Ngoja nikapunguze mawazo

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
28
Rais Jakaya Kikwete, aliondoka nchini jana mchana kuelekea Davos, Uswisi kuhudhuria kikao cha kila mwaka kuhusu uchumi (World Economic Forum), kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, jijini Dar es Salaam jana.
Taarifa hiyo ilisema kikao hicho kitakachoanza kesho na kumalizika Januari 30, mwaka huu, kinahudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi, wachumi, viongozi wa mashirika mbalimbali, wanataaluma, viongozi wa dini na wanaharakati mbalimbali duniani.
Mara baada ya kikao cha Davos, Rais Kikwete ataelekea Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria kikao cha kila mwaka cha Wakuu wa Nchi za Afrika, kitakachoanza Januari 31 hadi Februari 2, mwaka huu na kurejea nchini.

CHANZO: NIPASHE
 
Mimi sielewi.

ndo utaelewa sasa jamaa yuko anapaa sasa. safari za mbali yeye hizi za karibu kenya hapa anamtuma shein. Duh jamaa anasafiri ukitafuta rate ya safari zake kwa mwezi ni hatari. Au an wasiwasi hatorudi kwa hiyo anatumia na kuchukua chale mapema nini?
 
Lets be realistic, kikao kinataka rais awepo... na hata angebaki hapa kwani kungekuwa na any difference??

Kumbukeni system inamuangusha kwa kuachia watendaji wabovu wabaki, cha kusikitisha ndio hao wanaopeana vyeo vyote vikubwa,

tumuache JK akapumzike hotelini ulaya
 
Lets be realistic, kikao kinataka rais awepo... na hata angebaki hapa kwani kungekuwa na any difference??

Kumbukeni system inamuangusha kwa kuachia watendaji wabovu wabaki, cha kusikitisha ndio hao wanaopeana vyeo vyote vikubwa,

tumuache JK akapumzike hotelini ulaya

Yeye mwenyewe kateua mabomu sasa atamlaumu nani?? Na pili pesa ya watu aliyotumia kwenye kampeni ndo inamponza na ndiyo maana unaona ameamua akae kimya na ktk uchaguzi ujao hataki kutumia pesa za watu wale ili aweze kuwashughulikia pale ikibidi.
 
Yeye mwenyewe kateua mabomu sasa atamlaumu nani?? Na pili pesa ya watu aliyotumia kwenye kampeni ndo inamponza na ndiyo maana unaona ameamua akae kimya na ktk uchaguzi ujao hataki kutumia pesa za watu wale ili aweze kuwashughulikia pale ikibidi.

De novo was being sarcastic...:D
 
rais jakaya kikwete, aliondoka nchini jana mchana kuelekea davos, uswisi kuhudhuria kikao cha kila mwaka kuhusu uchumi (world economic forum), kwa mujibu wa taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya rais, ikulu, jijini dar es salaam jana.
Taarifa hiyo ilisema kikao hicho kitakachoanza kesho na kumalizika januari 30, mwaka huu, kinahudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi, wachumi, viongozi wa mashirika mbalimbali, wanataaluma, viongozi wa dini na wanaharakati mbalimbali duniani.
Mara baada ya kikao cha davos, rais kikwete ataelekea addis ababa, ethiopia kuhudhuria kikao cha kila mwaka cha wakuu wa nchi za afrika, kitakachoanza januari 31 hadi februari 2, mwaka huu na kurejea nchini.

Chanzo: Nipashe
kapitia libya akiwa njiani kuelekea davos uswisi na kumshukuru ghaddafi kwa msaada waliotoaa wakusaidiaa mafurikooooooo nchiniiii...

Ikulu hii nayo ni habari mbona hamkuisemaaaaaa?????????
 
Mpaka soli za viatu vyake muungwana ziishe, kanyaga twende!


sema hapa viatu vyake havionekani nafikiri soli imeenda upande halafu mbona rais wetu hana chai

01_10_5benff.jpg
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa zamani wa Marekani, Bill Cliton mjini Davos, Uswisi jana ambapo wawili hao wanahudhuria kongamano la kiuchumi la Duniani(Picha na Freddy Maro)
 
Back
Top Bottom