New Barrick Group kuinunua Acacia


Hizi hoja zote mbili ni kitu kimoja kwasababu katika UWEKEZAJI NI JINA ZURI LINA SEHEMU KUBWA SANA. Hivyo Barrick/Accacia kachafuka lakini pia Tanzania imechafuka sana. Kwasababu kuna mwingine kasema juzi hili deni tunalodai ni gharama ya safari ya kwenda mwezini na kurudi.


Hapa nakubaliana na wewe nusu-nusu. Kweli mzee alikurupuka kutaka sifa za kisiasa lakini ilikuwa ni kwa fiada ya nani hata kama angepata sifa za kisiasa na kufanikiwa ? Jibu ni faida yetu sote. Japo itabidi abadilike na aache tabia za kukurupuka kwasababu ana hiyo rekodi mbovu kuanzia kwenye Samaki hadi Bombardier.


Hoja ambayo ninabisha na vijana wengi hapa siyo kuhusu uhalali wa mikataba. Hata kama tunapata asilimua 5% kama tulisaini huo mkataba basi makosa ni yetu sisi na mkataba utaendelea kuwa halali. Hoja ya msingi ni hizi zifuatazo: Je, tuendelee kuibiwa kisa mikataba ni halali ?

Hiyo hoja yako pia ya kutokuwa na skilled workforce, teknolojia, miundombinu n.k nakubaliana nayo. Hata Baba wa Taifa aliliona hili
Pia, tunasema hawa watu wanatuibia, tunapika ripoti kuonyesha huo wizi sasa hii si hisia zaidi ya uhalisia? Kama tunaibiwa ni kitu gani haswa tunaibiwa? Tuna ripoti inayoonyesha uhalisia wa tunachoibiwa ukiachilia hizi ripoti feki? Kama hamna ni kipi hasa tunaibiwa.

Ni kiasi gani tunataka kupata kama nchi ili tusiwetunaibiwa. Mpaka sasa naona watu wanasema tunaibiwa lakini ni kiasi gani haswa tunaibiwa? Pia tuelewe hii ni biashara ambayo mtu kaweka mtaji wake apate faida.

Mwisho wa siku isijekuwa hatujui tunachotaka kiasi kwamba hata tukipewa kiasi fulani cha pesa bado tunasema hawa watu wanatuibia. Kama hujui unachoibiwa ukienda kwenye majadiliano unajuaje bado huibiwi?

Mkuu ngoja nimalizie kazi ya muhimu halafu ntakuja kuchangia!
 
Haya ndo yale niliyokuwa nayasema wakati ule! Hata baada ya "merger", New Barrick Group ndo hapo ina thamani ya USD 18.3 Billion.
Hivi wewe kwa akili yako, unakubali kuwa takwimu hiyo iko sahihi? Kama si uzwaza ni kitu gani?

Mo (Mohamed Dewji) kampuni yake tu binafsi ina thamani ya USD 2.8 Billion. Eti kampuni ya Acacia ina thamani ya USD 303 million, sawa na thamani ya ndege ya Dreamliner yetu moja tu? Don't be fooled so easily.
 
Chige, mwaka 2017 walikuwa na reserves za Madini za thamani ya Pound 14Billion i think ni kama zaidi ya Usd20 Billion. Hapo bado hujaweka Machines za uchimbaji na Assets zingine. Nafikiri hiyo iliyotajwa bado ndogo wakishaungana ndo itazidi zaidi.
 
Ik
Iko siku dharau hizi utaacha baada kuona tumelipwa
 
Mkuu kwa hili uko sawa tulishadanganywa kulaliwa tusikubali ijirudie
 
Ki ukweli hapa kuna kadhia mbili... kadhia kwenye sekta ya madini kwa ujumla na kadhia kwenye suala la Acacia! Kama kweli Acacia ni wezi, sitaki kuamini hata kidogo kwamba makampuni mengine yote hawatuibii except Acacia!

Zamani (before 2016) kila mwaka nilikuwa na utaratibu wa kusoma official government reports za uzalishaji wa madini kwa makampuni yote makubwa ya uchimbaji madini! Ripoti hizi zilikuwa for public records kwa sababu zilikuwa zinapatikana kwenye tovuti ya wizara!

Hivi sasa hizi ripoti ni ama hazipo public au wanaziweka sehemu nyingine lakini kule ambako nilikuwa nazifukuaga siku hizi zisioni!

