"Nilikutana na bibi mmoja nikamweleza ninavyo mpenda, naye akasema amekubali, mwisho wake akanipa ahadi, niende kwake nikamtembelee.....".
Pengine nime-basheti kidogo "beti", lakini ni wimbo Fulani wa zamani. Zamani zile ukitongoza utategemea kupata moja kati ya majibu haya matatu, 1-unakubaliwa, 2-unakataliwa (unapigwa buti) au 3-Binti aende kwanza akafikirie (hii ilikuwa minjonjo tu, kwani 90% atakupa tu).
Toka mkutano wa "Beijing", mambo yamebadilika, hakuna mambo ya kuzugana kama zama zile za "mabitozi" na "masista-duu".