New Barrick Group kuinunua Acacia

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Baada ya Kampuni ya Barrick Gold kuungana na Kampuni ya Randgold Resources na kuwa kampuni inayoitwa New Barrick Group yenye thamani ya US$18.3 bilioni. Kwa sasa kuna taratibu zinazofanyika ili kuzinunua hisa zilizobakia za Acacia ambazo ni asilimia 36 zenye thamani ya US$303 milioni kwa hesabu iliyofanya Jumanne wiki hii.

‘’Baada ya kukamilisha kazi ya kuziunganisha kampuni za Barrick Gold na Randgold Resource, tutakaa na Acacia na Serikali ya Tanzania ili kumaliza tofauti zilizopo’’, Alisema Mark Bristow ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa New Barrick Group.

Acacia ilinukuliwa ikisema kuwa ilikuwa ikisubiri kupewa taarifa rasmi na Barrick kuhusu mazungumzo yake na serikali ya Tanzania.

Serikali ya Tanzania imekataa kukutana na Acacia kutokana na suala la ukwepaji wa kodi.

"Kama ilivyoshauriwa hapo awali, Barrick bado haijaipa Acacia mapendekezo ya ufumbuzi kamili wa migogoro ambayo Barrick ameweza kukubaliana na Serikali ya Tanzania licha ya majadiliano yao ya moja kwa moja yalifanywa mnamo Oktoba 2017," ilisema Acacia.

Katika mahojiano na Globe and Mail mnamo Septemba John Thornton, mwenyekiti mtendaji wa Barrick Gold, alisema Acacia "hakuwahi kulipia kodi ya mapato" kwa serikali ya Tanzania na njia bora ya kukabiliana na tatizo hili ilikuwa kupitia majadiliano na serikali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Randgold Resources ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa New Barrick Group, Mark Bristow aliliambia gazeti la Miningmx mnamo Oktoba 1 kwamba alikuwa na nia ya kuwekeza Tanzania. Alisema, "Je, sisi, kama Randgold, tunaenda Tanzania? Kabisa. Je! Tumefanya kazi na serikali ya Tanzania kama Randgold? Ndio, tumefanya "alisema.

Habari kwa lugha ya Kiingereza:

SOURCE: Bloomberg and Financial Times newspaper.
 
Baada ya Kampuni ya Barrick Gold kuungana na Kampuni ya Randgold Resources na kuwa kampuni inayoitwa New Barrick Group yenye thamani ya US$18.3 bilioni. .
Haya ndo yale niliyokuwa nayasema wakati ule! Hata baada ya "merger", New Barrick Group ndo hapo ina thamani ya USD 18.3 Billion.

Kitoto kimoja cha old Barrick tunakidai USD 190 Billion halafu bado kuna mtu anaendelea kuamini ipo siku tutakuja kulipwa! Bado kuna mtu anaamini data za akina Profesa Mruma!!

Technically, endapo Tanzania tutaweza ku-prove tunaibiwa na hivyo kuwa na haki ya kuzi-abuse a known world gold data, kinachoweza kufanyika katika kutenda haki labda Acacia kuwa dissolved kwa sababu audited books za Acacia na Barrick zinaonesha hazina hiyo thamani!

Malcom Lumumba
 
Kwa macho yetu tunaona kama hawa watu hawajuani na wanafanya biashara, lakini ukweli inaonesha wanaichezea nchi yetu kwa kubadili badili majina tu kwa nia ya kutuchuna madini yetu na mambo yakiwafika pabaya wachache kati yao wanarudi kwao kubadili jina na kurudi kama kampuni nyingne kuinunua iliyopo lakni ukweli ni kwamba hawa jamaa wakianza kupitia wakati mgumu wanabadili majina ya kampuni yao na wafanyakazi kubadilishana vituo nchi hadi nchi lakini sisi tunaona kuwa wameuziana ila lengo ni kuua matatizo na changamoto wanazokuwa wanazipitia.

