Ngeleja kwa kujiamini uso kwa uso na wabunge dodoma.

COMPLICATOR2011

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
253
35
"Ndugu zangu Watanzania baada ya kuwashuhudia kwa wiki kadhaa mawaziri wakiwasilisha bajeti zao na kukumbwa na changamoto nyingi kutoka kwa wabunge hasa wale wa upinzani, ijumaa hii ni zamu ya Ngeleja, anawasilisha bajeti kwa wabunge huku wengi wao wakiwa tayari wameapa kumtoa jasho bila kujali itikadi za vyama vyao. Macho na masikio yote ni kwa NGELEJAAAA!
 
Kwa nini wamempatia Ijumaa au akimaliza kusoma ndani ya Weekend aweze kusikilizia wabunge wanasemaje na awapoze vipi kabla ya Jumatatu?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tofauti na wizara nyingine yeye amepewa siku mbili tena ijumaa-jumatatu nasikia kuna waheshimiwa kashawapoza ili wampigie makofi mpaka wawachanganganye wenzao, dogo anampunga usiulize kabisa. Najua bajeti itapita sbb ya magamba kuwa mengi mjengoni lkn lazima atachubuka.
 
Hivi kuna bajeti (ya Wizara yoyote) ilishawahi kukataliwa/kutopitishwa na wa-Bunge?

Huna haja ya kusikiliza hotuba ya bajeti ya Wizara yoyote ile (By the way UMEME hautakuwepo sehemu kubwa ya nchi) kwa maana ni kama kutizama filamu za Steven Seagal!
 
Tofauti na wizara nyingine yeye amepewa siku mbili tena ijumaa-jumatatu nasikia kuna waheshimiwa kashawapoza ili wampigie makofi mpaka wawachanganganye wenzao, dogo anampunga usiulize kabisa. Najua bajeti itapita sbb ya magamba kuwa mengi mjengoni lkn lazima atachubuka.
 
Wabunge wa ccm ni wengi sana kwa hiyo hata kama wakikosoa baadae huishia kuunga mkono hoja.
 
Wabunge wa ccm ni wengi sana kwa hiyo hata kama wakikosoa baadae huishia kuunga mkono hoja.
Ndiyo watamtoa jasho. "Waziri ni mzembe, wizara imejaa mafisadi, mikataba mobovu, maji Mtera ni kisingizio, blah, blah, blah, ............................................................................ lakini Mheshimiwa Spika mimi naunga mkono hoja mia kwa mia!!!!!! ". Ngeleja jasho linamtoka.
 
Back
Top Bottom