Ngeleja: Mnyika mnafiki, anapotosha wananchi

JacksonMichael

JF-Expert Member
Mar 22, 2012
339
61
Haya wadau upande mwingine wa shilingi!

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amemtaka Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), asitumie kigezo cha kukatikakatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam kunakosababishwa na hitilafu za kiufundi, kuwapotosha wananchi.

Amesema huo ni unafiki na kuwataka wananchi wampuuze Mbunge huyo kwa sababu utekelezaji wa miradi ya umeme unafahamika na tayari mipango hiyo imezaa matunda kwa kuwepo kwa umeme wa ziada nchini.

Ngeleja ametoa kauli hiyo ofisini kwake Mtaa wa Samora, Dar es Salaam leo ambako pamoja na mambo mengine, amezungumzia kauli aliyoitoa Mnyika jana akisema umefika wakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kimuundo na kiuongozi katika Wizara hiyo kwa kushindwa kuhimili mahitaji ya sasa.

"Nashangazwa na ukimya wa Serikali kuhusu utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na maendeleo ya sekta ya nishati ambayo hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi," Mnyika alikaririwa akisema juzi.

Lakini Waziri Ngeleja alimshangaa Mbunge huyo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kutokuwa na taarifa ya utekelezaji wa mpango huo wakati ilitolewa bungeni na amekuwa akishiriki vikao vya Kamati yake hiyo.

"Si kweli kuwa tumeshindwa kuhimili mahitaji ya sasa, nakubali zipo changamoto, lakini Serikali imechukua hatua kadhaa tangu ulipotolewa Mpango wa dharura bungeni Agosti mwaka jana. Namshangaa Mheshimiwa Mnyika kwa sababu ni mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, anayajua haya. Huu ni unafiki mkubwa na wananchi wanapaswa kumpuuza," amesema Ngeleja.

Akizungumzia sekta ya madini, amesema mafanikio ni pamoja na kutungwa kwa Sera ya Madini (2009) na Sheria ya Madini (2010) ambavyo zimeimarisha usimamizi wa sekta hiyo; kutokana na sheria hiyo sasa Serikali inamiliki hisa katika migodi ya uchimbaji ikiwamo Buckreef Serikali ina hisa asilimia 45 kupitia Stamico; Mchuchuma na Liganga ina hisa asilimia 20 kupitia NDC na Ngaka ina hisa asilimia 30 pia kupitia NDC.

Amesema pia migodi mikubwa inatakiwa kujisajili katika masoko ya hisa na kwa kuanzia, tayari Kampuni ya Barrick imeshaanza kusajili hisa zake, wakati huo huo Mgodi wa Dhahabu wa Geita, Resolute, Tulawaka na TanzaniteOne, imeshalipa kodi ya mapato serikalini ya asilimia 30.

Kuhusu madini ya urani, ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wanaendelea na mchakato wa kupata kibali kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa mujibu wa Itifaki ya Kimataifa na itaendelea kutoa taarifa kwa kadri mchakato unavyoendelea.

HabariLeo
 
Naona sera za CCM siku hizi ni matusi tu na kuita watu wanafiki. Wameshindwa kujibu hoja.
 
Umeme umekatika sasa hivi! Na haukuwapo toka jana! Umewaka nusu saa tu! Shkamoo ngeleja!
 
Naona sera za CCM siku hizi ni matusi tu na kuita watu wanafiki. Wameshindwa kujibu hoja.

Mkuu mnafiki sio tusi, ni mtu anayezungumza asiyotarenda au asiyoyaamini, na ni kweli tumeyaona sana kwa baadhi ya wanasiasa wetu hasa wa upinzani. Mnyika anataka kutumia hali kukatika kwa umeme kama chance ya kurejesha imani aliyoipoteza pale UBUNGO.
 
The only magamba leader you can trust is a dead magamba leader!
 
Hapa umeme ushakata, whether ni mgao au hapana kwa kweli hatuwaelewi. Mimi mwananchi wa kawaida nimepigika sana angalau nataka nikirudi ghetto niwashe feni ya mezani na hiyo inakuwa shida.
 
Mkuu mnafiki sio tusi, ni mtu anayezungumza asiyotarenda au asiyoyaamini, na ni kweli tumeyaona sana kwa baadhi ya wanasiasa wetu hasa wa upinzani. Mnyika anataka kutumia hali kukatika kwa umeme kama chance ya kurejesha imani aliyoipoteza pale UBUNGO.

Labda kapoteza imani kwenye Ubungo ya kijijini kwenu,lakini si jimbo la Ubungo D.s.m ambalo wakazi wake wengi na wanaojielewa!
 
Wanafiki ni watu wajanja sana, hawapendi kuitwa wanafiki na mara nyingi hawajibu hoja bali kwa tuhuma nzito ili kuchanganganya akili za watu.

Kati ya Mnyika na Ngeleja mnafikia anajulikana.

Ndiyo maana hata January Makamba alisema ni heri kutokuwa waziri kuliko kuwa waziri usiyeaminik katika mdahalo dhidi na Zitto. Makamba aliliona hilo la unafiki wa Ngeleja ndiyo maana akamtupia dongo.

