Ngoma za mashetani

Ngoma za mashetani

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
50,182
Reaction score
96,271
Mshana Jr Hapa mtaani kwa ndugu zangu wadigo leo ni siku ya tatu wanacheza ngoma za mashetani. Watu wamejaa, wengi. Magari huwezi amini wingi wake. Mbuzi, kondoo, kuku vinachinjwa , damu mbichi zinanyweka etc. Ebu tufahamishe ngoma za mashetani ndiyo kitu gani? Umuhimu wake ni upi?
 
Umezijuaje kama zinaitwa za Mashetani? Au umeshazipa jina tayari mkuu?
Kwa ufupi ngoma na vinanvyohusiana navyo ni matawi ya shetani. Sasa kuanzia hapo kama unataka kujua umuhimu wake itakuwa unahitaji licha ya UHASI wake (negativity).
 
hahaha huyo mama mtaani kwangu ni maarufu kwa hizo ngoma

Na sjui why zinajaaga mashoga ndio wachezaji

Me sjambo kaka angu hofu kwako
Hizo ngoma ni maarufu kwenye mikoa kama ya Tanga, Kigoma, Tabora, Mwanza na Dar na utashangaa kuna hata wasomi na watu wenye exposure huwa wanashiriki

Miye sijambo pia namshukuru Mola
 
sjui hua zina maana gani, na ng'ombe wanaochinjwa hapo si mchezo, nakumbuka niliwah kupita karibu mana hua watu wanajaaga nikaona huyo mama memtaja kwa mbele kaweka kitu kama mapembe na manyasi nyasi pembe kazifunga na kitambaa chekundu anaenda na beat ya ngoma ile nilikua na maswali mengi sana bora hii mada imewekwa hapa nipate kujifunza halaf sasa navosikia wanawekwa maziwa sjui miwa asali wanatenga kabisa katika sinia then wanaweka kwneye chumba kinajulikana kama kilinge yan ndio wametengewa hao mashetani hahahahaha naomba tu leo nijifunze mana naona kudanganyika tu na maswali kibao kichwan kwangu

Kumekucha kaka
 
Mshana Jr Hapa mtaani kwa ndugu zangu wadigo leo ni siku ya tatu wanacheza ngoma za mashetani. Watu wamejaa, wengi. Magari huwezi amini wingi wake. Mbuzi, kondoo, kuku vinachinjwa , damu mbichi zinanyweka etc. Ebu tufahamishe ngoma za mashetani ndiyo kitu gani? Umuhimu wake ni upi?
Hazina umuhimu zaidi ya watu kuzidhulumu nafsi zao.
 
Hizo ngoma ni maarufu kwenye mikoa kama ya Tanga, Kigoma, Tabora, Mwanza na Dar na utashangaa kuna hata wasomi na watu wenye exposure huwa wanashiriki

Miye sijambo pia namshukuru Mola
Bro bila shaka hapa umeongelea USOMI wa usecular sio ?

Bro secular haina uwezo wa kumjulisha mtu kwamba jambo fulani baya na jambo fulani zuri hasa kitabia. Kwahiyo usishangae hata yule aitwae msomi wa ki secular akawa anakula huku anakimbia,akawa hajui hata kuoga janaba,vipi atajua kuhusu ubaya wa hayo mangoma ?

Nakukumbusha tu usecular hauna uwezo wa kumgutusha mtu na kumfanya mtu awe mstaarabu.

Usecular una udhaifu mkubwa sana hasa kimaadili na kitabia.

Nakumbuku nilivyokuwa mdogo haya nilikuwa naya shuhudia mkoani Tabora.
 
wanawekwa maziwa sjui miwa asali wanatenga kabisa katika sinia then wanaweka kwneye chumba kinajulikana kama kilinge yan ndio wametengewa hao mashetani
Hiyo inaitwa chano. Inakua na vitu vitamu kama miwa, asali, ndizi kusukari, halua, mkate wa kumimina na vitu kama juice ambavyo huwekwa kwenye sinia

Wanasema hicho ni chakula cha hao mashetani ambao huja kupitia miili ya binadamu na kuja kula hivo vitu. Katika baadhi ya makabila na koo jambo hili linafanyika kila mwaka na wanapiga na hizo ngoma za kuwaalika hao viumbe

Inasemekana kua hiyo ni aina ya matambiko kama matambiko mengine yanayofanywa kwa aina tofauti kwenye makabila mengi hapa nchini au Afrika kwa ujumla

Kuna wakati Tanga zinapopigwa hizi ngoma huwa wanatembea barabarani mchana kweupe, wanaume wakiwa vifua wazi na wanawake manyonyo nje!

Wanaoshiriki mambo haya wanadai inawafanya wakae vizuri katika maisha yao kwa mwaka mzima. Yaani ni matambiko ya kuondoa mikosi ya kuumwa, kuharibikiwa na mambo ya kazi au biashara, kuvurugikiwa na mahusiano ya kifamilia kama vile ndoa n.k

Jambo la kushangaza kama nilivosema awali ni kwamba hata waliowasomi na wenye exposure kubwa kwenye hizo koo ikiwemo waliowahi kuishi Ulaya na Amerika wanaamini na kushiriki hayo mambo!
 
