Ngeleja: Nina faraja baada ya kusamehewa na Rais

Nani alivujisha sauti zao kwanza tuanze hapo...ndiyo ujue kuwa mitandao tunayotumia sio salama
 
View attachment 1205792

Dodoma. Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja leo Alhamisi Septemba 12, 2019 amezungumza kwa mara ya kwanza tangu Rais wa Tanzania, John Magufuli alipotangaza kumsamehe pamoja na mwenzake, January Makamba (Bumbuli).

Ngeleja amezungumza bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa muswada wa Sheria Mbalimbali namba 6 wa mwaka 2019, akimshukuru Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwapongeza wabunge waliomuomba msamaha Rais Magufuli.

Ngeleja na Makamba walikuwa wabunge wa kwanza kumuomba radhi Magufuli kufuatia kuhusishwa na sauti zilizosambaa mitandaoni zikizungumzia barua ya makatibu wa zamani wa CCM na pia hali ya chama kudhoofika na kumkejeli kiongozi mkuu huyo wa nchi.
Juzi mbunge wa Mtama, Nape Nnauye naye aliomba msamaha na kuwa mtu wa tatu kati ya wanachama sita wa chama hicho tawala waliohusishwa na sauti hizo.
Akizungumza bungeni Ngeleja amesema, “Kibinadamu wote tunajua msamaha siku zote unaleta faraja. Mimi mwenyewe lakini kwa niaba ya wananchi wa Sengerema nitumie nafasi hii kuelezea faraja niliyonayo kwa kupata huo msamaha. Pia, nakushukuru (Ndugai) kwa namna ambavyo umeliweka.”

Anaposema kwa niaba ya wananchi wa SENGEREMA anamaanisha kwamba Rais alitukanwa na wananchi wote wa SENGEREMA??.
Mbona anawadhalilisha sana wasengerema wenzie huyu jamaa!!!.
Ajiandae kuachia jimbo tuu basi, msamaha mwisho kwa Rais.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wakulima wa korosho wamedhulumiwa zaidi ya shilling bilioni 400. Msimu wa kununua pamba nchini katika mikoa inayolima pamba umeanza. Serikali haina pesa hivyo walanguzi wanawalalia wakulima wa pamba hivyo kuuza kwa hasara, lakini habari kubwa nchini ni kuhusu kuombwa msamaha kwa mfalme nduli.
😳😳😳😳😳

Sifa kubwa ya kuwa mwana ccm ni unafiki.
 
UPUUZI MTUPU! Na UNAFIKI ULIOKITHIRI.

Back
Top Bottom