Ngeleja azima hoja ya Escrow

Ngeleja azima hoja ya Escrow

KIJANI

Senior Member
Joined
Dec 13, 2010
Posts
138
Reaction score
26
Mbunge wa Sengerema, Mkoani Mwanza, Bw. William Ngeleja, amesema wapinzani wake kisiasa wanapoteza muda wao wanapotoa hoja dhaifu kwa wananchi wa jimbo hilo juu ya kuhusika kwake kwenye sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow na kuzungumzia tatizo la maji.

Bw. Ngeleja aliyasema hayo juzi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Pambalu,
Kata ya Ibisabageni, wilayani humo akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za kukagua na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa jimboni humo.

Baadhi ya wapinzani wangu kisiasa wanatumia hoja dhaifu ambazo hazina mashiko ikiwemo ya sakata la Escrow na tatizo la maji kutaka kunimaliza...leo nimekuja hapa kuwaambia ukweli juu ya mambo hayo ili ukweli ujulikane.

Mwaka 2014, tulikuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, hapa Sengerema CCM ilishinda kwa asilimia 83 na wapinzani wetu CHADEMA waliambulia asilimia 17, najua tungeweza kupata ushindi zaidi ya huo lakini nchi ilitikiswa na masuala mawili likiwemo la Escrow na Katiba Mpya," alisema.

Aliongeza kuwa, katika sakata la Escrow, watu wasifikiri kuna ujanja wowote ulifanyika; bali fedha alizopewa ni msaada kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo jimboni kwake, uchangiaji harambee kwenye makanisa, misikiti na vikundi vya ujasiriamali.

Alisema msaada huo umetoka kwa wafadhili ili kusaidia wananchi; hivyo si kosa wala dhambi kupokea msaada kwani ruzuku inayotolewa na Serikali pekee, haitoshi kumaliza kero mbalimbali za wananchi hususan jimboni humo.
"Leo (jana), nimekuja na orodha ndefu inayoonesha jinsi nilivyotumia sh. milioni 40 nilizopewa kama msaada ambazo pia nilizilipia kodi kwa mujibu wa sheria na fedha zilizobaki, zilikuwa sh. milioni 27 pekee.

Dhamira yangu ilikuwa kuwasaidia wananchi wangu, lakini bado taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hakuna sehemu inayonitaja, suala hili lililetwa bungeni kupitia Kamati ya Bw. Zitto Kabwe (Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali-PAC)," alisema.

Bw. Ngeleja alifafanua kuwa, Bw. Kabwe ni miongoni mwa watu waliopokea mgawo kutoka kwa mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, James Rugemalira ambaye alimpa sh. milioni 33 lakini yeye hakujadiliwa licha ya kutolewa vielelezo vyote bungeni.

Kutokana na jambo hili, ukiliangalia kwa makini utagundua kuwa, wengine wakipewa misaada hakuna shida, lakini akipewa Ngeleja ni nongwa, alihoji Bw. Ngeleja.

Akizungumzia tatizo la maji linalowakabili wananchi jimboni humo, Bw. Ngeleja alisema hicho ndicho kipaumbele chake kikubwa akiwataka wananchi wawe watulivu kwani muda si mrefu, tatizo hilo litakwisha na kubaki historia.

"Upatikanaji wa maji katika maeneo mengi nchini ni tatizo la kitaifa, kero hii katika jimbo langu naifahamu na wananchi wa jimbo langu pia ni mashahidi, hivi sasa kuna mradi mkubwa wa maji ulioanza kutekelezwa wenye thamani ya sh. bilioni 23; hivyo wanaotumia kero hii kutaka umaarufu watakosa la kusema baada ya kukamilika," alisema.

Bw. Ngeleja ambaye amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, mradi huo unatakiwa kukamilika Januari 2016 lakini kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, wamekubaliana na
Mkandarasi atandaze bomba kubwa la maji kutoka Nyamazugo ili huduma hiyo ipatikane mapema.

Katika mkutano huo, Bw. Ngeleja alitoa fursa kwa wananchi waulize maswali ambao wengi wao walitaka kujua ukweli juu ya kuhusika kwake kwenye sakata la Escrow na tatizo la maji lakini waliridhika na majibu aliyowapa.

Miongoni mwa wananchi waliouliza maswali, Bw. James John, alitaka kufahamu kama Bw. Ngeleja alihusika katika kashfa hiyo, wengine wakitaka kujua hatua anazochukua
kukabiliana na tatizo la maji, mrundikano wa mahabusu katika Gereza la Wilaya Kasungamile.

Mambo mengine waliyotaka majibu ya Bw. Ngeleja na tatizo la ajira kwa vijana ambapo mama mmoja anayeitwa Letisia William, alimtaka mbunge huyo kupeleka hoja binafsi bungeni ili kuzuia unywaji pombe aina ya viroba kwa vijana.

