Ngeleja: Mnyika mnafiki, anapotosha wananchi

MNYIKA "Nashangazwa na ukimya wa Serikali kuhusu utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na maendeleo ya sekta ya nishati ambayo hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi," Mnyika alikaririwa akisema juzi.

NGELEJA "Si kweli kuwa tumeshindwa kuhimili mahitaji ya sasa, nakubali zipo changamoto, lakini Serikali imechukua hatua kadhaa tangu ulipotolewa Mpango wa dharura bungeni Agosti mwaka jana. Namshangaa Mheshimiwa Mnyika kwa sababu ni mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, anayajua haya. Huu ni unafiki mkubwa na wananchi wanapaswa kumpuuza," amesema Ngeleja.
Ngeleja acha porojo, hatua kadhaa ni kitu gani hicho? Acha blah blah njoo na takwimu hapo tutakuelewa lakini kiukweli kati yako na Mnyika wewe ndiye mnafiki maana unapinga kauli yake pasipo kuwa na takwimu zozote.. mipango ya kwenye makaratasi tumeizoea usifikiri watanzania ni wale wale..
 
........Amesema huo ni unafiki na kuwataka wananchi wampuuze Mbunge huyo kwa sababu utekelezaji wa miradi ya umeme unafahamika na tayari mipango hiyo imezaa matunda kwa kuwepo kwa umeme wa ziada nchini.

Umeme wa ziaada?????? !!!!!!!
Mhh kweli kuna vogozi wa kitaifa wanadhani tanzania ni dar tu. Kuna mikoa haina umeme wa grid ya taifa aafu ngeleja anaongeleaa umeme wa zaida. Hata Dar yenyewe bado umeme unakatia katika. ........

Inachekesha. kaa si kukera. Kumbe tayari Tanzania tuna umeme wa ziada....
 
Kati vinavyokera ni taarifa zinazotolewa na akina Ngeleja kuwa, hakuna mgawo wa umeme wakati wananchi tuna taabika. Wanashindwa kukiri uwepo wa tatizo la umeme. Sisi ndiyo tuko mitaani na tunaona jinsi maeneo ya Mwenge, K/koo, Posta, na hata yale ya majumbani yanavyokosa umeme kati ya masaa 4-7.

Najiuliza hii Moral Authority ya kusema Mnyika ni mnafiki anaitoa wapi? Kwa nini Ngeleja asionekane kuwa mnafiki zaidi kwa kuuleza umma kuwa hakuna mgawo wa umeme wakati mtaani tunatabika na mgawo?
 
Mkuu mnafiki sio tusi, ni mtu anayezungumza asiyotarenda au asiyoyaamini, na ni kweli tumeyaona sana kwa baadhi ya wanasiasa wetu hasa wa upinzani. Mnyika anataka kutumia hali kukatika kwa umeme kama chance ya kurejesha imani aliyoipoteza pale UBUNGO.

Umenifurahisha sana mjumbe, kama ndiyo tafsiri ya unafiki hiyo basi hakuna aliyenusurika. Maisha bora kwa kila matnzania wakati bei za vitu zinapanda kila kukicha, kuvua magamba na walengwa wakiwa mapacha watatu 'RACHEL' wakati jamaa wametuna hawatikisiki, kamati kuu ya CCM kuitaka Serikali ihakikishe bei ya mafuta ya taa inashuka huku bidhaa hiyo ikiendelea kupanda kila wakati, kuanzisha TAKUKURU kupambana na kuzuia rushwa huku ikiendelea kuota mizizi hasa kwa Chama tawala katika kura za maoni. Kwa kweli kwa ufafanuzi wako kila mtanzania ni mnafiki.
 
Ngeleja ni hayawani,kwanini hawaelezi wananchi kwa nini Aggreko imezima baadhi ya Generator na IPTL wanazima mda si mrefu
 
Mambo mengine mjue yanatia hasira,hv huyu ngeleja anadhani hatuna akili? Pumb.af sana huyu bwana.ila ipo siku nyie ngojeni.
 
Kuwaaacha watu kama ngeleja wanaita watu wanafiki ni upuuzi!!!

Ngeleja ni Mpuuzi mkubwa
 
Mgao hautaisha mpaka uwekezaji wa maana utakapofanywa katika sekta hii. Tunahitaji mitaji mikubwa kwa ajili ya uzalishaji umeme kwani vyanzo tunavyo vingi. Tatizo mafisadi wanatumia upungufu uliopo wa nishati hii kujinufaisha. Mkaa wa mawe na mradi kama wa Steigler's Gorge inaweza kutupatia nafuu iwapo itafikiriwa kwa makini. Bila hivyo tutitana wanafiki mpaka kiama.
 
