watu hata pale vituo vyote vilipokuwa havitoi huduma.
 
Back
Top Bottom