VERSE 3.
Kumbe na maana zao,
Ndio sasa nimeelewa,
Eti rangi nyeusi, Maana yake ni upofu,
Kivipi utakwepa..
kubunywa usipoona,
Kuwa yupo mahututi,
Ndiyo ile rangi ya njano,
Blue ID ya umbumbumbu,
Eti masikini wakati maji anayo,
Napongezwa kwa ukijani,
Baada ya twiga wote kuibwa,
Binti anatia huruma,
Mabrother wake wamemponza,
Amekuwa ombaomba, Na harufu mbaya ya maisha,
Maana kila anayemchukua,
Anamfanya mradi wake,
Binti huyu ni yuleyule,
Ambaye Solo Thang kamuimba.