Kama siyi mnafiki mbona hakumjibu Makamba?
 
Nani wa kupuuzwa sasa, enyi watawala hebu tupeni ukweli nini kinaendelea hizi contradiction zenu hamuoni kuwa sisi wananchi mnatuchanganya?
 
Wanasiasa bana! hivi Ngeleja bado anahisi kwamba wananchi wanamsikiliza?!
 
Huyu ngeleja anakorogwa kweli. Ina maana hizo hitilafu za umeme huwa zinatokea kila baada ya dk 15!!? Kuanzia asubuhi mpaka jioni umeme haupo. Jioni hii umeme umerudishwa,lakini umeshakatwa zaidi ya mara 3 au kwa vile una standby generetor! Shame on you william kama sio maliamu.
 
Haya wadau upande mwingine wa shilingi!

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amemtaka Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), asitumie kigezo cha kukatikakatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam kunakosababishwa na hitilafu za kiufundi, kuwapotosha wananchi.

Amesema huo ni unafiki na kuwataka wananchi wampuuze Mbunge huyo kwa sababu utekelezaji wa miradi ya umeme unafahamika na tayari mipango hiyo imezaa matunda kwa kuwepo kwa umeme wa ziada nchini.

Ngeleja ametoa kauli hiyo ofisini kwake Mtaa wa Samora, Dar es Salaam leo ambako pamoja na mambo mengine, amezungumzia kauli aliyoitoa Mnyika jana akisema umefika wakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kimuundo na kiuongozi katika Wizara hiyo kwa kushindwa kuhimili mahitaji ya sasa.

“Nashangazwa na ukimya wa Serikali kuhusu utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na maendeleo ya sekta ya nishati ambayo hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi,” Mnyika alikaririwa akisema juzi.

Lakini Waziri Ngeleja alimshangaa Mbunge huyo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kutokuwa na taarifa ya utekelezaji wa mpango huo wakati ilitolewa bungeni na amekuwa akishiriki vikao vya Kamati yake hiyo.

“Si kweli kuwa tumeshindwa kuhimili mahitaji ya sasa, nakubali zipo changamoto, lakini Serikali imechukua hatua kadhaa tangu ulipotolewa Mpango wa dharura bungeni Agosti mwaka jana. Namshangaa Mheshimiwa Mnyika kwa sababu ni mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, anayajua haya. Huu ni unafiki mkubwa na wananchi wanapaswa kumpuuza,” amesema Ngeleja.

Akizungumzia sekta ya madini, amesema mafanikio ni pamoja na kutungwa kwa Sera ya Madini (2009) na Sheria ya Madini (2010) ambavyo zimeimarisha usimamizi wa sekta hiyo; kutokana na sheria hiyo sasa Serikali inamiliki hisa katika migodi ya uchimbaji ikiwamo Buckreef Serikali ina hisa asilimia 45 kupitia Stamico; Mchuchuma na Liganga ina hisa asilimia 20 kupitia NDC na Ngaka ina hisa asilimia 30 pia kupitia NDC.

Amesema pia migodi mikubwa inatakiwa kujisajili katika masoko ya hisa na kwa kuanzia, tayari Kampuni ya Barrick imeshaanza kusajili hisa zake, wakati huo huo Mgodi wa Dhahabu wa Geita, Resolute, Tulawaka na TanzaniteOne, imeshalipa kodi ya mapato serikalini ya asilimia 30.

Kuhusu madini ya urani, ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wanaendelea na mchakato wa kupata kibali kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa mujibu wa Itifaki ya Kimataifa na itaendelea kutoa taarifa kwa kadri mchakato unavyoendelea.

HabariLeo | Ngeleja- Mnyika mnafiki, anapotosha wananchi

Nyie Waandishi, tumeshawaomba muache kuandika taarabu, tumechoshwa na habari za kishenzi kila siku na si habari za kuleta maendeleo. Sasa hii ni maana gani ya kutuletea malumbano ya Ngeleja na Mnyika hapa?? Hapa ni JF hatutaki umbeaumbea na habari ndefuuuuuu lakini ukimaliza kuisoma inaishia hapohapo. Porojo tupu Tanzania. Mnatuchosha hembu badilikeni na wapuuzeni hao, wakiona hawaandikwi wataacha wenyewe kuropoka na kuanza kufanya kazi.
 
Umeme unaozalishwa kwa sasa ni zaidi ya 1200 MW mahitaji ni 850 MW, tuna ziada ya umeme kwa sasa.

Hongera JMK.
 
Umeme unaozalishwa kwa sasa ni zaidi ya 1200 MW mahitaji ni 850 MW, tuna ziada ya umeme kwa sasa.

Hongera JMK.

Sasa mkuu huwo umeme wa 1200 MW upo wapi? Mbona kila siku mitaani tunasikia miungurumo ya jenereta tu?
 
Mimi ni mkazi
Ilala umeme una
katika saa 2 asubui
mpaka 12 jioni
huu si mgao? Tuache
unafki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom