Ngoja nikwambie sasa, sisi wahuni wa miaka ya 90 na tulivyo sasa

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,507
Unajua nawacheki vijana wa kisasa naona kama wanaigiza uhuni kuliko uhalisia. Sisi tuliishi nyakati za hatari miaka ya 90 halafu bado tumebaki na akili za kusimulia vijana.

Umetoka Ubungo ukapita External, ukapita Garage kituo kinachofuata ni Tabata Relini (Mwananchi)

Ukishuka pale unavuka barabara unaingia kulia unafuata barabara au unaambaa ambaa na reli ile mpaka unaposhuka tena kulia na kupandisha kamlima kadogo ukiacha ile Bar ya Mtaita. (Pale walikuwa pia wanauza Sambusa nzuri sana za Nyama miaka ya 90) ukiendelea mbele utakutana na uliokuwa MJI MPYA.

Ukitembea sana utakuja kutana na Uwanja wa Twiga. Mimi ndo ulikuwa uwanja wangu wa kuangalia mpira jioni, mazoezi au mechi.

Miaka hiyo kuna team ta Twiga iliyokuwa na jersey za utumbo zenye namba kubwa mgongoni 60, 78, 86, 97 n.k

Pale mlangoni ulikuwa unamkuta gollie mmoja mbabe sana anaitwa Omary. Sijui yu wapi huyu bwana. Nataman sana kumwona. Jamaa alikuwa anapendeza sana mlangoni, hasa kwa udakaji wake na alivyokuwa akiwagonga vichwa wachezaji pinzani kwa usiri mkubwa sana.

Kulikuwa na wachezaji wazuri wenye speed mmoja wapo alikuwa Martin Kiberenge. Huyu jamaa alikuwa anakimbia na mpira balaa. Maskini alikuja ishia kuwa mpiga picha tu. But huyu jamaa hakupaswa kucheza soka la Bongo.

Alikuwepo Kiruguru. Huyu alikuwa amekomaa sana na mfupi asiye na woga uwanjani. Kisha unakuja kutana na Mluguru mwingine mrefu ambaye miaka hiyo wenzake wanacheza mpira wamevaa viatu yeye alikuwa anacheza peku na alikuwa anaçhana sana mipira kwa miguu yake.

Alikuwa na nguvu na amekomaa sana. Mechi zilikuwa zinachezwa huku refarii ameweka panga kiunoni maana ilikuwa kipigo nje nje kwa marefa. Kama refa unaonekana umeshindwa kuumudu mchezo basi wananchi wanaonesha wanaweza kukumudu.

Mara nyingi sana kulikuwa kunatokea vipigo vya mawe, mapanga n.k so si ajabu wakati wa kumaliza mpira refa akawa ameenda simama eneo ambalo anajua anaweza chomoka kwa urahisi kukimbia kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.

Wakati huo kundi kubwa la masela lina check mpira huku linavuta bhangi pembeni ya uwanja. Sasa usiwe na kiherehere ukataka uangalie mpira peke yako kwa kusimama na kuwaziba wengine. Utapigwa makonzi mpaka kichwa kibonyee halafu baadaye ndo kivimbe utadhani ndani kimewekwa kokoto pasipo mpangilio maalum.

Maisha mtaani yalikuwa ya ubabe. Demu unampata kwa ubabe na unadumu naye ukiwa mbabe, otherwise watu watakuchukulia tu.

Nakumbuka miaka hiyo ndo kukatokea kutokuelewana katika team ya Twiga ikavunjika na kuwa na Team Mbili. Twiga (Wastaarabu) na Begeju (watoto wa Mbwa) ilikuwa inapigwa game zikikutana team hizi mbili ni hatari na nusu. Na mwishowe si ajabu kutokea kipigo

But kumbuka ni team za hapo hapo na zinatumia uwanja mmoja. Mimi walikuwa mara nyingi wakinishawishi niende nao tunapoenda kucheza mechi mbali,Temeke, Ubungo n.k ili ikitokea tunahitaji kuchapana mkono nami niwape msaaada wangu.

Mimi nlikuwa napenda ugomvi.napenda sana miaka hiyo nmemaliza shule ya Msingi Makubuli/Mabibo then nasoma Tambaza ( wababe wa Dar) so nlikuwa mbabe ila nina akili.

Kulikuwa na wapiga mnanda maarufu miaka hiyo akina Furahisha(alikuja kuwa teja) Fikirini, Ali, Masud na wengine nmewasahau. Bhangi, Mademu na Pombe.

Mimi sasa naonekana mambo safi mtoto wa kidosi ila niliyechangamka.maana nlikuwa naweza kugonga sana ngumi.jamaa wengi kitaa walikuwa wanaishia darasa la saba na wengine hawamalizi hata hilo darasa la saba.

Late 2000 nikiwa mwaka wa 2 UDSM. Mzee aliamua tuhame tuhamie Sinza ambako pia tulikuwa na nyumba na ilikuwa wazazi wanakaa kule sisi na baba mdogo tunaishi huku Tabata Kimanga. Nakumbuka ile picha iliyokuwa na maneno HII NGUNA LAZIMA IISHE LEO,IWE IWEJE!

Miaka ile mitaani ulikuwa huwezi kuta shoga.utampata wapi na vijana tulifunzwa ukakamavu mapema sana? Nilikuwa mhuni sana ambaye leo hii natamani niende fanya visiting yale maeneo niwatafute wana. Zaidi ya miaka 20 sijafika tena huko.

Najitizama najiona nmebadilika sana.nlichange kwa ghafla sana katika maisha na leo hii nmekuwa hivi nilivyo mpole na mwenye aibu sielewi sababu ni nini hasa.
 
Mkuu huo uhuni fresh.....lkn kwa miaka hio hio nikikuletea mambo yaliokua yakitendeka pale Mbeya....haki utabaki mdomoa wazi....

Mbeya town pale nilishudia vijana maeno ya ilemi chini walikua kama nane hivi.....wanapigana kwa visu afu kumbe ni pambano kabisa walishaambiana wakutane wazichape......makundi mawili tofauti........watu watatu walifia pale pale.....!!!

Mzee moja jirani yetu alishushwa kwenye landrover yake kama masihara.....afu watu wakashika uskani wakasepa....kina Nani hao.....Jombi baba
 
Mkuu huo uhuni fresh.....lkn kwa miaka hio hio nikikuletea mambo yaliokua yakitendeka pale Mbeya....haki utabaki mdomoa wazi....

Mbeya town pale nilishudia vijana maeno ya ilemi chini walikua kama nane hivi.....wanapigana kwa visu afu kumbe ni pambano kabisa walishaambiana wakutane wazichape......makundi mawili tofauti........watu watatu walifia pale pale.....!!!

Mzee moja jirani yetu alishushwa kwenye landrover yake kama masihara.....afu watu wakashika uskani wakasepa....kina Nani hao.....Jombi baba
Hebu tupe hicho kisa tuone uhalisia wake.....kama wanatuzidi sisi uhuni....
 
Back
Top Bottom