Kwenye ripoti zile ambazo hivi sasa watu wanaweza kuzi-discredit kwa sababu zilikuwa zinakuwa approved na TMAA, zilikuwa zinaonesha kampuni kama Geita Gold Mine ndie largest gold producer nchini; discredit ambayo mbele za sheria haiwezi kuwa na nguvu yoyote kwa sababu hadi sasa hakuna aliye-prove beyond reasonable doubt kwamba TMAA walikuwa wanakula rushwa!

The question is: Huyu GGM na wenzake (excluding Acacia) ni kwanini na wao wasifanyiwe Special Mineral Production Audit kama "walivyofanyiwa" Acacia? Kwanini tunaamini takwimu za GGM na wenzake ni correct data kasoro zile za Acacia peke yao?

Your concern is about an empirical solution.

Kwa Case I ambayo ni kadhia kwenye sekta ya madini kwa ujumla... empirical solution ni kufanya special mineral production audit kwa kampuni ZOTE za madini nchini.

Awali ya yote, serikali ingeanza kutuma dodoso (legal questionaire) la kuwatega as if haifikirii kufanya kitu chochote kile dhidi yao! Questionaire ambayo baada ya kujaza, wangetakiwa ku-confirm kwa kutumia mwanasheria wao (company secretary) kwamba taarifa wanazojaza kwenye dodoso husika ni za kweli, kweli kabisa na zinaweza kutumika mahakamani dhidi yao ikionekana wamedanganya!

Questionaire hii unaijaza porojo za hapa na pale za kuficha lengo lakini main goal ikiwa ni kuwatega waelezee status na mazingira ya uzalishaji wa dhahabu over the past 5 years na hali ya uzalishaji kwa wakati uliopo!!

Kwavile status ya gold production over the past 5 years inafahamika na serikali kutokana na data zilizopo, I believe status ya uzalishaji kwa sasa wasingeonesha ipo tofauti sana na uzalishaji wa zamani ili wasije wakaibua hisia hasi!

Baada ya kupata hizi dodoso (walizoji-commit) zilizopewa nguvu za kisheria hata na wao wenyewe, kinachofuata ni Special Mineral Production Audit kwa kampuni zote zinazozalisha madini nchini.

Hii iwe ni participatory au inclussive audit... kwamba, kila upande uchague watu inaowaamini waingie kwenye audit team na sio yale mambo ya akina Mruma peke yao wanaenda kufungua makontena ya Acacia pasi na Acacia kuwepo kisha wanatarajia Acacia wakubali findings walizofanya wakiwa peke yao!

So, huku Government Team kule GGM Team kisha tunaanza kufanya special mineral audit ya GGM. Waombe Mungu kwamba findings za hii special mineral audit ifanane na takwimu za uzalishaji wao siku za nyuma.

Now let's assume past records zinasema GGM walikuwa wanazalisha kwa wastani tani 50 za dhahabu kwa mwaka! Lakini baada ya kufanya hii special audit ambayo na wenyewe wameshiriki, inaonekana status ya uzalishaji kwa sasa ina-reflect uzalishaji wao ni tani 500 kwa mwaka!

Sasa ikiwa hapo kabla walishaji-commit kwenye questionaire kwamba taarifa zote ni sahihi na mazingira ya uzalishaji kwa mwaka husika hayana tofauti sana na mazingira ya uzalishaji kwa miaka ya nyuma, kwanini basi serikali iamini uzalishaji wa tani 50 na sio tani 500 ambazo, na GGM wenyewe walishiriki kwenye kupata hizi findings?!

Kwanini hapo serikali isiamini miaka ya nyuma kulikuwa na udanganyifu wa kutisha na ndio maana uzalishaji ulikuwa unaonekana chini kabisa compared na special audt findings?

Ukifika hapo ndipo unakifanya kile kilichofanyika kwa Acacia!

Kama wataenda MIGA wakati walishaji-commit legally kwamba mazingira ya uzalishaji hayajabadilika basi itabidi huko MIGA wakaeleze ikiwa mazingira ya uzalishaji hayajabadilika, ni kwanini basi hapo kabla walikuwa wana-declare mavuno ya tani 50 huku special audit ambayo na wenyewe wameshiriki ikionesha ni uzalishaji wao ni tani 500! Kuna nini hapa katikati!!

Hapo kitakachofuata ni kudai chetu ambacho tumepigwa ambacho pia technically, na wenyewe wanakuwa wamethibitisha kwamba wametupiga!

