NEW! Nyayo za Mwanadamu wa kale, Zaidi ya 400 zagunduliwa Tanzania.

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
394CD7C500000578-3832444-image-a-25_1476188961382.jpg

Wanasayansi na watafiti wamepata ushahidi wa kipekee sana duniani kwa kupata nyayo Zaidi ya 400 za mwanadamu wa kale katika tabaka linalokadiriwa kuwa na miaka 5000 mpaka 19,000. Nyayo hizo ni za makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wametembea juu ya tope la majivu ya volcano pembezoni mwa Ziwa Natron katika site iliyopewa jina la Engare Sero, sio mbali na mlima wa volcano wa Ol Doinyo Lengai (Mlima wa Mungu kwa tafsiri ya Kimasai).

-a-3_1476261934777.jpg

Kuna nyayo nyingine za 3.5 Millioni ambazo zipo Laetoli na zinashikilia rekodi ya kuwa nyayo za kale Zaidi. Pia kuna nyayo za South Afrika ambazo zinakadiriwa kuwa na miaka 117,000 zilizogundulika mwaka 1995.


Nyayo hizi zilizogundulika hivi karibuni zina upekee sana kutokana na wingi wa nyayo na zimehusisha watu wa aina nyingi. Katika vipimo vya foot anatomy inaweza kuonyesha size ya individual, ukubwa wa mwili pamoja na umri. Hii itasaidia pia kuchunguza tabia za jamii. Hii ni kutoka kwa Dr Cynthia Liutkus-Pierce kutoka chou kikuu cha Appalanchian State University ambaye ni geologist na mwanachama wa National Geographic Channel.

Kipimo cha umri wa hizo nyayo kilitumia Radiometric dating ya kupima crystals za udongo mgumu wenye hizo nyayo.


Hii ni mojawapo kati ya tafiti kubwa duniani kuhusiana na mambo kale katika bara la Africa hususani Tanzania. Tanzania imekuwa ikiwa na ushahidi na site kubwa zinazofahamika duniani lakini je tunazitumia vipi hizo site katika kuleta maendeleo?

2_1476261871073.jpg
 
He he he! mkuu vitu vyengine huonekana vidogovidogo lkn hupelekea kuja kubainika kwa vitu vikubwa let them work.
umeshajiuliza kwanini maeneo hayo tu(kwa hapa bongo) ndo kunapatikana vitu kama hivyo..?
Mangapi walishayagundua lakini mpaka leo hali ndo ile ile tu?,
wasitake kutuchezea,
tena unakuta baada ya kitu kugunduliwa ndo hali inazidi kuwa mbaya...
 
Mangapi walishayagundua lakini mpaka leo hali ndo ile ile tu?,
wasitake kutuchezea,
tena unakuta baada ya kitu kugunduliwa ndo hali inazidi kuwa mbaya...
Ha ha ha leo naona wanajamii wenzangu mmekasirika sana duh!.
nadhani wanaweza kuifanya kuwa sehemu ya utalii waweke promo tu
 
Hivyo vitu bora hata wasiendelee kuvigundua, manake vipo vingi vyamaana vilivyogunduliwa na bado haviwafaidishi wananchi..
UPUUZI

Bado serikali haioni kuna umuhimu. Researchers wa hizi project wengi ni wazungu na watanzania wanaohusika pia kuwa funded za external sponsors.

Funds za Tanzania hazionekani.

Museums na vituo vya kuhifadhi havipo

Experts wengine hawana kazi

Kuna vituo vya mambo kale zaidi ya elfu havina cultural officers .
 
Ujinga wa wazungu..hivi wewe kila siku unatembea kwenye tope ...kila mahali jee ujaacha mark yoyote ije ionekane miaka 100 ijayo?
Wazungu mengine wanapiga jaramba tu
 
Tutabaki na hayo hayo but kunufaika nayo hakuna, fyuuuuuuu!!

Faida ya tourism, Unesco na mashirika ya nje ni kubwa pia. Plus pesa za vibali vya research na visa ni faida. Bado museums na identity ya nchi.

Pia ukiachana na faida, Kwa kanuni za kimataifa ni lazima kila nchi kutunza heritages yake.
 
Ujinga wa wazungu..hivi wewe kila siku unatembea kwenye tope ...kila mahali jee ujaacha mark yoyote ije ionekane miaka 100 ijayo?
Wazungu mengine wanapiga jaramba tu

Sio tope unalolifahamu mkuu, ni tope la majivu baada ya kulipuka volcano. Tope lake likikauka huwa extrusive igneous rock.
 
Back
Top Bottom