New Mount Meru Hotel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

New Mount Meru Hotel

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ndezi, Dec 2, 2010.

 1. n

  ndezi Member

  #1
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani kwa wakaazi wa Arusha na vitongoji vyake watakuwa wameshaona kwenye mabango mbalimbali barabarani ama kupitia redio ama magazeti ya kuwa iliyokuwa inaitwa novotel mount meru hotel inafunguliwa tena upya ikijulikana kama New Mount Meru Hotel.

  Kikubwa nachotaka kuwafikishia watanzania wenzangu ni kuwa nimestaajabika sana ile maana kamili ya uwekezaji kuendelea kutupwa kapuni. Huwezi amini moderator na watanzania kwa ujumla, Hotel hii hadi maua na mchanga vyote vimetoka South Africa ambapo ndipo ilipo kampuni iliyopewa jukumu la kuindesha hotel hii ijulikanayo kama Zabulan.

  Nachokiona hapa ni kuwa wasauzi afrika wao wanathamini vyao hata kama wako nje ya kwao, itakumbukwa watu walishapiga kelele kuhusu bidhaa zipatikanazo shoprite ya kuwa hadi nyanya na vitunguu hata mchicha vinatoka hukohuko SA, sasa ambacho watu watajionea hapa ni kuwa mchanga, maua, mbolea, signboards, tisheti, viatu, sabuni, vitambaa, computer, curtains na vyooote vinatoka sauzi afrika, hivi ina maana hapa hatuna hivyo vitu; vingine itasemekana labda viwango na jee hata mbolea na mchanga??

  Kali zaidi ni kuwa Senior staffs woote ni ndani ya sauzi afrika ama asia au kwa watani wa jadi, ina maana hapa hatuna mameneja wazuri wakuendesha hotel? hatuna mashefu wazuri hapa tz?

  Ikumbukwe walisema katika ajira wataweka mbele wazawa...hii imefia wapi??

  Kama uwekezaji ndo hivi jamani bora tufie na tai shingoni.

  Kali nyingine ni kuwa Raisi wetu yuleyule aliyeifunguaga Snow Crest Hotel then kesho yake ikaja kuvunjwa ukuta ndio anakuja tarehe 17Dec kuifungua hii ambayo ilikuwa mali ya watanzania then mkapa na magufuli wakaiuza na sasa watanzania hawana hata percent moja hapa, hilo moja pili ni kuwa wafanyakazi woote ni wametoka kenya ama sauzi afrika ma bara asia na pia waliopewa tenda za ku-supply vyakula ni wakenya tupu na vyote vinatoka hukuhuko kenya kuanzia kuku, maharage hadi matunda, jamani rais hana washauri wakamfungua kwenye hili na jee watanzania tutakuwa wapole hadi lini watu wanakuja kupora malighafi zetu na kukimbia??

  Ama ndio kichwa cha mwendawazimu??

  TUAMKE WATANZANIA NA TULIANGALIE HILI SWALA LA MOUNT MERU KWA JICHO LATATU.

  NGUVU YA UMAA IFANYE KAZI JAMANI............
   
 2. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Naomba kuuliza hao si ndio walioiua hii hotel kabla ya kubinafsishwa?
   
 3. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa sijui kumbe Tanzania tunazalisha Computer? Hii kali...
   
 4. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Source?
   
 5. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hii hotel ilipokuwa imefungwa hukupiga kelele leo inafunguliwa unajitokeza mbona kama vile unachuki binafsi mkuu...unataka kusema hakuna mtanzania aliyeajiriwa pale embu angalia hii documentary: YouTube - Ubinafsishaji na Maendeleo
   
 6. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Acha uongo wewe hii hotel inamilikiwa kwa ubia mwenye hisa nyingi ni Sunda mfanyabiashara wa madini Arusha na anaimiliki kupitia kampuni ya blue jewel ya Arusha, acha kudanganya wana jf ukifikiri wote hatuna taarifa umetumwa nini?
   
 7. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kampuni ya Blue jewel iliingia ubia na Southern Africa Development Fund, ndio wawekezeaji wenza wa Sunda ukiiendelea na uongo wako hapa nakuumbua.

  Acha chuki tunataka mji wetu wa Arusha uendelee na sio kuleta chuki kama zako
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hii ndiyo nchi yetu jamani, plz tuache kuhoji haya mambo tusije tukaambiwa ni wabaguzi hivyo tunahatarisha amani ya nchi yetu
   
 9. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu umekanusha ipasavyo hapo...

  Lakini;

  Vipi kuhusu huo mchanga na maua ...

  Taarifa zilizotolewa hapo nazo ni kwlei au si kwlei!!

  ..Ili tujue uzalendo ...uliopo hapo ni kiasi gani!
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Mchaga,

  Mkuu wangu Sunda ana hisa chache sana wawekezaji ndio majority shareholder.sunda alifulia siku nyingi hakuwa na sababu ya kuvunja vunja Mt meru alitakiwa kufanya ukarabati kidogo uku biashara ikiendela alikuja gundua hawezi kuikarabati hotel mwenyewe ikabidi awaite wawekezaji wa kumsaidia kuikarabati na kuiendesha upo mkuu.Ebu fikiri kidogo muda aliotumia kuikarabati hadi leo ni miaka mingapi.Kwa taarifa yako Mt meru bila mkono wa F Sumaye waziri mkuu mstaafu Sunda asingeipata sana sana wanamtumia.
   
 11. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Aminia Ngongo!
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Sumaye naye yumo?
   
 13. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,946
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Ndio manake ,unauliza ndevu kwa Osama
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tz shamba la bibi unaweza kuta mpaka wapishi wote,toilet attendants etc watatoka kenya sisi tutaambulia kuwa walinzi
   
 15. H

  Haika JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  mwenzenu huwa napenda kujua source ya Tatizo. ningeomba ufafanuzi wa sheria, sera nk
  - mtanzania anaruhusiwa kuuza ardhi kwa mtu ambaye si mtanzania? (100%)
  - ubia ulioko wa makampuni yanayomiliki hii hoteli ni wa asilimia ngapi? yani shares ngapi
  - je inawezekana management team ya investment kuajiria yot ekutoka nje ya nchi?
   
 16. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,061
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  Yote hii ni sababu ya Nyerere! Kama si yeye Watanzania wasingekuwa ***** mtozeni, washamba, wa.....
   
 17. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  kwanza sijaona chochote cha maana walicho ifanya hiyo hotel . sisi tulijua itakuwa kali kuliko kilmanjaro kempinski . huu ni upuu tu wamefanya.
   
 18. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Nice and Beautiful again,
  Looks like Kempinsk Kilimanjaro Hotel.
  Arusha ni Mahoteli Full kuanzia Sanawari,Ngurelo & Philips hadi raha.

  Karibuni Sana Arusha.
   
 19. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180

  hamna kitu hapo . hivi unajua mount meru na umuhimi wake kwa Arusha?
   
Loading...