Wanafiki ni watu wajanja sana, hawapendi kuitwa wanafiki na mara nyingi hawajibu hoja bali kwa tuhuma nzito ili kuchanganganya akili za watu.

Kati ya Mnyika na Ngeleja mnafikia anajulikana.

Ndiyo maana hata January Makamba alisema ni heri kutokuwa waziri kuliko kuwa waziri usiyeaminik katika mdahalo dhidi na Zitto. Makamba aliliona hilo la unafiki wa Ngeleja ndiyo maana akamtupia dongo.

Kama siyi mnafiki mbona hakumjibu Makamba?

Halafu nasikia ngeleja kila baada ya dk 5 huwa anaingia jf kuona hali ya upepo maana siku hizi ukizubaa waweza kuta mkwre keshabadili baraza la mawaziri
 
Mkuu mnafiki sio tusi, ni mtu anayezungumza asiyotarenda au asiyoyaamini, na ni kweli tumeyaona sana kwa baadhi ya wanasiasa wetu hasa wa upinzani. Mnyika anataka kutumia hali kukatika kwa umeme kama chance ya kurejesha imani aliyoipoteza pale UBUNGO.

JacksonMichael,

Asante kwa maoni yako:

Mosi, unaweza kuingia hapa ukasoma kwanza kauli yangu niliyotoa ambayo Waziri Ngeleja ameijibu alivyojibu ndio unaweza kuhitimisha iwapo amejibu hoja au amezusha vioja:JOHN MNYIKA: Mnyika: Mpango wa Dharura wa Umeme. Katika kauli hiyo nimeeleza bayana tofauti ya katizo na mgawo na kueleza wazi namna utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme unavyosuasua, na sikutoa maelezo ya ujumla, bali yenye vielelezo. Nilitarajia Waziri wa Nishati na Madini naye atoe majibu ya kina kwa umma.

Pili, kuhusu imani ya wananchi, maelezo yako yanaonyesha kuwa wewe sio mkazi wa Ubungo. Imani ya wananchi wanaweza kuizungumza wananchi wenyewe, hata hivyo unaweza kuona baadhi ya picha za mikutano yangu ya wananchi ya karibuni jimboni Ubungo: JOHN MNYIKA: Mkutano wa hadhara wa Kimara Mwisho 25/03/2012 Huu ni mkutano wa jumapili iliyopita, katika mkutano huo niliwauliza wananchi wapige kura ya wazi ya imani au kutokuwa na imani, na wananchi unaona waona walinyoosha mikono ya kuwa na imani. Nikawaulizia pia iwapo wana imani waonyeshe kwa vitendo kwa kuchangia fedha kwa ajili ya kesi ya kulinda ushindi wao kwa kuwa wao ndio walionichagua, papo hapo kwa michango midogo midogo walichanga 185,000. Na mwisho wa mkutano wakanikanisindikiza kwa maandamano mpaka kwenye vijiwe vya kahawa, na baada ya kumaliza mazungumzo na Wazee, vijana wakaamua kusukuma gari.

Tuendelee kushirikiana; Maslahi ya Umma Kwanza

JJ
 
We Mnyika, yaani hako kamkutano kako ka hadhara ndiyo kanakupa imani kuwa bado unapendwa. Pole sana!
 
Utamadun wa kuzungumza kwa ushahid ni mzuri xana,
wasaidiz weng wa jk hawana mambo ya TAKWIM
JacksonMichael,

Asante kwa maoni yako:

Mosi, unaweza kuingia hapa ukasoma kwanza kauli yangu niliyotoa ambayo Waziri Ngeleja ameijibu alivyojibu ndio unaweza kuhitimisha iwapo amejibu hoja au amezusha vioja:JOHN MNYIKA: Mnyika: Mpango wa Dharura wa Umeme. Katika kauli hiyo nimeeleza bayana tofauti ya katizo na mgawo na kueleza wazi namna utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme unavyosuasua, na sikutoa maelezo ya ujumla, bali yenye vielelezo. Nilitarajia Waziri wa Nishati na Madini naye atoe majibu ya kina kwa umma.

Pili, kuhusu imani ya wananchi, maelezo yako yanaonyesha kuwa wewe sio mkazi wa Ubungo. Imani ya wananchi wanaweza kuizungumza wananchi wenyewe, hata hivyo unaweza kuona baadhi ya picha za mikutano yangu ya wananchi ya karibuni jimboni Ubungo: JOHN MNYIKA: Mkutano wa hadhara wa Kimara Mwisho 25/03/2012 Huu ni mkutano wa jumapili iliyopita, katika mkutano huo niliwauliza wananchi wapige kura ya wazi ya imani au kutokuwa na imani, na wananchi unaona waona walinyoosha mikono ya kuwa na imani. Nikawaulizia pia iwapo wana imani waonyeshe kwa vitendo kwa kuchangia fedha kwa ajili ya kesi ya kulinda ushindi wao kwa kuwa wao ndio walionichagua, papo hapo kwa michango midogo midogo walichanga 185,000. Na mwisho wa mkutano wakanikanisindikiza kwa maandamano mpaka kwenye vijiwe vya kahawa, na baada ya kumaliza mazungumzo na Wazee, vijana wakaamua kusukuma gari.