Baada ya Bw. Ngeleja kumaliza mkutano huo, wananchi walimsindikiza kwa maandamano kwenda Ofisi za CCM wilayani humo wakicheza nyimbo za aliyekuwa kada
wa chama hicho marehemu John Komba.

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira wilayani humo, Bw. Wawa Nyonyori, aliwahakikishia wananchi jimboni humo kuwa mradi huo utakamilika kama ulivyopangwa.

"Yametengenezwa matangi matano kwa ajili ya kuhifadhi maji yanayotokana na mradi huo," alisema.

Naye Mkandarasi Mshauri wa Kampuni ya China Civil Engineering, Bw. Marco Nyagabona, alisema wameweka kipaumbele katika mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Bw. Ngeleja alivunja mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika Kijiji cha Ibondo, wilayani humo baada ya wananchi kuukimbia na kuhudhuria mkutano wake.

Mkutano huo ulikuwa ufanyike katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ibondo, ukiongozwa na Diwani wa Kata ya Nyampulukano, Bw. Emmanuel Mnwanis, umbali wa mita 50 kutoka eneo ambalo Bw. Ngeleja alikuwa akifanya mkutano wake.

CHADEMA walitumia mbinu mbalimbali zikiwemo matangazo na muziki ili kuwavuta wananchi, lakini hali haikuwa shwari kwani wananchi waliendelea kumsikiliza Bw. Ngeleja na kusababisha mkutano huo usifanyike.

CHANZO: MAJIRA WEDNESDAY, APRIL 15 2015
 
Huyu jamaa yupo vizuri na anafaa coz yupo karibu saana na wananchi wake.anafaa kuwa kiongozi wa ngazi ya juu tz
 
Mwandishi kanjanja huyo na kwa taarifa yake hatumrudish ngereja bungen mtu asiyeweza kazi wa nini sisi swala la maji hapa jimbon ni ahadi anayoisema daily na hasa inapofika mida hii ya kampeni lakn hajawai kutimiza
Alafu anajua upepo ulivyo mgumu kwakwe ndiyo maana anajishaua hapo asubir october tumpe haki yake
 
Sidhani kama kweli wewe ni mwana sengerema au unatend kuwasemea wana sengerema.

Maamuzi ya Sengerema yako mikononi mwetu watu wa sengerema.

Well done Ngeleja, njia ni Nyeupe kwako kwa ngazi ya juu zaidi kuliko hata huo ubunge.
 
Ngeleja nikiongozi asiye na papala huwa akurupuki kufanya mamuzi take, safi sana ngeleja kwa kutu weka wazi watanzania mungu akubariki sana.
 
Mwandishi kanjanja huyo na kwa taarifa yake hatumrudish ngereja bungen mtu asiyeweza kazi wa nini sisi swala la maji hapa jimbon ni ahadi anayoisema daily na hasa inapofika mida hii ya kampeni lakn hajawai kutimiza
Alafu anajua upepo ulivyo mgumu kwakwe ndiyo maana anajishaua hapo asubir october tumpe haki yake

Nadhani wewe unamatatizo muone doctor,yani kwa umri wako hujui mchango wa ngeleja hapa nchini haswa kwenye nishati na madini,au wewe sio MTanzania.
 
Kioju hujui lolote kuhusu sengerema na ukweli upo wazi,usikurupuke tuu ndg Ngeleja ni habari ya mjini na anajua anachokifanya. Kaza buti ngeleja watanzania wanakuelewa saana waache wasage lami ww mbele kwa mbele
 
Kwa mtazamo huu lazima thamani ya shilling ya Tanzania ifike 2500/ kwa dola moja ya marekani ifikapo December 2015.
 
Sidhani kama kweli wewe ni mwana sengerema au unatend kuwasemea wana sengerema.

Maamuzi ya Sengerema yako mikononi mwetu watu wa sengerema.

Well done Ngeleja, njia ni Nyeupe kwako kwa ngazi ya juu zaidi kuliko hata huo ubunge.

