Ngoja niropoke

Ha haa unachukua hatua wakati bado upo nae. Mtaishia kukomoana mpeane stress mwishowe muuane. Hiyo ni love au?
Sisi tunapendana sana maana pia tulifanya na kolabo ya kilingeni..
hapa nina ruhusa ya kuongeza msaidizi kiroho safi kabisa...! Kupuliza kidoho muhimu sana ujue
 
Sometimes ni huruma tu na msaada kwakuwa ndoa ina maana kubwa kwa mwanamke kuliko mwanaume
In his late fifties mwanaume anaweza kuoa binti wa under 25 kitu ambacho ni kinyume kabisa kwa wanawake
Ha haa eti huruma. You are not serious.
Anakupelekesha maugomvi kila siku, ni msomi ana pesa zake unamuonea huruma ili iweje?
Hapo wewe ndo unamuhitaji zaidi ya yeye anavyokuhitaji.
Mwanamke yoyote akikuhitaji atanyenyekea...ukiona hakunyenyekei ujue hajali umuache usimuache yeye sawa.
 
Hili ni darasa tosha na mwenye masikio na asikie. Wanawake wapo vizuri pindi wakiwa na hivyo vitu i.e. Elimu, Fedha, Cheo au Madaraka au bado "anauzika" i.e. bado hajachuja. n.k.. Wengi wanasahau kuwa hivyo ni vitu vya mpito tu. Wanajisahau iko siku inakuja watakuwa ni retired officers, watakuwa ni bibi vikongwe na nguvu(Physical strength) imepungua sana. Hapo ndipo ile Asili ya mwanamke kuwa chini ya Mwanaume inarudi kwa nguvu sana lakini by then ni too late. i.e. Mwanamke kwa Asili huhitaji awepo mtu(Me) atakeyempelekea kero zake, shida au hata kumuuliza maswali na kutaka walau kusikia akijibiwa na huyo mwanaume. Kama Mume alikwisha fariki basi mwanamke atakuwa na cha kusema e.g. "Dah, angelikuwapo .......(Me)hili lisingekuwa hivi."
Asante Mshana Jr kwa somo mujarabu sana.
 
Acha niwe mshamba, wakati bado nasaka maisha niliapa kutooa msomi Wala mwanamke mwenye kazi.kwasababu sioi mfanyakazi Bali naoa mtu wa kujenga naye familia

Nilifanikisha lengo langu, sijisifu Hadi leo sijawahi kutamkiwa neno lenye kuniumiza pamoja na kwamba ndoa haikosi changamoto.

Lakini nayoyaona kwenye ndoa za wenzangu, namshukuru sana MUNGU
 
Maneno ya Mungu yanatuasa tuishi nao kwa AKILI! Nazingatia sana hayo maneno
 
Pengine walipokuwa wanasoma waliambiwa maneno kama "Soma sana, tafuta fedha zako ili mwanaume asikusumbue kwa lolote lile" (hii ndo shida kubwa)

Kwahiyo wengi kuanzia hapo wakawa wanatembea na competetive mentality (fikra za kishindani) na muda wote wapo kinyume na jinsia ya kiume.

Kinachotokea, wakiolewa wanafanya mambo kama washindani (competetors) kwa wanaume wao na sio wapambanaji wenza (teammates)

Kitu kingine kinachowaharibu ni hizi FEMINISTS MOVEMENTS (harakazi zinazodaiwa kumpa nguvu mwanamke na kumkomboa kifikra)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…