Tukirudi Case II... Acacia Case, to be honest, naamini tumeshavurunda vya kutosha! Tumevurunda kwa sababu uchunguzi wa akina Mruma hauwezi kuwa na nguvu za kisheria kwa sababu ni wa upande mmoja.

Hata hivyo, si kwamba hawawezi kulipa kabisa... wanaweza kulipa endapo wanaona productive life span iliyobaki ni kubwa kiasi cha kuweza ku-offset kile watakacholipa!

Hata hivyo, lazima ulipaji wao watauweka katika sura ile ile ya "tunalipa in a good faith" na sio kukubali findings za akina Mruma ambazo itakuwa ni kama wanakiri walikuwa wanatuibia wakati hawakushiriki kwenye huo uchunguzi!

Lakini hata wakilipa; watakacholipa hakiwezi kufika hataTrilion 2 out of 450 na serikali hawatakuwa na namna zaidi ya kupokea!! Watalipa tofauti kabisa na stahiki yetu kwa sababu ya uzembe wetu!

Tumetaka tusitake, only solution ni ile ya "tusikose kabisa." And I hate to say this, hicho ndicho watakachofanya akina Kabudi! Watatoka mbele ya kamera na kudai baada ya majadiliano makali, hatimae Acacia wamekubali kulipa 500M.

Watataja 500M huku wakiacha kutaja kwamba Acacia "wamekubali" kulipa just in a good faith na pia kwamba, serikali nao wamekata shauri wachukue hiyo hiyo 500M kwa sababu, heri ya nusu shari kuliko shari kamili!

Lakini kwa upande mwingine, kuna wakati hapa niliweka Ripoti ya TMAA ikionesha gharama za smelter plant ni takribani 500M na kwa kuzingatia kiwango cha makinikia inayozalishwa, hiyo investment haiwezi kuwa commercially viable unless yanafanyika mambo fulani fulani!

Ripoti ile ilikejeliwa sana na "Wazalendo" wa JF huku wakisema bei za smelter hazifiki hata USD 25,000.

Nakumbuka Magu nae mwaka 2015 aliwahi kusema ni ukosefu wa akili makinikia kuipeleka Japan wakati hata sisi wenyewe tungeweza kujenga furnace zinazoweza ku-raise temperature to 1500 C, then BOOM... dhahabu hiyo hapo!!!
​

Binafsi nilifanya utafiti wangu binafsi na nikakuta zile gharama zilizotajwa na TMAA zinakaribia na ukweli!

Wale waliokuwa wanapinga na kuingia Google kisha kurudi na furnace za USD 25,000 walishindwa kutofautisha kati ya uchenjuaji wa copper concentrates unaolenga kuzalisha copper na uchenjuaji wa copper concentrates unaolenga ku-extract gold from other earth metals!

So, another empirical solution kwa issue ya Acacia ni ile ya "Kizalendo!"

Kwamba, kama kweli yale makinikia ya bandarini yana kiwango kikubwa cha dhahabu kiasi hicho, na kwavile hizi smelters ni USD 25,000 tu au hata JPM anaweza kutoa shule ya kujenga furnace zitakazoweza kupandisha joto kufikia nyuzijoto 1500, basi tupate hizo smelters za 25K (au za JPM) kisha tuchenjue sisi wenyewe hapa hapa!

Changamoto kama hiyo niliwahi kuitoa takribani mwaka mmoja uliopita lakini bado sijaziona furnace za Magu wala zile za 25K. Hapa wazalendo wanasahau tungeweza kuzalisha ajira nyingi sana!
 
Mkuu kwa hili uko sawa tulishadanganywa kulaliwa tusikubali ijirudie
Kwani mbona kwenye Dhahabu hatuna shida na mizozo nahawa jama Barick/Accacia. Shida tu naona iko kwenye Makinikia. Kwanini sasa tusikae nao tukaweka mgao mzuri wa makinikia ili next time tusigombane nao.
 
Habari ndiyo hiyo.... badili jina piga kazi, kwani watalaam wetu si wanajua? Mikataba si wanatia saini wao? Mbona makampuni mengi yanabadili majina? Shida ni kwa vikampuni vyetu vya kibongo..
Hili ndo linatoa maana ya Elimu Ni Ufunguo Wa Maisha.
 