Tuendelee kushirikiana; Maslahi ya Umma Kwanza

JJ
 
Jan 2012: Sitagombea Urais 2015, baadaye Nautaka Urais 2015

Kabla ya hapo: Sitagombea Ubunge 2010, hatimaye Naombeni kura niwe mbunge kwa miaka 5 ya mwisho.

Sasa, Sitagombea Uongozi CHADEMA; natabiri 2013- Nimeombwa na wanachama, nagombea. (Atakuwa amesahu kuwa alisema uongozi sio suala la kuombwa ni KUUTAKA).

Sasa, timu iliyopo inatosha kuongoza chama, Mbowe amejenga chama; natabiri 2013- Mbowe na Slaa wamekaa sana, wamechoka, CHADEMA inahitaji timu ya viongozi vijana.

Sitaki, Nataka ya Zitto Kigeugeu. Kwa nini yote haya wakati huu wa uchaguzi wa Arumeru Mashariki?
 
Nadhani kuna tatizo ama kuna kusudi. Hapa ni Zitto anayekuza ama ni sisi? Alizungumzia umri wa Urais; akasema chama ndiye mwamuzi wa kama agombee nafasi yoyote ama la; na kwamba yeye akiombwa na chama chake atakubali nafasi yoyote hata urais na kwamba hana mpango wa kugombea nafasi yoyote nje ya Chadema: Sasa sisi tunasema alisema anautaka urais na kuonyesha kwamba anautaka kwa vyovyote iwavyo tea kwa kuwazuia wengine wasiutake: Akafafanua, kuwa si kweli kwamba anautaka kwa lazima, tunasema kageuka kwamba hautaki: Sasa hapa ni sisi ama yeye?

Zitto kama binadamu yeoyote, ana mapungufu yake, tena mengine yanatukera sote, kama ambavyo na sisi tuna mapungufu ambayo baadhi yanamkera hata na yeye na wengine, lakini katika hili, tusimhukumu vibaya. Ukiwa mfanya biashara wa nguo makini, utatamani ifike siku uwe na kiwanda cha nguo; kadhalika hakuna mwanasiasa makini asiyetamani kuwa kiongozi wa juu, vinginevyo si mwanasiasa mwenye malengo: sote kila mtu anatamani katika fani yake apande juu ya alipo kwa mafanikio, na hivyo si ajabu kwa wanasiasa kutaka nafasi ya urais.

Tatizo ni jinsi gani ya kufika huko na hapo ndipo tunatakiwa tujadili na kwa HAKI na wengine wanambeza Zitto, wanashabikia wanasiasa wezi na mafisadi kupanda ngazi kutaka uongozi wa juu. Tujadili kwa Maslahi ya Tanzania si yetu binafsi.

Kama Zitto ana mapungufu, tuyajadili kwa ushahidi si kujadili anataka ama hataki. Kutaka ama kutotaka si HOJA, Hoja ni kwa njia gani? Na si yeye tu, na si urais tu, hata udiwani, ubunge na kadhalika maana 2013 tutaona madaraja ya 2015 yatakavyojengwa kwa matofali ya rushwa ndani ya CCM kama ilivyoonekana Arumeru na watu bila aibu wanashangilia wakiwamo waliokua wakimpinga huyu mgombea wa CCM wa sasa Siyoi kwa kigezo kwamba ametoa rushwa na si raia.

Leo hii hata RC na Katibu wa CCM na wenzake wanaenda Arumeru kuwalaghai wapiga kura wamchague mtu aliyetoa rushwa na hata wapinzani hilo la rushwa halisemwi tena hata JF limezimika hata magazeti yamesahau kabisaaaaaa!! Na Takukuru wameshawasahau waliowakamata!!! Hapa ndio tujadili, rushwa inahalalishwaje?

Na hiyo ndio safari imeanza ya 2015 rushwa mbele kwa mbele.
 
hakuna wa kumuamini katika hili si huyo ngeleja,serikali wala tanesco,mara hakuna mgao wa umeme, mara kuna umeme wa ziada lakini mbona umeme wenyewe bado unakatwa kwa masaa kadhaa ina maana ngeleja halijui hili au anadanganywa kama si na yeye kuwahadaa watz,awe mkweli tu watz watamuelewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom