Samahani wana Jamvi mnivumilie kidogo na kama sio mahala pake basi naombeni mnisamehe lakini kuwagutusha ni jukumu langu pia. Ni hivi; leo terehe 3/05/2013 siku Ijumaa majira ya saa 11.15am na saa 02.50am kuna watu wawili wamempgia jamaa yangu simu wakijifanya wanamjua saana jina ila tu hawajui anapatikana wapi wala anafanyakazi gani.. Wanamwambia kuwa wako kwenye mradi wa Kilimo Kwanza huko Rufiji na wanamatekta tisa mabovu wanataka mtu wampe tenda ya kununua spea..sijajua namba ya huyo jamaa yangu wameitoa wapi ila wanajifanya kumfahamu sana. Katika kufuatilia namba hizo ambazo ni 0714 979 167 huyu jina hajalipata na mwingine ni namba yake ni 0652 036 102 amesajili namba yake kwenye Tigo Pesa ni BONIFACE MGAMBA. Hivyo nimeona niwagutushe kuna utapeli wa aina hii unaendelea hapa kwa sasa muwe makini na hizi namba. Pia wanaweza kutumia namba nyingine ni vema kuwa mdadisi mno pindi watakapokupigia kwa namba ngeni!!
Nawasilisha kama siasa za utapeli kwa njia ya Simu
Nawasilisha kama siasa za utapeli kwa njia ya Simu