NGO yadaiwa kutapeli mamilioni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
http://www.ewura.go.tz/
logo.gif
Tafuta:
Jumatatu Novemba 02, 2009 Habari za Bunge

NGO yadaiwa kutapeli mamilioni
Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 30th October 2009 @ 13:10 Imesomwa na watu: 107; Jumla ya maoni: 0


Habari Zaidi:NGO yadaiwa kutapeli mamilioni
Mbunge: Inauma sana
Mjusi wa Tanzania aipatia Ujerumani sh bilioni 3.2
Maveterani wa vita kuu ya dunia kusaidiwa
Mbunge alazwa Dodoma
NGO yadaiwa kutapeli mamilioni
'Ngorongoro haijaondolewa kwenye maajabu 7'
Pinda atoa somo kwa viwanda vya bia
Ruksa kuipata, kuitumia Hati ya Muungano
Tanzania haijachangia mabadiliko ya tabianchi
‘CUF si watakatifu’
Mji, visiwa hatarini kutoweka
Sitta akemea wabunge wasumbufu
Sungusungu marufuku kutoa adhabu
Wanaofanya biashara ya mikanda ya ngono kukiona
Wabunge watatu kuwasilisha hoja binafsi
Sitta awashangaa watanzania
Sitta, Marmo, Chikawe wampongeza Werema
Bunge lamuapisha mrithi wa Mwanyika

Habari zinazosomwa zaidi:Balaa lingine kwa Chenge
Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
Vatican yamvua jimbo Askofu
Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
SHIRIKA lisilo la kiserikali liitwalo, Tanzania Adult Education ( TAADE) linadaiwa kuwatapeli wananchi mamilioni ya fedha.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetangaza bungeni kuwa inalifahamu shirika hilo linalodaiwa kuwa na makao makuu mjini Dodoma, na ina ofisi mkoani Shinyanga.

Bunge limeelezwa kwamba, watendaji wa TAADE walipita katika mikoa, wilaya na vijiji kutoa mafunzo waliyodai kuwa yangewawezesha wahusika kupata ujuzi ili waajiriwe kama walimu waliokosa elimu ya msingi.

Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, amelieleza Bunge kuwa, wananchi waliohitaji kupata mafunzo hayo walitozwa sh 20,000 kila mmoja, taasisi hiyo ikajikusanyia mamilioni ya fedha na kutokomea.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mwantumu Mahiza, amesema bungeni kuwa Serikali inawatambua TAADE na ni kweli shirika hilo imekuwa likiwachangisha fedha walimu wa kujitolea.

Mahiza amewaeleza wabunge kuwa, TAADE ilisajiliwa mwaka 2007 na kwamba, ni Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na utoaji wa elimu ya watu wazima.

“Shirika hilo lilipata usajili kutoka kwa Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali mwaka 2007, namba yake ikiwa ni NGO/1995” amesema Mahiza kubainisha kwamba, alichosema Simbachawene ni kweli.

“Tabia hiyo imezua malalamiko kutoka kwa viongozi wa mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Dodoma. Ili kuondoa kero hiyo, wizara yangu imewagiza TAADE kutoa elimu bila kuchangisha” amesema Mahiza.

Wizara hiyo imewaagiza maofisa elimu ya watu wazima wadhibiti shughuli za taasisi isiyo ya kiserikali ya TAADE katika halmashauri zao. Mahiza pia amesema, wananchi wanapaswa kuwa makini ili wasitapeliwe.
 
Back
Top Bottom