Ngereja kachakachua sheria ya madini

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
867
219
Ngeleja alisema utafiti uliofanywa na kampuni hiyo unaionyesha kuwapo kwa mashapu ya dhahabu yanayoweza kuchimbwa kwa faida na kwamba, imeanza kufanya upembuzi yakinifu na kuajiri kampuni ya MTL Engineering Consultant kufanya tathmini ya athari ya mazingira (TAM).

“Kutokanana sharti la kisheria linalozuia kutolewa kwa leseni ya kuchimba madini ya dhahabu kwa eneo linalozidi kilomita za mraba 10, kampuni hiyo imelazimika kuomba leseni mbili,” alisema.

Waziri Ngeleja alisema upembuzi yakinifu utasaidia kuonyesha idadi ya wananchi watakaoathirika na mradi huo, itabainisha orodha ya watakaotakiwa kulipwa fidia au kuhamishwa na kujengewa makazi mapya.

SOURCE MWANANCHI

MY TAKE: HAPO KWENYE RED sheria imeshazuia kutoa leseni zaidi ya kilometa za mraba 10, sio mwanasheria lakini ni hakika hakuna sababu ya sheria kuvuia kutoa hicho kibali kwa kilometa 10, kisha ikaruhusu waziri kutoa vibali viwili sasa matiki ya hii sheria nini? au wizara inachakachua sheria, na je sheria ina ruhusu hivyo vibali viwili katika eneo moja? au ndio mambo ya 10% hapo yalishatembea
 
Back
Top Bottom