Ngoma za mashetani

Kuna ngoma zinaitwa Dufu ndo zikoje hizo.
 
Bora umeuliza jirani, unakufaham kwa mwananyange?? Halaf naskia ukipita karibu kamauna jini kichwani waweza jiunganao kwenye ngoma yao, hapo itakua tukwa kibao
Wewe mdigo pia. Hebu tuambie kwa kina.
 
Wengi hata kimaendeleo wako nyuma sana,hilo kabila kwa Tanga ndo liko nyuma sana kiuchumi kielimu pia sababu ya shirki.
 
Umenichekesha kweli dada, inamaana kapewa dawa fekilakini tatizo lake likaisha!

Huoni ni mambo ya saikolojia tu hayo? Waganga wanapiga hela balaa na wateja hawaishi maana wajinga wapo wa kutosha

Lakini pia kuna dawa za mitishamba za magonjwa ya kawaida kama chango la watoto, vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa n.k
Hizi zipo na wanafanya watu ambao wala hawajiusishi na ushirikina
 
Hizo ngoma ni matawi ya Freemasonry na wote hao ni Freemasonry, sawa na ngoma za vodoo za west Africa.
Inawezekana kabisa mkuu, sio Afrika tu hata Caribbean kama Haiti na Dominica ambapo ngozi nyeusi ipo kwa wingi hizi mambo zipo
 
hahahaha sasa unataka kuyaona maziwa ya dada zako,mashangazi zako bibi zako utapofuka
Vijijini kwenye unyago,au kwenye mila zinazotahiri vifua wazi viko vingi tu kama mswati,utamaduni wa kuvaa nguo tumeletewa na wazungu.Aibu ni baada ya kuishi mjini vijijini sehemu zingine kuwa uchi ni kitu cha kawaida wala hakuna ashangae,mtoni mnaoga wote,hakuna anaejali.
 
Bro mambo ya kishirikina yote huongozwa na ujinga.

Pili,sijawahi kuona usecular ukioinga juu yamambo haya,labda unionyeshe leo ni wapi usecular unapinga mambo kama haya au mfano wake.
Usecular ndio nini!!
 
Kwani mkuu usomi kunakufanya MTU kusahau mila na utamaduni wako??
Hapana usomi haukufanyi usahau au upuuze mila Beef Lasagna

Kinachogomba hapa ni mila zisizofaa kama kutembea matiti wazi kwa wanawake tena wakiwa wamechanganyika dada, kaka, shangazi, mjomba n.k, kutukana matusi ya nguoni mbele ya watu wako unaowaheshimu, na mengi mengine yanayokera
 
utajitaftia laana shaur zako
Tanga wanazicheza sana
Wakati niko mdogo palikuwepo na babu basi walikuja watu wanaopandisha sisi tunaita (Majini) kumtibu mtu huyo ngoma zilikuwa zikipigwa na kufanya sherehe (Chano) na kafara (hapo utaaguliwa na kuchanjwa chale mwilini) kisha watakiweka dawa tena huwa wanafanya pale yule jini anapopataka mfano chini ya mti,njia panda au hata kwenye vile vijumba vya waganga ambavyo hujengwa maeneo maalumu kwa mujibu ya ndoto zao.

Mwishowe mtu anapona
(Chano inatumika pia pale mama mzazi anapoenda kwa babu na kuaguliwa kwa lengo la kumkinga mtoto na wanga au watu wenye vijicho ili asipigwe "zongo" na "visimo" tena vya kizeia

"Nakumbuka yule aliyeniibia shilingi 4,000,000 milioni nne na kwenda kwa yule babu yangu na baada ya siku nne yule mwizi alikuja kwangu na kiasi cha zile pesa hazijapungua na aliniomba msamaha eti nimsamehe alikosea"

Anyaway nilishaondoka kijijini kwa sasa niko mjini na haya mambo hayana nafasi tena kwangu
 
ndio mana nikakwambia imani kaka, mtu akiamini hua, yan nilicheka sana ile siku nikagundua waganga wengi sio wa kweli,
 
kuna ile shetani anataja jina nayo inakuaje?? Mimi haya mambo mekuja yaona huku tanga, karibu waganga wengi hufanya hivi hizi ngoma huku n maarufu sana na zile nai zikipulizwa mm zinanikera sana saa zingine hakuja kucha unazisikia ni kazi jaman mambo mengine
 
Dogoli, waathirika wengi ni kina mama wasio na elimu. Ni mara chache sana kukuta wababa na kina mama wasomi.
 
"Nakumbuka yule aliyeniibia shilingi 4,000,000 milioni nne na kwenda kwa yule babu yangu na baada ya siku nne yule mwizi alikuja kwangu na kiasi cha zile pesa hazijapunahagua na aliniomba msamaha eti nimsamehe alikosea"
Dah! Milion nne ikarudi nzima nzima mkuu, hahahaa si mchezo aisee

Inabidi Serikali watumie watu kama hao ili kudhibiti ufisadiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Mtu akipiga hela ya uma anajikuta anaingiwa na pepo la kuzirudisha yeye mwenyewe kama alivofanyaga Ngeleja zile za mgao wake wa Escrow 😎😎😎
 
Hapo kwenye unyago pia ni kwa nn mwari akichachezwa hutandikwa bakora hasa akiwa mjeuri??? Wanasema pia unyago una mizungu kiasi kupelekea wanaoicheza wengi kua washirikina kuna ukwelu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…