Mwenzenu nipo addictive na sigara jamani.
It give me pleasures,it helps me the time to think and help me to shut out all distractions in my head.
Haswa wallet ikinuna,akaunti ikiwa haisomi lazima nipulize Embassy Light pakti 2 akili ikae sawa.
Nimeanza kuvuta nipo nimemaliza o level nasubiria kuingia Advance.
Nakumbuka aliyeniingiza ni dada yangu mmoja hivi anakula ile majani miraa akitafuna miraa lazima avute siagara au shisha. Siku nilipoionja ikawa mkombozi nikiwa nataka kusoma kutoboa,nikiwa na mawazo nikiwa sina pesa.
Hapo nitapuliza nitakuwa burudani kabisaa.
Situmii ulevi wowote iwe pombe,bangi,mirungi.
Starehe yangu ni sigara tu japo huwezi kunikuta nikivuta mbele za watu unless ni marafiki zangu wa karibu au na wanafamilia loo hata shem wenu hafahamu hilo.
Sasa basi nataka nijaribu kuiachaila nashindwa nitaanzaje kila nikijaribu nashindwa familia wameniambia nikisikia hamu ya kuvuta ni bora shisha ila mi naona ndo yale yale halafu tabu mamitungi kuanza kuweka moto kutengeneza inachukua mda tofauti na sigara bana.
Saa nyingine kama nikiwa disko naenda kuvuta smoking room huwa naona aibu kweli mdada mie ila ntafanyeje sasa na nisipovuta nakuwa mpole balaaaaaa akili haifanyi kazi wakati nasoma siwezi kusolve kitu au kudiscuss mpaka nikashtue kidogo.
Kama hapa leo tokea saa 7 usiku nalipuliza tu mpaka saa kumi mda wa daku nimeacha kula daku ila kiu haijaisha.
Nahitaji kuacha jamani mnisaidie nahitaji ushauri sihitaji madongo wala matusi.[/QUOTE/]
Humu watu watakushauri weeeeeeeeeeeeee but at the end of the day wewe pekee ndo unaweza kufanya desicion,lakini mimi nisikufiche sigara kama mtu unataka kuquit haihitaji dawa wala ushauri ni siku moja tu unaamka asubuhi unasema sitaki tena sigara then unakuwa umeacha,mf. mimi nimevuta sigara almost 7yrs lakini niliacha siku moja 2 nilipoamua,Heroine nimevuta almost 3yrs na niliacha siku niliyoamua kuacha but before wazee wangu walihangaika kunipeleka rehab,kanisani etc etc sikuweza kuacha mpaka siku kutoka ndani niliposema sitaki tena unga and thats it