New month first 01 November

New month first 01 November

mwaibile

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2022
Posts
2,136
Reaction score
5,170
Natumaini tupo poa,mungu awape hafua kwa wagonjwa,mwaka ulianza kwa slow motion dah 🄲 kufika kati kwangu naona speed ikawa kali sana,now tumeanza novemba,yote kwa yote tushukulu kwa yote hata kama malengo uliyojiwekea mtu hayajatimia kikubwa linda afya,maana afya ndo utajili wa kwanza,boss wako atakupenda ukiwa na afya ya kumfanyia kazi zake,tuwe na siku njema na ibada njema
 
Ee Mungu Baba yetu uliye mbinguni, tunakuja mbele zako kwa moyo wa shukrani na unyenyekevu. Tunakushukuru kwa kutulinda, kutuhifadhi na kutuvusha salama katika miezi iliyopita. Leo umetupa neema ya kuiona tarehe 1 Novemba. Si kwa nguvu zetu, wala si kwa uwezo wetu, bali ni kwa rehema na upendo wako.

Bwana, tunakushukuru kwa zawadi ya uhai, afya, familia na nafasi nyingine ya kuendelea kuishi katika kusudi lako. Tunaomba utangulie mbele yetu katika mwezi huu mpya. Utuongoze katika kila hatua, utupe hekima katika maamuzi yetu, utulinde na mabaya, na utujalie mioyo inayokutafuta kwa bidii zaidi.

Baba, leo tunakuja pia mbele zako kwa ajili ya wale wote ambao bado wanaishi katika dhambi. Wale waliofungwa na ulevi, uzinzi, uasherati, ushoga, usagaji, wizi, uongo, chuki, kiburi na kila aina ya uovu. Wale ambao bado hawajakujua, na hata wale wanaokujua lakini wameiacha njia yako.

Ee Bwana, usiwaache waangamie katika dhambi zao. Waguse mioyo yao kwa Roho wako Mtakatifu. Wafungue macho yao watambue hali zao za kiroho na waone umuhimu wa wokovu unaopatikana katika Yesu Kristo. Wape neema ya kutubu kwa kweli na kuziacha njia zao mbaya.

Tunawaombea pia wale wanaodhani kwamba wanaweza kuishi bila wewe, wale wanaojivunia dhambi zao, wanaodharau Neno lako na wanaopinga injili ya Yesu Kristo. Bwana, uwahurumie. Kama ulivyotuhurumia sisi tulipokuwa bado wenye dhambi, wahurumie na wao. Wafikishie ujumbe wa wokovu na uwape mioyo mipya.

Bwana Yesu, tunatambua kwamba hakuna mwanadamu anayeweza kujikomboa mwenyewe kutoka katika utumwa wa dhambi bila neema yako. Tunakuomba uwainue walioanguka, uwaponye waliovunjika moyo na uwatafute wale waliopotea.

Tufanye sisi kuwa vyombo vya kuifikisha injili yako kwa upendo, ujasiri na unyenyekevu, bila kuwahukumu wengine kwa kiburi, bali tukikumbuka kwamba nasi tuliokolewa kwa neema yako.

Tunayaweka maisha yetu, familia zetu, nchi zetu na ulimwengu mzima mikononi mwako katika mwezi huu wa Novemba. Tunaomba mwezi huu uwe mwezi wa toba, wokovu, urejesho na ushuhuda wa ukuu wako.

Tunakushukuru kwa sababu tunajua kwamba unasikia maombi yetu. Tunaomba na kuamini katika jina kuu la Yesu Kristo, Mwokozi na Bwana wetu.

Amina na Amina!
 
Natumaini tupo poa,mungu awape hafua kwa wagonjwa,mwaka ulianza kwa slow motion dah 🄲 kufika kati kwangu naona speed ikawa kali sana,now tumeanza novemba,yote kwa yote tushukulu kwa yote hata kama malengo uliyojiwekea mtu hayajatimia kikubwa linda afya,maana afya ndo utajili wa kwanza,boss wako atakupenda ukiwa na afya ya kumfanyia kazi zake,tuwe na siku njema na ibada njema
Happy new month to y'all
 
My friends,
ladies and gentlemen,

Kesho ni siku ya Marehemu Wote inayojulikana Kilatini kama Commemoratio Omnium Fidelium Defunctorum, huadhimishwa kila mwaka tarehe 2 Novemba ili kuwakumbuka, kuwaenzi na kuwaombea waamini wote waliotangulia mbele ya haki.

Ukipa fursa ni muhimu kuhudhuria ibada hiyo ya maana sana.

Hata hivyo,
ni muhimu sana kujiombea wenyewe ili Neema na Baraka za Mungu ziwe pamoja nasi tunapoelekea kumaliza mwaka 2026.

Kumbuka,
hakuna extra time katika maisha šŸ’
 
Back
Top Bottom