JacksonMichael
JF-Expert Member
- Mar 22, 2012
- 339
- 61
Haya wadau upande mwingine wa shilingi!
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amemtaka Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), asitumie kigezo cha kukatikakatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam kunakosababishwa na hitilafu za kiufundi, kuwapotosha wananchi.
Amesema huo ni unafiki na kuwataka wananchi wampuuze Mbunge huyo kwa sababu utekelezaji wa miradi ya umeme unafahamika na tayari mipango hiyo imezaa matunda kwa kuwepo kwa umeme wa ziada nchini.
Ngeleja ametoa kauli hiyo ofisini kwake Mtaa wa Samora, Dar es Salaam leo ambako pamoja na mambo mengine, amezungumzia kauli aliyoitoa Mnyika jana akisema umefika wakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kimuundo na kiuongozi katika Wizara hiyo kwa kushindwa kuhimili mahitaji ya sasa.
"Nashangazwa na ukimya wa Serikali kuhusu utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na maendeleo ya sekta ya nishati ambayo hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi," Mnyika alikaririwa akisema juzi.
Lakini Waziri Ngeleja alimshangaa Mbunge huyo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kutokuwa na taarifa ya utekelezaji wa mpango huo wakati ilitolewa bungeni na amekuwa akishiriki vikao vya Kamati yake hiyo.
"Si kweli kuwa tumeshindwa kuhimili mahitaji ya sasa, nakubali zipo changamoto, lakini Serikali imechukua hatua kadhaa tangu ulipotolewa Mpango wa dharura bungeni Agosti mwaka jana. Namshangaa Mheshimiwa Mnyika kwa sababu ni mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, anayajua haya. Huu ni unafiki mkubwa na wananchi wanapaswa kumpuuza," amesema Ngeleja.
Akizungumzia sekta ya madini, amesema mafanikio ni pamoja na kutungwa kwa Sera ya Madini (2009) na Sheria ya Madini (2010) ambavyo zimeimarisha usimamizi wa sekta hiyo; kutokana na sheria hiyo sasa Serikali inamiliki hisa katika migodi ya uchimbaji ikiwamo Buckreef Serikali ina hisa asilimia 45 kupitia Stamico; Mchuchuma na Liganga ina hisa asilimia 20 kupitia NDC na Ngaka ina hisa asilimia 30 pia kupitia NDC.
Amesema pia migodi mikubwa inatakiwa kujisajili katika masoko ya hisa na kwa kuanzia, tayari Kampuni ya Barrick imeshaanza kusajili hisa zake, wakati huo huo Mgodi wa Dhahabu wa Geita, Resolute, Tulawaka na TanzaniteOne, imeshalipa kodi ya mapato serikalini ya asilimia 30.
Kuhusu madini ya urani, ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wanaendelea na mchakato wa kupata kibali kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa mujibu wa Itifaki ya Kimataifa na itaendelea kutoa taarifa kwa kadri mchakato unavyoendelea.
HabariLeo