Ngeleja: Nina faraja baada ya kusamehewa na Rais

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
ngeleja+pic.jpg

Dodoma. Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja leo Alhamisi Septemba 12, 2019 amezungumza kwa mara ya kwanza tangu Rais wa Tanzania, John Magufuli alipotangaza kumsamehe pamoja na mwenzake, January Makamba (Bumbuli).

Ngeleja amezungumza bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa muswada wa Sheria Mbalimbali namba 6 wa mwaka 2019, akimshukuru Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwapongeza wabunge waliomuomba msamaha Rais Magufuli.

Ngeleja na Makamba walikuwa wabunge wa kwanza kumuomba radhi Magufuli kufuatia kuhusishwa na sauti zilizosambaa mitandaoni zikizungumzia barua ya makatibu wa zamani wa CCM na pia hali ya chama kudhoofika na kumkejeli kiongozi mkuu huyo wa nchi.
Juzi mbunge wa Mtama, Nape Nnauye naye aliomba msamaha na kuwa mtu wa tatu kati ya wanachama sita wa chama hicho tawala waliohusishwa na sauti hizo.
Akizungumza bungeni Ngeleja amesema, “Kibinadamu wote tunajua msamaha siku zote unaleta faraja. Mimi mwenyewe lakini kwa niaba ya wananchi wa Sengerema nitumie nafasi hii kuelezea faraja niliyonayo kwa kupata huo msamaha. Pia, nakushukuru (Ndugai) kwa namna ambavyo umeliweka.”

Kwa taifa letu Rais ni mkubwa mnooo!!! Na mkuu kwa kauli zake,anaonekana alikuwa na bifu hatareee!! Hongera Mh.Kwa kujifanya mjinga siku ipite.
Huu mgogoro wangekuwa chadrma saa hizi wangekuwa wanagawana fito
 
Ni Mungu wao hivyo lazma afurahi
Hapo hata ukimwambia amtukane Mungu aliye hai yupo Radhi amfurahishe Mungu wao
Ndo sababu Mimi yangu awali niliamua kutafuta maisha yangu nje ya siasa. Ukiwa ndani ya siasa sharti use mnafiki ka kudhalilika kama hawa jamaa.
 
Nasubiri azimio la kumpongeza Rais kwa moyo wa huruma na kusamehe!!

Tuna wanasiasa wa ajabu. Eti kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Sengerema - kwani walimtuma asema aliyosema?? Unafiki ni jambo baya sana!!
 
View attachment 1205792

Dodoma. Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja leo Alhamisi Septemba 12, 2019 amezungumza kwa mara ya kwanza tangu Rais wa Tanzania, John Magufuli alipotangaza kumsamehe pamoja na mwenzake, January Makamba (Bumbuli).

Ngeleja amezungumza bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa muswada wa Sheria Mbalimbali namba 6 wa mwaka 2019, akimshukuru Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwapongeza wabunge waliomuomba msamaha Rais Magufuli.

Ngeleja na Makamba walikuwa wabunge wa kwanza kumuomba radhi Magufuli kufuatia kuhusishwa na sauti zilizosambaa mitandaoni zikizungumzia barua ya makatibu wa zamani wa CCM na pia hali ya chama kudhoofika na kumkejeli kiongozi mkuu huyo wa nchi.
Juzi mbunge wa Mtama, Nape Nnauye naye aliomba msamaha na kuwa mtu wa tatu kati ya wanachama sita wa chama hicho tawala waliohusishwa na sauti hizo.
Akizungumza bungeni Ngeleja amesema, “Kibinadamu wote tunajua msamaha siku zote unaleta faraja. Mimi mwenyewe lakini kwa niaba ya wananchi wa Sengerema nitumie nafasi hii kuelezea faraja niliyonayo kwa kupata huo msamaha. Pia, nakushukuru (Ndugai) kwa namna ambavyo umeliweka.”

Lakini kwanini ulimtukana mzee wa watu alikukosea nini? Tunaiomba CCM isikupitishe kugombea Ubunge 2020
 
Yaani jamaa wana what we call “GUTS” kumuita Rais wa nchi mshamba, Mzee kachanganganyikiwa!! Kwenye Audio mr Musiba jamaa alimpa mwenza wake billioni kadhaa na kuzipeleka Kenya kuzificha wakati alipokuwa waziri wa madini, Je dollar zimerudishwaa nyumbani bongo? Au Musiba alisema uongo?
 
Back
Top Bottom