News Alert: Rafu kura za maoni CCM Temeke

News Alert: Rafu kura za maoni CCM Temeke

Magimbi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
1,434
Reaction score
1,215
Hapa sasa uwani wanapigwa watu picha na kuandikishwa majina ili watengenezewe vitambulisho vya CCM. Kumbuka hili zoezi lafanyika kwa siri na wanakusanywa watu wanadhani ni vitambulisho vya kupiga kura kumbe ni kadi za CCM zianzoandikishwa kwa ulazima ili mgombea aliyeratibu zoezi hili apate kura za kutosha. Hapa mtaa wa Yombo wanatarget wana CCM kama 300 hivi..sijafahamu mgombea gani anafanya fojari hii lakini nitaipata tu taarifa soon kwa huyu mjumbe wa CCM mtaa wetu huu.

Jamani chama chetu..lini tutakuwa objectivebkatika kusaka madaraka. Kwa nini ni ukanjanja kwa kila kitu jamanii. Daah kweli CCM ya Nyerere ishazikwa rasmi na hii ya wafisadi. Natamani iruddi tena. Nilikuwa nasimuliwa tu na kubisha lakini leo hii muda huu najionea. Kadi za kulazimisha jamani tena burs hutoi hata ile ada ya uwanachama.. Duu Mungu iibariki Tanzania
 
kama rafu zilifanyika kwenye uraisi itashikeje kwenye Ubunge na Udiwani?
 
tena umechelewa sana kujua , hiyo ndio mbinu ya ccm temeke miaka yote , ajabu ni kwamba kila kambi inafanya hivyo , wahusika hulipwa 5000 tu .
 
Wewe unamuona Lembeli mjinga hadi akafikia hatua ya kuikimbia CCM!? CCM ya leo kama wewe ni masikini subiri tu kupigia kura matajiri.
 
Na bado mpaka mjue vyama ni mitaji ya wachache. . . . . mkiacha kushabikia vyama baaas kitaeleweka
 
Hapa sasa uwani wanapigwa watu picha na kuandikishwa majina ili watengenezewe vitambulisho vya CCM. Kumbuka hili zoezi lafanyika kwa siri na wanakusanywa watu wanadhani ni vitambulisho vya kupiga kura kumbe ni kadi za CCM zianzoandikishwa kwa ulazima ili mgombea aliyeratibu zoezi hili apate kura za kutosha. Hapa mtaa wa Yombo wanatarget wana CCM kama 300 hivi..sijafahamu mgombea gani anafanya fojari hii lakini nitaipata tu taarifa soon kwa huyu mjumbe wa CCM mtaa wetu huu.

Jamani chama chetu..lini tutakuwa objectivebkatika kusaka madaraka. Kwa nini ni ukanjanja kwa kila kitu jamanii. Daah kweli CCM ya Nyerere ishazikwa rasmi na hii ya wafisadi. Natamani iruddi tena. Nilikuwa nasimuliwa tu na kubisha lakini leo hii muda huu najionea. Kadi za kulazimisha jamani tena burs hutoi hata ile ada ya uwanachama.. Duu Mungu iibariki Tanzania

Kumbe watu mpo ccm halafu hamjui hata kinachoendelea?

Ni hivi reja za wanachama zimeshafungwa na ccm wamechapisha leja mpya kwahiyo wanachama wa zamani wanahamishiwa kwenye leja mpya na mgombea aliyesuka mipango anaingiza wanachama feki humo humo.

Mfano kata ina wanachama hai 600 tu utashangaa leja ya matawi sasa hivi kata inafikisha wanachama 6000. Tayari kuna kadi zimechapishiwa china.

Hizi kadi zimechapishwa kwa wingi China kwa ajili ya kucheza rafu ya kura za maoni na hakika mtashuhudia vilio baada ya kura hizi.

Na hii ndio faulo anayoitegemea Makongoro Mahanga na nawahakikishia atashinda ndani ya ccm ila wakandarasi tunamsubili site.

Nawapa ushauri wa bure ccm na Nape asome hapa njia pekee ya kuinusuru ccm ni kupiga kura za wazi kila kata wagombea wapange foleni wanaowaunga mkono wasimame nyuma yao na hii ndio njia pekee ya kukomesha unafki wa vizee vya ccm kula pesa za kila mgombea.

Ni kula za wazi tu ndio zinaweza kuinusuru ccm na zimwi la kura za maoni.

Naandika haya kwa uchungu mkubwa kuna watu wazuri ndani ya ccm wanazimwa ndoto zao kwa sababu ya ujangili huu wa kuingiza wanachama hewa kwenye leja unaoratibiwa na makatibu wa matawi na makatibu kata kwa ubinafsi na njaa ya pesa.

Na kama Kikwete wale wanachama anaosema wa ccm wapo millioni sita( 6) basi anajidanganya ccm ina colum kubwa tu lakini si wanachama,wanachama wa ccm hawazidi millioni tatu( 3) tu. hizi leja zinawadanganya sana ccm kwenye leja za ccm wapo hadi wanachama wa upinzani wanaingizwa kwa mkopo kwa ajili ya zoezi la kura za maoni tu ila zikija kura za umma ndio maana mnashangaa mtu anaanguka.
 
Jamaa ana uchungu na magamba. Huenda nae ni mtia na ameshindwa kucheza rafu. Rafu ndo jadi ya ccm. kama vipi nawewe cheza rafu au funga goli la mkono huko huko ndani ya chama
 
mimi mwenyewe broo wangu alienda nyumbani kwa mh. mmoja na wenziwe wakapewa kila mtu 25000.
 
I bet mtoa mada ni mtia nia but hana "kamati ya fitina"
 
Back
Top Bottom