Laiti kama tungejua Why kulikua na Acacia wala tusingesifia haya. Kwani hiyo migodi iliokua inamilikiwa na Acacia ilianza kuitwa Acacia wakati wa uanzishwaji wake!? NA kama jibu ni HAPANA, baada ya kuuziana na huyo mmiliki wa kwanza, je huyo mmiliki wa kwanza alilipa pesa za uuzaji wake wa HISA Tanzania!? Kitu kimoja kinacho tufanya Watanzania wengi tuwe tunadharauliwa sana hasa na wana siasa wa chama tawala ni uwezo wetu mkubwa wa usahaulifu. Sisi ni wasahaulifu hadi inatia KINYA!
 
Nadhani hoja hapa sio kuamini data za kina Prof. Mruma kwa kutumia thamani ya kampuni kwa sasa. Kumbuka kuwa kampuni imekuwa ikilipa gawio kwa wabia/wamiliki wake kutokana na faida iliyopata katika biashara zake.

Nadhani ingekuwa ni vizuri tukajua kuwa tokea hii kampuni ianze kufanya kazi nchini imepata mapato kiasi gani? Hiki nadhani ndio kigezo cha kujua ukweli wa hoja za Prof. Mruma kama zina uhalali katika hesabu. Kumbuka kwenye pesa hizo kuna riba na faini.

Ninakubaliana na wewe kuwa haiwezekani kulipwa pesa ambayo serikali inadai imeibiwa. Hii hata serikali inafahamu lakini wameamua kutumia namba hizo kama fimbo ya bargaining power.
 
Chige, mwaka 2017 walikuwa na reserves za Madini za thamani ya Pound 14Billion i think ni kama zaidi ya Usd20 Billion. Hapo bado hujaweka Machines za uchimbaji na Assets zingine. Nafikiri hiyo iliyotajwa bado ndogo wakishaungana ndo itazidi zaidi.
NI nani hao mkuu wangu? NI Acacia au Barrick Gold?

But all in all, ni reserve ya aina gani inayoielezea wewe?! Hoja yangu hii inatokana na, BoT kwa mfano, ukisikia wana gold reserve yenye thamani ya 50 Billion manake hiyo ni pure gold unayoweza kuiingiza sokoni any time!

Kinyume chake, kampuni za madini nazo huwa huwa wana-declare mineral reserves kwenye ripoti zao na kwa muktadha huu, huwa wana-declare gold reserves!

Lakini tofauti ni central banks and any other bank ambazo zinakuwa na pure gold iliyo tayari kuingizwa sokoni, hii ya kampuni za madini inaitwa probable and proven gold reserve. Hii inakuwa ardhini na bado haijachimbwa!

Probable gold reserve ni ile ambayo katika mazingira fulani fulani unaweza kuichimba dhahabu husika na uchimbaji huo ukawa ni commercially viable na proven reserve ni ile ambayo probability ya uchimbaji kuwa commercially viable ni kubwa zaidi compared to probable reserve!

That having said, kama utachimba dhahabu yote hiyo kwa mara moja kisha ukatoa gharama za uchimbaji, unakuta tunarudi kule kule!
 
The problem ni kwamba, kwa mazingira hayo ina maana tutalazimika kutumia audited finacial reports ambazo tayari nimeshataja hapo juu zinaonesha nini! Hizo dividends wanazolipwa wanahisa na zenyewe taarifa zake zipo kwenye hizo hizo audited financial reports ambazo hatuwezi kuzikwepa!

Hizi financial reports nimekuwa nikizisoma mara kwa mara... kwa mfano, 2012 to 2016 Financial Report ya Barrick Gold (Acacia ikiwa ndani) ni hii:


Nadhani unaona kama tutatumia financial reports tutakwama wapi! Hiyo inaonesha Gross Profit kwa miaka 4 mfululizo na ni mwaka mmoja tu ndipo gross profit ilifika angalau USD 5 Billion!

Kama ndivyo, tukiamua kuchukua mkondo huo, itakuwa imekula kwetu kwa 100% kwa sababu, ripoti hiyo ya Barrick ina-reflect what Acacia walichokuwa wanapata na kutulipa na kwahiyo itakuwa case closed... hatuna chetu!!

Lakini kama uchunguzi wa akina Mruma ungekuwa inclussive, ukiwahusisha na Acacia wenyewe, mosi, ndo kama nilivyosema hapo awali, Acacia wasingekuwa na grounds za kuikataa ripoti ya Mruma!