Mi n mwanasengerema nimaemjua vzr sana ngereja na nikwambie vzr kbsa kuwa hakuna alichokifanya ila kama anatafuta kujua upepo unakwndaje bhasi hchi ndicho nachokwambia tulishachoshwa naye labda aje mwngine hata kama ni ccm lakn sio ngereja peleka salam hzi kwake and am sure kama ccm s'rema wanataka kushnda huu uchaguz waweke mgombea mwingne na sio huyu mchovu
Subir october mkuu ntarejea hapa kukumbusha what is real in this town. Na anajua salam tulizompa wakat wa chaguz za serikali za mitaa na ukilingansha na chaguz zilizopita ni ujinga kujisifia bdo unaongoza wakat ni dhahir hal n mbaya tena hasa kwa hapa maeneo ya kata za hapa mjini achilia mbal vijijin ambapo kuna uwezekno upepo mkubwa ulo anza hapa katka kata za nyampulukano, ibisabagen na nyatukala nk kukumba kata zingne hzo mjipange mkuu kwasababu n wakat wa mabadiliko ambayo hata yaamini
 
Kioju hujui lolote kuhusu sengerema na ukweli upo wazi,usikurupuke tuu ndg Ngeleja ni habari ya mjini na anajua anachokifanya. Kaza buti ngeleja watanzania wanakuelewa saana waache wasage lami ww mbele kwa mbele

Ni aibu sana tena mno kukujibu au kujibizana na wewe, by the way endlea kuwa mpambe wa ngereja na kuwa kasuku ambaye amepofushwa na fedha chafu zinazokufumba macho. Ni kwel ngereja hawezi kusahaulika ktk wizara yake kwa kuleta mgao wa kihistoria ever.
 
.... alisema fedha alizopewa ni msaada kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo jimboni kwake,
CHANZO: MAJIRA WEDNESDAY, APRIL 15 2015

Maendeleo yanaletwa na fedha za wizi ?
Mnatuibia halafu bado mnatufanya wajinga.
 
Ni aibu sana tena mno kukujibu au kujibizana na wewe, by the way endlea kuwa mpambe wa ngereja na kuwa kasuku ambaye amepofushwa na fedha chafu zinazokufumba macho. Ni kwel ngereja hawezi kusahaulika ktk wizara yake kwa kuleta mgao wa kihistoria ever.

Wewe kioju hujui nini unazungumza au hujui nini unafanya Ngeleja amesaidia chama chake cha CCM kimepata 83% dhid ya17% za CDM richa ya kashfa za kinafiki na zakuzushiwa za escrow, we kioju unazungumza propaganda tu na siasa za maji taka lakini unajua kuwa ngeleja uwezo wake Mkubwa na ana legacy kubwa hapa nchini.
 
attachment.php
 
hap onaonyesha kua Ngeleja anatak kufanywa kam mbuz wa kafara il wngn na chama kpone...ila nina iman na ngeleja na anaweza kaz...n kiongoz anayefaa ndio maan hat hilo sakata la escrow alilipa kodi...Ngeleja pambana,.kila ktu knaugum wake...ila muda ndo utaamua
 
Wajinga ndiyo waliwao! Hana sifa ya kuendelea kuwa kiongozi wa watu,wizi mtupu! Wananchi wa sengerema pigeni chini huyo kesho kutwa kwenye uchaguzi kama sisi tutakavyompiga chini huyu mganga wa kienyeji!
 
Mi n mwanasengerema nimaemjua vzr sana ngereja na nikwambie vzr kbsa kuwa hakuna alichokifanya ila kama anatafuta kujua upepo unakwndaje bhasi hchi ndicho nachokwambia tulishachoshwa naye labda aje mwngine hata kama ni ccm lakn sio ngereja peleka salam hzi kwake and am sure kama ccm s'rema wanataka kushnda huu uchaguz waweke mgombea mwingne na sio huyu mchovu
Subir october mkuu ntarejea hapa kukumbusha what is real in this town. Na anajua salam tulizompa wakat wa chaguz za serikali za mitaa na ukilingansha na chaguz zilizopita ni ujinga kujisifia bdo unaongoza wakat ni dhahir hal n mbaya tena hasa kwa hapa maeneo ya kata za hapa mjini achilia mbal vijijin ambapo kuna uwezekno upepo mkubwa ulo anza hapa katka kata za nyampulukano, ibisabagen na nyatukala nk kukumba kata zingne hzo mjipange mkuu kwasababu n wakat wa mabadiliko ambayo hata yaamini

Wewe ndo humtaki ila wanasengerema kwake ni mia mia. Uchaguzi serikali za mitaa kashinda kwa ushindi wa kishindo wa 83% against 17% Ukawa halafu ujibalaguze kuwa hana kitu jimboni.

Kwa taarifa yako, Ngeleja ni level ya kitaifa, presidential post na sio habari ya Ubunge. Nyie jibalaguzeni tu ila yeye hana tatizo na wana sengerema maana anajua akitaka jimbo wiki moja tu anachukua jimbo.
 
Escrow ni Mpango wa wabaya wa ngeleja kujaribu kuizima nyota yake. Lakini wamechemka na ndiyo maana kanda ya ziwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kaongoza kwa 83% huku wapinzani wakigawana 17%. Ngeleja katapila. Anafaa kuongoza nchi.
 
Back
Top Bottom