Ngeleja awalipua Upinzani

Ngeleja awalipua Upinzani

Harudi tena kwenye uwaziri.Ana machafu mengi.Siku akitaka kuchukua fomu basi JF itakuwa tayari kuanika mambo yake.
 
tatizo tanzania tumejenga mfumo wa siasa wa staili ya nyani kuwacheka wengine kuwa wako uchi kumbe anayecheka na mwenyewe yuko uchi.

tunataka vyama viwe na sera ya gesi nasi tutaviunga mkono kulingana na sera zao katika hili pamoja na mambo mengine. swala la kukosoana wakati ukimuuliza wewe unayekosoa mpango wako ni upi hana.

Hujui serikali Ndo huaandaa rasmu ya sera husika na kuwakilisha bungeni Au unataka jukumu Hilo wapewe upinzani? okay kubali na kuachia uongozi wa serikali vinginevyo wapinzani watakupinga kila kosa la sera na uongozi mpaka ukubali kushindwa kuongoza vinginevyo nimeshuhudia Mara nyingi upinzani ukitoa ushauri kwa serikali ambayo huwa haisikilizi wala kujali Bali hubeza tuu.
 
Wabunge wa ccm ni wasemaji wa serikali na si wawakilishi wa wananchi! Poleni sana watanzania kwa kuwapa wasemaji wa serikali kura zenu, badala ya kuwapa wawakilishi wenu!
 
Ngeleja kajilipua mwenyewe,asitegemee wapinzani wa kweli kutoka CDM watakaa wakisifia ufisadi.in short utawadanganya ambao hawajasikiliza live.huyo fisadi kajilipua
 
Ukiona mtu ametoka utotoni afu akarukia uzeeni angalia akili yake vizuri...
 
Hujui serikali Ndo huaandaa rasmu ya sera husika na kuwakilisha bungeni Au unataka jukumu Hilo wapewe upinzani? okay kubali na kuachia uongozi wa serikali vinginevyo wapinzani watakupinga kila kosa la sera na uongozi mpaka ukubali kushindwa kuongoza vinginevyo nimeshuhudia Mara nyingi upinzani ukitoa ushauri kwa serikali ambayo huwa haisikilizi wala kujali Bali hubeza tuu.

sera zinaanzia kwenye chama, chama kinasema mfano sisi mpango wetu wa uvunaji wa gesi uko hivi. mkitupa uongozi tunaenda kutekeleza mpango huu. wakishika madaraka wanaanza kutekeleza sera zao kwa mfano sera ya taifa ya gesi haizungumzii kama kuleta wawekezaji kutoka nje au kuwekeza fedha za ndani. lakini vyama sera zao zinafafanua hili kusema sisi mtizamo wetu ni kuwakaribisha wawekezaji wa nje kuwekeza katika rasilimali ya gesi wavune tugawane. chama kinaweza kuwa na sera ya rasilimali ya gesi tukope tuiendeleze wenyewe. kila chama na aproach yake ya kusimamia na kuvuna rasilimali za taifa.

swala la kusema gesi ichakatwe wapi ingekuwa tayari iko katika ilani ya chama na watu wanapopinga sera ya chama fulani wanaangalia chama gani kina sera nzuri wanachagua kiwaongoze badala ya kufanya vurugu. sasa vyama na wabunge wake tulivyonavyo hawana sera wanasikiliza wananchi wanasema nini ndio wanasapoti wakati huo. hii ni tatizo maana unaweza kusikiliza wanaopiga kelele kumi ukawaunga mkono kumbe walio kaa kimya wanaopinga wanaopiga kelele ni wengi zaidi.

na ili kuepuka chama kuwa kigeugeu unatoa msimamo wako wanachama wanakuunga mkono wakijua misimamo yako
 
Wizara ilisafishwa kuanzia waziri mpaka chini sasa ngeleja analia bure na kujifanya kuogea kwa jazba kama vile ni waziri anajibu hoja za wabunge
 
Huyu jamaa bado ana hasira za kutemeshwa nishati na madini pale!uwaziri mtamu bwana.
 
Kumbe Ngeleja yupo!!!
Long time...
 
Ngeleja ni super fisadi hawezi kumlipua mtu ama chama chochote hata siku moja. Sana sana akijitahidi anaweza kujilipua mwenyewe.
 
Dr.Kigwangwalla alisema Ngereja naye anataka kugombea urais kupitia CCM 2015.

Nasikia kuna tetesi zinadai Ngereja ameshaanza kupanga na baraza lake la mawaziri, huenda Jairo atakuwa Waziri mkuu!!

Kwi! Kwi! Kwi! Kwi!
 
Ha! Ha! Ha! Ha! Hivi nyie CHADEMA mmewashika sehemu gani hawa ccm , Mbona wana hangaika ?
 
kweli ccm ni jamvi la kila mtu, yani hata huyu ana nguvu za kukemea? nikiangalia shida za wizara ya nishati na mkumbuka Ngeleja
 
Upinzani wa namna hii ni wa kipuuzi sana kwa nini wasiwekitu kimoja katika masuala ya maendeleo.
 
Ngeleja awalipua upinzani Bungeni leo kuwa lengo lao ni kupinga hoja zinazoletwa mezani na Serikali ya CCM. Hii ikiwa ni lengo lao kuu la kutaka kushika madaraka. Wao muda wote wako kuhangaikia kutafuta madaraka na kusahau kuunga mkono hoja za kimaendeleo za waTanzania.

Wanasema uongo na kuchochea chuki wananchi kwa Serikali yao huku wakipinga mikakati ya wizara mbalimbali ya kimaendeleo. Je huu ndio upinzani? kupinga hata maendeleo?
Siku si nyingi atajua maana ya kuwa mpinzani na kazi ya mbunge ni nini wakati yeye akiwa anasikiliza bunge kama sisi wengine huku mitaani.
 
Ngeleja awalipua upinzani Bungeni leo kuwa lengo lao ni kupinga hoja zinazoletwa mezani na Serikali ya CCM. Hii ikiwa ni lengo lao kuu la kutaka kushika madaraka. Wao muda wote wako kuhangaikia kutafuta madaraka na kusahau kuunga mkono hoja za kimaendeleo za waTanzania.

Wanasema uongo na kuchochea chuki wananchi kwa Serikali yao huku wakipinga mikakati ya wizara mbalimbali ya kimaendeleo. Je huu ndio upinzani? kupinga hata maendeleo?

mzee wa kualalumpa yupo?umewafaa vijana wanaoingia kwenye ndoa kumbi zake zimewafaa.
 
kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi ya vyama vya upinzani chadema wanafanya kazi yao ipasavyo...kupinga na kuja na hoja mbadala. We ngeleja, acha kulalama: adui yako mwombee njaa. Chadema haipo pale kwa ajili ya kuisaidia ccm kuleta maendeleo wala kuisifia. Ngeleja wewe kumbuka: Mccain vs obama is a good reference.
 
Back
Top Bottom