New Mzalendo Style. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

New Mzalendo Style.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Malila, Feb 2, 2012.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Ukisoma uzi wa ufugaji kuku aliotoa Mzalendo unaweza kucheka, kwa sababu alisema ukweli kwamba alianza na kuku mmoja tena jogoo,baadae alimla. Hii style ni nzuri kwa sababu, kwanza inakuondoa kwenye nadharia na kukupeleka kwenye vitendo. Imebidi nii-copy na kui-paste kwangu. Nimenunua ng`ombe mmoja tu chotara aliyepandishwa. Kwa wale wanaopenda kufuga ng`ombe basi tuwasiliane hapa hapa jamvini. Mzee aliyeniuzia mimi ana ng`ombe wengi wazuri na bei yake ni nzuri.
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Malila uliyoyanena ni ya kweli kabisa

  kuna sector ambazo serekali ingekuwa imeweka msukumo naamini ingewatoa watanganyika wengi,,kila siku nafikiria UVUVI, UFUGAJI HUSUSANI UZALISHAJI WA MAZIWA, ASALI, MBUZI=KONDOO wanasoko kubwa sana Arabuni mayai. Tatizo watawala wetu wamekosa dira tu hakuna lingine

  kaka naomba utupe taarifa zaidi hawa mifugo wanapatikana wapi na kwa bei gani? Ukimwgaga taarifa hapa utakuwa umesaidia wengi saana,,,mie nilikuwa nataka ngombe kama wawili waliopandwa nitakushukuru ukini PM

  Ubarikiwe saana
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Hawa ng`ombe wako Mkuranga, bei yake ni laki sita tu bila dalali. Ukitaka wa kienyeji ndama mdogo andaa laki tatu,lakini chotara ndama mdogo andaa laki nne tu.
   
 4. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Kaka nashukuru saana
  hawa ngombe ni aina gani mkuu
  naweza pata Borani ambao wamechanganyika?
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Huyu mfugaji aliniambia ni crossbreed ya Mafia. Sasa na mimi nikasahau kutafuta hii breed ya Mafia ni ipi/inafanana na ipi. Tutapata majibu japo kwa kuchelewa kidogo.
   
 6. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ndo maana napenda hapa jukwaani!!
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Kuna rafiki yangu mmoja kapata Boran toka sehemu fulani baada ya kushindwa kupata frisien (spelling sijui), nitamuuliza kama Boran bado wapo.
   
 8. bulldoza

  bulldoza Senior Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana mkuu,sasa mkuranga kubwa lakini naomba maelekezo zaidi niko mbioni soon ntamaliza ujenzi wa banda langu nipate japo mmoja wa kuanzia aka newmzalendo style tuko wengi ,...
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Mkuranga mjini kabisa pale pale, nitakupa simu yangu kwa njia ya PM ili nikuelekeze vizuri.
   
 10. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Just out of curiosity Mkuu Malila. Hivi hao ng'ombe wa Mkuranga wanatoa maziwa takribani lita ngapi kwa siku?
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Huyu Mkulima alisema mzao wa kwanza unaweza kupata lita tano asubuhi na jioni pia kama unamlisha vizuri. Mkulima huyu yy hakumui maziwa kwa biashara, ni yake na watoto wake. Nilichojifunza ni kwamba mpango wa maziwa hana,hata pale home kwake hata maji ya kunywa mifugo yake hana. Ila ana ng`ombe wengi sana na wazuri kiafya.
   
 12. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Shukrani Mkuu, huyu Ngombe anaweza akawa msaada mkubwa sana kwenye kulea familia hapa mjini, lakini naona kama hajakaa vizuri sana kibiashara. Kuna ndugu yangu yeye aliagiza Friesian Cow mmoja kutoka Kenya akampeleka Moshi, anatoa 35 ltrs per day. naona wazee wake hawamsumbui tena na hela ya kujikimu. Naona kama aina hii imekaa vizuri kibiashara, kama una eneo zuri na unakaa sehemu isiyo na Joto kama Dsm
   

  Attached Files:

 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Friesian nina wajua walipo, nina uwezo wa kuwachukua, lakini ni delicate sana kwa mazingira ya pwani. Pili, sasa hivi nafanya in-house training kwa vijana wangu ili wajue kukaa na ng`ombe wa maziwa,tatu nataka huyu Chotara awe ndio mlipa mshahara kwao. Sasa nikiona wamemudu vizuri kumtunza huyu Chotara, naleta aina nzuri toka Ruvu, kisha tunagawana. Maziwa ya Chotara yao na huyu mpya yangu. Chotara akizaa mtoto wa kwanza wangu, wa pili wa kijana wangu. Hii ndio plan yangu.
   
 14. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  I salute you, your Honour.Kwa ridhaa yako, naomba nireplicate hii model sehemu fulani, lakini kabla ya kufika huko nitakuwa nimeshakutafuta ili nijifunze kitu fulani hata kama ni kwa kugharamia. Aksante
   
 15. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu Malila; i salute you man, sasa mimi nitakutafuta kuanzia tarehe 25 ili tubadilishane mawazo...
  Nina ndoto ya kua mjasiriamali
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Kama uko Bongo, basi mimi nitakuwepo kuanzia 28 february mpaka 27 march, ktk kipindi hicho naweza kukutana na wewe bila shida. Ktk mambo haya ya kupeana uzoefu, gharama hazitakiwi kuwepo kabisa. Naamini tutaonana. Hiyo itumie tu ndugu, mafanikio yako ndio mafanikio yangu na jamii kwa ujumla.
   
 17. M

  Malila JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Hata mimi pia nitafurahi tukionana ili na mimi nipate kutoka kwako. Nitaingia Dar february mwishoni, Mungu ni mwema atatupa muda na afya.
   
 18. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Noted. Nimeshaiingiza schedule yako kwenye Kalenda yangu, nadhani tutakuwa na mengi ya kujifunza Mkuu. Aksante na Kila la heri pia
   
Loading...