Hiyo ngoma ya kucheza vifua wazi na maziwa nje kwa wanawake inaitwa kifudu, huchezwa na wadigo hujumuisha matusi s mchezo,nilisahau hilo jina kaka chano, nimeshawah kuta njia panda pia kuna mkate wa kumimina naona ni shirki tu, halaf skua najua majini huja kupitia binadam na kula nilijua wamefungiwa humo ndani wanakula asante kwa kunijuza zaidi
Hiyo inaitwa chano. Inakua na vitu vitamu kama miwa, asali, ndizi kusukari, halua, mkate wa kumimina na vitu kama juice ambavyo huwekwa kwenye sinia

Wanasema hicho ni chakula cha hao mashetani ambao huja kupitia miili ya binadamu na kuja kula hivo vitu. Katika baadhi ya makabila na koo jambo hili linafanyika kila mwaka na wanapiga na hizo ngoma za kuwaalika hao viumbe

Inasemekana kua hiyo ni aina ya matambiko kama matambiko mengine yanayofanywa kwa aina tofauti kwenye makabila mengi hapa nchini au Afrika kwa ujumla

Kuna wakati Tanga zinapopigwa hizi ngoma huwa wanatembea barabarani mchana kweupe, wanaume wakiwa vifua wazi na wanawake manyonyo nje!

Wanaoshiriki mambo haya wanadai inawafanya wakae vizuri katika maisha yao kwa mwaka mzima. Yaani ni matambiko ya kuondoa mikosi ya kuumwa, kuharibikiwa na mambo ya kazi au biashara, kuvurugikiwa na mahusiano ya kifamilia kama vile ndoa n.k

Jambo la kushangaza kama nilivosema awali ni kwamba hata waliowasomi na wenye exposure kubwa kwenye hizo koo ikiwemo waliowahi kuishi Ulaya na Amerika wanaamini na kushiriki hayo mambo!
 
Bro secular haina uwezo wa kumjulisha mtu kwamba jambo fulani baya na jambo fulani zuri hasa kitabia. Kwahiyo usishangae hata yule aitwae msomi wa ki secular akawa anakula huku anakimbia,akawa hajui hata kuoga janaba,vipi atajua kuhusu ubaya wa hayo mangoma ?

Kwa kiasi fulani nakubaliana nawe kua sio ustaarabu wote unaletwa na u secular. Kuna mambo mengi sana yamekwenda kombo kwa kuumbatia huo u secular. Lakini elimu ya ki secular si inapingana moja kwa moja na mambo haya mkuu?

Nakumbuku nilivyokuwa mdogo haya nilikuwa naya shuhudia mkoani Tabora
Tabora ndio kwenyewe sasa mkuu. Kuna baadhi ya maeneo kule kila baada ya nyumba nne au tano kuna "fundi" wa ngoma hizi!

Pia kuna viongozi wakubwa Serikalini akiwemo Marehemu Chifu Abdallah Fundikira, Marehemu Samuel Sitta na wengineo walikua viongozi hasa wa waziwazi na wa kisiri wa mila na matambiko haya ya jadi

Labda kuna siri kubwa zaidi ndani ya mambo haya ambayo wajuzi zaidi watufahamishe na kutuelimisha
 
Mwaka 2012 kuna ngoma zilikuwa zinapigwa kama hizo, akatoka mchungaj mmoja na mtumishi mwingine wa kawaida ambae kwa sasa nae amekuwa mchungaji.

Walisimama mita kama 100 kutoka pale ambapo ngoma ilikuwa inapigwa, waliomba kwa dakika kama 2 ama 3. Hazizidi 3, wakasema wanafunga anga kwa mamlaka ya Jina la Yesu na maneno mengine.

Walipomaliza tu kuomba after one minute palikuwa kimya na wale wapiga ngoma macho yakaelekea maeneo lilipo kanisa, mmoja mmoja washika baiskeli zao wakaondoka.

Haukupita mwezi yule mganga mahali pale akaondoka.

Mkuu, usimruhusu mwanao, wewe au mtu yoyote kwenda hata kushuhudia hizo ngoma.
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana nawe kua sio ustaarabu wote unaletwa na u secular. Kuna mambo mengi sana yamekwenda kombo kwa kuumbatia huo u secular. Lakini elimu ya ki secular si inapingana moja kwa moja na mambo haya mkuu?

Tabora ndio kwenyewe sasa mkuu. Kuna baadhi ya maeneo kule kila baada ya nyumba nne au tano kuna "fundi" wa ngoma hizi!

Pia kuna viongozi wakubwa Serikalini akiwemo Marehemu Chifu Abdallah Fundikira, Marehemu Samuel Sitta na wengineo walikua viongozi hasa wa waziwazi na wa kisiri wa mila na matambiko haya ya jadi

Labda kuna siri kubwa zaidi ndani ya mambo haya ambayo wajuzi zaidi watufahamishe na kutuelimisha
Bro mambo ya kishirikina yote huongozwa na ujinga.

Pili,sijawahi kuona usecular ukioinga juu yamambo haya,labda unionyeshe leo ni wapi usecular unapinga mambo kama haya au mfano wake.
 
Back
Top Bottom