Ngeleja awalipua Upinzani

Ngeleja awalipua Upinzani

... haka kajamaa kanahasira sana tangu kafukuzwe uwaziri,kanaona chadema ndo mchawi wake,kwani kalizaliwa kawaziri..?? hebu kaache visasi,kila kakisimama kanalilia uwaziri tu...
 
wale wale. toka lini kipofu akamwongoza kipofu mwenzake?
 
Huyu. Ngeleja alikuwa anaongea kana kwamba anajibu hoja za wabunge. Alisahau kuwa yeye siyo waziri bali ni mbunge aliyetakiwa kuongelea mambo ya jimboni kwake. Niliishia kumhurumia. Dah! Kumbe uwaziri mtamu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Kwani Ngereja ni yupi! Kama ni yule tunaemfahamu, siamini kama anajipya. Labda alitaka wapiga kura wake wasikie kuwa ameongea bungeni
 
Pole ngeleja kwa kutojitambua...uliyokula yanakutosha.
 
... haka kajamaa kanahasira sana tangu kafukuzwe uwaziri,kanaona chadema ndo mchawi wake,kwani kalizaliwa kawaziri..?? hebu kaache visasi,kila kakisimama kanalilia uwaziri tu...

Eti nako nasikia kanawania uraisi. Nani atampigia kura mwidhi huyo?
 
naona unaweka kichwa cha habari kuwavuta watu, amewalipua wapi sasa? au kichwa chako ndo kimelipuka kusikia.habari hiyo?
 
Ngeleja awalipua upinzani Bungeni leo kuwa lengo lao ni kupinga hoja zinazoletwa mezani na Serikali ya CCM. Hii ikiwa ni lengo lao kuu la kutaka kushika madaraka. Wao muda wote wako kuhangaikia kutafuta madaraka na kusahau kuunga mkono hoja za kimaendeleo za waTanzania.

Wanasema uongo na kuchochea chuki wananchi kwa Serikali yao huku wakipinga mikakati ya wizara mbalimbali ya kimaendeleo. Je huu ndio upinzani? kupinga hata maendeleo?

William Ngeleja; a spent shell
 
Msimlaumu ngeleja, ni mhanga wa wapinzani lazma awamaind
 
Upinzani unazidi kudorora kwa kukosa hoja na kubaki walalamikaji tu
 
Anapaswa ajitazame upya kuwa amebakiza/ana kishfa ngapi na atajisafisha lini na kwa style ipi ,, kilowasa lowasaaa au kimanda makindaa
 
Ngeleja awalipua upinzani Bungeni leo kuwa lengo lao ni kupinga hoja zinazoletwa mezani na Serikali ya CCM. Hii ikiwa ni lengo lao kuu la kutaka kushika madaraka. Wao muda wote wako kuhangaikia kutafuta madaraka na kusahau kuunga mkono hoja za kimaendeleo za waTanzania.

Wanasema uongo na kuchochea chuki wananchi kwa Serikali yao huku wakipinga mikakati ya wizara mbalimbali ya kimaendeleo. Je huu ndio upinzani? kupinga hata maendeleo?

Bado yupo hai?
 
Back
Top Bottom