Ngeleja kasema mgao utaisha mitambo yote ya dharura ikishafungwa, December. Msifikiri TV mnatazama peke'enu.
Nakumbuka waziri wa nishati na madin Mh. William Ngeleja siku alipokuwa akiwasilisha bajeti yake kwa mara ya pili alitamka kuwa "unafuu wa umeme unao onekana kwa sasa nchini unatokana na kuanza kwa kutekelezwa kwa mpango wa dharula hasa kuongezeka kwa uzalishaji wa Agreco kutoka MGw 20 mpaka 100". Lakini cha kushangaza siku mbili tu baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo mgao umeongezeka kasi na kuwa maradufu sehemu nyingi hapa Tanzania, mfano Sikonge Wilaya mojawapo ya mkoa wa Tabora mgao kwa sasa ni usiku kwa usiku yaani wanakata saa moja asubuhi na kurudisha saa tano usiku kila siku toka bajeti hii ipitishwe, kabla ya hapo mgao ulikuwa kwa either kuanzia saa 3 asubuhi na kurudisha saa 10 jioni au wanakata saa 10 jioni na kurudisha saa 5 usiku. Hali hii imejitokeza kwa jiji la Mwanza ambapo umeme umekatika kwa siku tatu mfululizo baada ya bajeti ya ngeleja kupata baraka za mjengoni. Sasa kwa hali hii Ngereja anaposema kuna unafuu anamaanisha unafuu upi ikiwa hali inazidi kuwa mbaya kama si kuwadanganya waheshimiwa ili wapitishe bajeti yake? au siku hizi mawaziri kusema uongo ndio sahihi badala ya kusema ukweli. kama kuna sehemu unafuu umeanza kupatikana naomba tujuzane ili tuamini maneno ya Ngereja.
Naomba kuwasilisha.
<br />Tatizo hili ni nafasi kwa Wataalamu wetu wa kizalendo kutafuta tiba mbadala ya umeme....Co tunalalamika 2 kila kukicha.Malalamiko ye2 hayawezi kupunguza makali ya umeme...Hebu tujiulize sisi Watanzagiza wengine tunaolalamika sana tumefanya juhudi gani juu ya suala hilo?Au tuonekane tunajua kuongea? Na wataalamu wa masuala ya umeme waliokopeshwa elimu vyuoni wapo wapi?Kama wapo watusaidie kulitatua tatizo,ni kweli mvua zimezingua lakini tuna vyanzo mbadala vingi vya umeme.Mfano:UPEPO,JUAKALI SANA,MAKAA YA MAWE n.k..
Ndugu yangu wataalamu unaosema hawawezi kuleta chochote bila fedha ambazo zinakusanywa na serikali hii legelege. Serikali iwape hizo hela hao wataalamu halafu washindwe ndo tuseme na siyo kupewa wanasiasa kama RA (Richmond)Tatizo hili ni nafasi kwa Wataalamu wetu wa kizalendo kutafuta tiba mbadala ya umeme....Co tunalalamika 2 kila kukicha.Malalamiko ye2 hayawezi kupunguza makali ya umeme...Hebu tujiulize sisi Watanzagiza wengine tunaolalamika sana tumefanya juhudi gani juu ya suala hilo?Au tuonekane tunajua kuongea? Na wataalamu wa masuala ya umeme waliokopeshwa elimu vyuoni wapo wapi?Kama wapo watusaidie kulitatua tatizo,ni kweli mvua zimezingua lakini tuna vyanzo mbadala vingi vya umeme.Mfano:UPEPO,JUAKALI SANA,MAKAA YA MAWE n.k..