Newtons laws of motion zina apply katika maisha!

gstar

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
759
1,250
Mwanasayansi Isack Newton katika uchunguzi wake alitengeneza sheria kuu tatu za mwendokasi nazo aliziita Newton's laws of motions tuangalie sheria hizi zina apply vipi katika maisha!!

1."Every body continues in the state of rest or uniform motion in a straight line unless there is an external force acts other wise"
Tafsiri--- utaendelea kuwa na maisha hayo hayo uliyo nayo hayata panda wala hayata shuka mpaka utokee msukumo wa nje( msukumo hasi au msukumo chanya) au ufanye maamuzi magumu ya kubadilika kwa kufanya kazi kwa bidii.

2. "The rate of change of momentum is directly proportional to the force applied"
Tafsiri-- Mabadiliko ya maisha yako yatategemea juhudi utakazo weka wewe mwenyewe binafsi au msaada kutoka nje, ukifanya kazi kwa bidii utafanikiwa, ukiwa mzembe utaharibikiwa na kushuka kimaisha.

3. "To every action there is an equal with the opposite reaction" Tafsiri--- chochote utakacho kitenda kitakuwa sawasawa na matokeo yake kwa upande wapili, mfano ukiwa mvivu utavuna uvivu, ukiwa mchoyo nawe utanyimwa, ukiwa mtoaji nawe utakirimiwa... penda kusaidia wasio jiweza kama umebarikiwa kupata kidogo kwani mkono unao toa ndio utakao pokea.

Nb:- Hii sio tafsiri halisi ya sheria hizi, ukishindwa kuzielewa nicheki kwa pm
By G.Star
 
Back
Top Bottom