Na kama wasingekuwa na grounds za kuikataa, serikali kwa upande wake ingekuwa kwenye nafasi ya ku-discredit hizo financial records za akina Barrick kwa sababu, findings za serikali na Acacia wenyewe, zingekuwa zinaonesha udanganyifu mkubwa kwenye kiwango cha madini kwenye makinikia. Kama wote wame-confirm udanganyifu kwenye viwango vya madini, ina maana any financial reports zilizotokana na udanganyifu huo, na zenyewe credibility yake inakuwa questionable!

And remember, issue hapa haitakuwa kuiamini au kutoiamini report ya akina Mruma bali credility ya report yenyewe ambayo ndiyo zao la madai yetu! And to be honest, naogopa hizi sana hizi merger na acquisition za akina Barrick manake tusipokuwa cautious, tutashitukia tunayemdai doesn't exist!

Unaweza kuja kushitukia mwisho wa siku mmiliki mpya alinunua only assets za mdaiwa wetu ambae doesn't exist anymore and not her liabilities!
 
Kwa kiwango kikubwa ninakubaliana na hoja zako hasa nikichukulia kuwa biashara zao zinaendeshwa katika nchi nyingi ambazo bado zina tatizo la rushwa na mapungufu ya sheria nzuri za kuwabana.

Kama kwa wachimbaji wadogo tu wanaweza kukwepa kodi, kwa nini isiwezekane kwa makampuni makubwa yenye uzoefu na wataalam wazuri wa masuala ya kodi.

Kama rushwa haitafanyika na tukatanguliza uzalendo, nadhani kwa sasa tuna wataalam wazuri nchini wa kuweza kujua mapungufu ya sheria na namna ya kuziba udhaifu wa kisheria na pia kusimamia sheria.
 
Kama Nchi ina fedha kwa nini Serikali isiinunue Acacia na Mali zake na deni zetu ambazo tunawadai watuachie vifaa, alafu iwagawie wazawa wachimbe hiyo migodi alafu madini yauzwe kupitia wizara ya Madini na Fedha kuliko kuitwa kushauriana na wakoloni wa Madini? Watu wa Tarime,Geita,Shinyanga nk walitakiwa kuwa wataalamu wa Madini kwa kuwezeshwa..
 
Punguza mihemuko ili uweze kuelewa kinachosemwa! Ni wapi paliposemwa thamani ya Acacia ni USD 303 Million?!
 
Lisu kwa nini ulitudanganya kwamba tutashitakiwa MIGA ?

Ulikuwa unataka tuogope tuwaache Acacia waendelee kutunyonya?

Kwa hali hiyo Lisu hufai kabisa na sijui umekula maharage ya watu

Lissu Ana ajenda yake
 
Kwa kiwango kikubwa ninakubaliana na andiko lako.

Serikali inatakiwa isiyumbe kwenye hoja zake na pia kama ulivyoandik zitumike kama bargaining power katika makubaliano.

Kesi zilizofunguliwa mahakamani kwa baadhi ya wafanyakazi wa Acacia ni mojawapo ya shinikizo kwa kampuni kama fimbo katika mazungumzo.
 
Iko siku dharau hizi utaacha baada kuona tumelipwa

Wale maprofessa wametudharau sisi sana. Lakini sisi tunaoonyesha uongo wao ndiyo tunaonekana tuna dharau.

Pia, tunaweza tukalipwa lakini ni baada ya mwekezaji kupima na kuona ni kheri atupe kiasi fulani tunyamaze ili aendelee kufanya biashara. Sahau dola 190 bilioni, huo ni uongo na hoja yangu ni kwa nini tutumie wanataaluma kama maprofessa na kamishna wa TRA kusema uongo?

Hasara yake ni kwamba tutakuwa tumeitangazia dunia kwenye masuala ya uwekezaji na biashara sisi si waaminifu. Tunapoteza zaidi. Kama kamishna anaweza kukubambikizia deni lisilo halali ni nani atataka kufanya biashara kwenye mazingira hayo?

Leo hii ukimkamata mwizi, na una ushahidi wote kwamba unamdai dola bilioni 190 na ushahidi unao, kwa nini ukae nae mezani na ukubali dola milioni 300 ambayo ni chini ya asilimia 1 ya unachomdai? Huoni tatizo lolote kwenye hili?

Hii ni ishara ushahidi ule wa maprofessa ulikuwa batili na wanapaswa kuomba radhi kwa kuongea uongo. Uongo wa professa si sawa na mwanasiasa. Uongo wa professa nchi nzima tunaonekana wajinga.

Kuhoji kwetu hivi vitu tunaonekana tuna dharau na hatuna uzalendo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…