LGE2024 Kura za maoni zazua 'mtiti' Unga Limited – Arusha, wengine watishia kutompa kura kada wao wa CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,793
6,635
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Viwandani kata ya Unga Limited Jijini Arusha, wametishia kutompa kura za ndio mgombea wa uenyekiti wa mtaa huo kupitia chama hicho endapo aliyeshinda kura za maoni hatawekwa kama mgombea katika nafasi hiyo.

Wanachamama hao wakizungumza na GADI TV mara baada ya kuandamana kwenda kwenye Ofisi za Chama hicho wilaya ya Arusha Mjini, wamesema wanashinikiza ndugu Rasuli Mshana ambaye alishinda kura za maoni ndani ya chama hicho jina lake lirudishwe ili aweze kugombea nafasi hiyo kutokana na ni mtu anayekubalika zaidi kwa wananchi.

Chanzo: Gadi TV
 
Wampe wa Chadema sasa wananchi waliogoma kujiandikshaji kupiga kura 🐒
 
Back
Top Bottom