Ngamia 10,000 kuuwawa kwa kupigwa risasi

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Maelfu ya Ngamia kusini mwa Australia watauawa kwa risasi kutoka kwenye helikopta kutokana na kuwepo kwa joto kali na ukame.

Zoezi hilo la siku tano limeanza Jumatano, jamii ya eneo hilo imeripoti kuwepo kwa makundi makubwa ya ngamia kuharibu miji na majengo.

''Wanaambaa mitaani wakitafuta maji ya kunywa. Tunahofu kuhusu usalama wa watoto'', anasema Marita Baker, ambao wanaishi kwenye jamii ya Kanypi.

Baadhi ya wanyama pori pia watauawa.

Maafisa watakaofanya kazi hiyo wanatoka katika idara ya mazingira na idara ya maji.
Imeelezwa kuwa kutokana na hali ya ukame ngamia wamekuwa tishio kwenye jamii hivyo unahitajika udhibiti wa haraka.

Jamii zinazoishi karibu na makazi ya ngamia hao wamesema wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu, kwa sababu ngamia hubomoa uzio, huzunguka nyumba wakijaribu kupata maji kupitia maji yanayodondoka kutoka kwenye viyoyozi.

Joto kali na ukame kumesababisha moto wa nyika nchini Australia kwa kipindi cha miezi kadhaa, lakini hali ya ukame ya nchi hiyo imekuwepo kwa miaka kadhaa.

Ngamia hawana asili ya Australia- walipelekwa nchini humo na walowezi kutoka India, Afghanistan na mashariki ya kati katika karne ya 19.

Ngamia hao huharibu uzio, huharibu vifaa vya shamba na makazi, na pia hunywa maji yanayohitajika kwa matumizi ya watu katika eneo hilo.

Pia hutoa gesi ya methane, gesi ambayo inachangia mabadiliko ya hali ya hewa.

Karibu makazi 2,000 yameharibiwa kutokana na moto uliodumu kwa miezi kadhaa. Karibu watu 25 wameuawa tangu mwezi Septemba. Maeneo ya mashariki na kusini mwa Australia yameharibiwa vibaya, na wanyama wengi wameuawa kwa moto.

Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na joto kali katika kipindi cha miongo ya hivi karibuni na hali inatarajiwa kuendelea.

Wanasayansi wametahadharisha kuwa hali ya joto kali, na ukame utachangia matukio ya moto mara kwa mara na wenye madhara.

_110434866_gettyimages-1160516527.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vita ya mazingira imeanza binadamu anatwangana na wanyama na risasi kugombea maji na mazingira
Tutunze mazingira pole kwa wafiwa wote mtakaofiwa na ngamia wenu

Vita za zamani zinarudi ambapo hata binadamu walikuwa wakipigana kugombea malisho ,maji ,Ardhi nk
 
Kuna muda wazungu nao akili zao zinajaa vumbi. Wameona kuwaua ni njia pekee ya kutatua tatizo na hata kama wameleta uharibifu haipaswi kuchukuliwa hatua hiyo.

Kuna nchi ambazo zinatumia kitoweo cha ngamia wanashindwa vipi kuandaa ngamia hao na wakauzwa kwenye nchi hizo kuliko kuwaua kwa dhamira mbaya hivyo.
 
Sio tu wanyama. Hata binadamu pia wanahatarisha usalama wa dunia.

Overpopulation will soon or later bring humanity to a brutal end.

Watu wengi, wanyama wengi, maji kiduchu, jua kali, chakula kinakauka, ajira hakuna, joto kali...

Bado baba yenu anawasisitiza mfyatue bila kikomo. Hapo hapo kuna watoto wanakunya juu ya matundu mabovu ya choo cha shule, hawana madarasa, wanasoma kwenye mazingira hatarishi...

Yeye yuko kwenye kiyoyozi anakula kuku na chachandu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyama ya ngamia inaliwa na ni biashara nzuri tu,kwanini wasiweke utaratibu wa kuwachinja na kupeleka kama msaada kwenye nchi zinazokabiliwa na baa la njaa? Ni bora kufanya hivyo kuliko kuwaua hovyo tena kwa kuwapiga risasi bila huruma!
Mkuu Ngamia ni haramu. Mstari uliomharamisha nguruwe kwenye biblia huo huo pia umemharamisha na ngamia. Tena umeanza kumharamisha ngamia. Ngamia unaweza kumtumia kama mnyama kazi lakini siyo kwa kula.
 
Back
Top Bottom