Hapo kabla, ktk miaka ya 1985-90 kampuni hii ilikuwa na jina jingne (nimelisahau kidogo), baadae ndo likaaja barick gold mining, baadae tena likapita na kuja Acacia gold mine,sasa eti inarudi ile ile kwa muondoko mpya wa Barick group.
Daaaaahhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
Hapa shamba litaendelea kuwa la bibi tu hata tukivinba namna gani.
 
Lisu kwa nini ulitudanganya kwamba tutashitakiwa MIGA ?

Ulikuwa unataka tuogope tuwaache Acacia waendelee kutunyonya?

Kwa hali hiyo Lisu hufai kabisa na sijui umekula maharage ya watu
 

Kuna mzungu moja juzi akasema hivi "deni analodai Magufuli kwa Accacia ni Trip ya kwenda mwezini na kurudi" nilicheka sana. Lakini yote tisa ukweli mchungu ni kwamba hili deni haliwezekaniki kulipwa kabisa. Kibaya zaidi upande wa Serikali kumeshatokea mkanganyiko mkubwa sana kwenye TAKWIMU.

Nadhani njia pekee na ya kuweza kwenda mbele vizuri ilikuwa ni kupitia upya hii mikataba katika Sovereign Right ili kuzuia upigaji mwingine. Ila hii ya kuendelea kusaka wachawi sidhani kama itafanikisha kitu.

Mzee hii mikataba mipya nchi iwe inapiga asilimia kubwa bila kulaliwa. Japo tukiangalia katika mtazamo mpana unadhani hao Barrick bila kukarashwa hivi wangekubali kukaa meza ya mazungumzo na kuwa na heshima ??

Mimi nadhani katika hili, deni lisifutwe bali ili litumike kama ya Bargaining Chip kwenye mikataba ijayo ili kuzuia kulaliwa.....
 
Wajinga ndio waliwao, hela yenu mmepewa sasa.
Mpaka sasa lengo lisiwe kupewa hela tu, maana hata kama wanalikubali hilo deni, hawatakuwa na uwezo wa kulilipa yaani its simply a Bad Debt. Muhimu ni kukaa kwenye mazungumzo na kuangalia jinsi gani nchi yetu inaweza kufaidika na huu uwekezaji bila kulaliwa tena kiboya-boya maana hata kama takwimu ziwe vipi bado hawa jamaa walikuwa wanatupiga sana. Kusema walikuwa hawapigi tutakuwa waongo.....
 

Mkuu sijakuelewa bado...unamaanisha unataka kuona Mwizi anaiba sawa na kile anachomiliki au una maana gani??
Sisi tunawadai kile tulichoona wanatuibia,maswala ya accacia wanathamani ya kiwango kipi sisi haituhusu
 
Kuna watu walifikiri Magufuli akiingia madarakani hakutokuwa na vipindi vigumu vya kupitia.....sasa mambo yanaanza kukaa sawa na Mungu amjalie afya njema na Moyo Wa ujasiri zaidi ya ule aliokuwa nao mwanzo.
Tutalipwa lini tril 495???
 
Mtu aliyekupa shule anajua uwezo wako, madini babu zetu walikuwa hakiyachezea tu na hawakujua umuhimu wake, mzungu akaja akatufundisha tukayafahamu.
Hatutawaweza hawajamaa mwishowe tutainua mikono
 
Fanya kazi Mkuu....hata zikilipwa hutopewa wewe mkononi Bali zitaingizwa kwenye miradi ya maendeleo
Unanisaidia kulisha familia mpaka uniambie nifanye kazi?
Akili zenu sijui mmezigawa wapi?Kwani tunahoji juu ya deni la taifa,kwani hizo pesa nitakuja kulipa mimi moja kwa moja?Hapana,ni kodi ninayokatwa ndio itakuja kulipa!Hivyo hata shughuli za maendeleo zikifanyika ni faida kwangu,wengine baadhi ya miradi ikifanyika tunaingiza pesa kupitia tenda tunazopata!!!
So lazima tufuatilie,tunalipwa lini?Au kama hatulipwi tujue!
 
Hii mikataba bila kuwekwa wazi tutaendelea kuchezea za mbavu tu maana aina za viongozi waliosaini ile mikataba ya mwanzo ndiyo bado tunao hadi leo hii
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…